Kama Bunge ni chombo cha kutunga sheria kwanini wabunge wengi sio Wanasheria?

Kyambamasimbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
762
Reaction score
1,597
Jamani wanajf habari. Jamani samahani naomba ufafanuzi Kama tunasema Bunge Ni chombo Cha kutunga sheria kwa Nini wabunge wengi sio Wanasheria?

Watungaje sheria wakati hawajui sheria? Mimi nafkiri kungekuwa na vigezo maalum vya kuwa mbunge kigezo mojawapo angalau mtu awe na certificate ya sheria.

Naomba kuwasilisha.
 
Wazungu wanasema you get it wrong.

Kazi ya wabunge ni kupitisha sheria zilizopendekezwa na serikali lakini pia kama kuna mbunge ana hoja na ina maslahi kwa umma anapendekeza itungiwe sheria ili utumike. Sio lazima aitunge yeye, akishatoa hoja ikapokelewa vizuri na wabunge wenzake basi huilazimisha serikali kutunga hiyo sheria.

Ndio maana bungeni kuna muwakilishi wa serikali kwa upande wa sheria ambae ni mwanasheria Mkuu wa serikali.
 
Ok Asante kwa ufafanuzi mzuri lakini huwa naona baadhi yao tangu waende mjengoni Ni kusinzia tu mkuu mpaka Miaka mitano inaisha
 
Wazungu wanasema you get it wrong.

Kazi ya wabunge ni kupitisha sheria zilizopendekezwa na serikali lakini pia kama kuna mbunge ana hoja na ina maslahi kwa umma anapendekeza itungiwe sheria ili utumike. Sio lazima aitunge yeye, akishatoa hoja ikapokelewa vizuri na wabunge wenzake basi huilazimisha serikali kutunga hiyo sheria.

Ndio maana bungeni kuna muwakilishi wa serikali kwa upande wa sheria ambae ni mwanasheria Mkuu wa serikali.
Hujaelewa mada, utapitishaje kitu ambacho hukijui?

Ni bora mtunga sheria awe hajui sheria kuliko mpitisha sheria awe hajui sheria.
 
Wabunge ni Wawakilishi wa Wananchi, na sio wawakilishi wa Wanasheria.
 
Hujaelewa mada, utapitishaje kitu ambacho hukijui?

Ni bora mtunga sheria awe hajui sheria kuliko mpitisha sheria awe hajui sheria.
Mkuu, sheria hazitungwi kwa ajili ya wanasheria bali zinatungwa kwa ajili ya wananchi bila kujali kazi zao. Zinatungwa na nani? Zinatungwa na wananchi wenyewe (wabunge).

Labda kama unachoongelea ni uandishi wa sheria, hapo ndio lazima uwe mtaalamu wa sheria. Ila kupanga kuwa kufanya jambo fulani itakuwa ni kosa, hakuhitaji utaalamu wa sheria bali makubaliano yenu kama wananchi. Ni kama baba anavyopanga muda wa watoto wake kurudi nyumbani
 
Wazungu wanasema you get it wrong.

Kazi ya wabunge ni kupitisha sheria zilizopendekezwa na serikali lakini pia kama kuna mbunge ana hoja na ina maslahi kwa umma anapendekeza itungiwe sheria ili utumike. Sio lazima aitunge yeye, akishatoa hoja ikapokelewa vizuri na wabunge wenzake basi huilazimisha serikali kutunga hiyo sheria.

Ndio maana bungeni kuna muwakilishi wa serikali kwa upande wa sheria ambae ni mwanasheria Mkuu wa serikali.
Sawa, lakini, sheria imetungwa na msomi mwanasheria, halafu kwenye kujadili itumike au la, na itumikeje, eti anayejadili hayo eti awe anajua kusoma na kuandika tu..!! Yaani anayepitisha au kukwamisha kilicholetwa na mwanasheria ni yule anayejua kusoma na kuandika tu..!! BOOLSHIT
 
Mkuu, sheria hazitungwi kwa ajili ya wanasheria bali zinatungwa kwa ajili ya wananchi bila kujali kazi zao. Zinatungwa na nani? Zinatungwa na wananchi wenyewe (wabunge).

Labda kama unachoongelea ni uandishi wa sheria, hapo ndio lazima uwe mtaalamu wa sheria. Ila kupanga kuwa kufanya jambo fulani itakuwa ni kosa, hakuhitaji utaalamu wa sheria bali makubaliano yenu kama wananchi. Ni kama baba anavyopanga muda wa watoto wake kurudi nyumbani
Zinatungwa na wananchi wenyewe (mbunge).. mwisho wa kunukuu.. Mbunge wa la saba B
 
Ndio imepita hiyo aisee - wananchi wenye madigrii wanasema hawataki kujihusisha na siasa, hawashiriki hata kupiga kura matokeo yake tunapata wabunge wa darasa la pili halafu wananchi wenye madigrii wanaanza kubeza wabunge wao (maana mbunge akichaguliwa anakuwa wa wote).. na wanaanza kulalamika kuona wanapangiwa maisha na wasomi wa darasa la pili
 
Mtoa mada anayo hoja, ila Wachangiaji wamekariri.....!
Hoja yake imeeleweka. Mwaka 2014 ni Zitto na Lissu walikuwa wanaweza kuchambua miswada kisheria kwa kuchambua madhara ya zile , 'au' 'na' nk.

Mleta mada anataka wabunge wawe na uelewa wa hivyo kwenye sheria, lakini hili sio muhimu kihivyo sababu sheria zinatungwa na kundi fulani kuratibu na kuongoza shughuli zao, ila wakishatunga hizo sheria, watamtafuta mwanasheria ili aziandike kisheria. Kina mama kwenye vicoba wanaposema mtu akichelewa kuleta marejesho atalipa na faini, hiyo ni sheria lakini wao sio wanasheria. Kwenye katiba ya kikundi chao watamtafuta mwanasheria aliweje jambo hilo kwa lugha ya kisheria. Ndio hivyo kwa wabunge sasa
 
Mimi nadhani jambo la msingi ni kwamba tunatakiwa tujue maana ya sheria, dhumuni la sheria, na utaratibu wa utungwaji wa sheria.......

Sheria zinaanzia ngazi ya familia kutoka kwa mkuu wa familia kwa faida ya familia....

Kwa mfano kama wewe unavyoamua kutunga sheria ndogo ndogo nyumbani kwako na kuzisimamia kwa adhabu ulizoziainisha kwa atakayevunja.......

Huu ni mjadala mzuri unaohitaji mawazo na michango yakinifu.....
 
Sawa, lakini, sheria imetungwa na msomi mwanasheria, halafu kwenye kujadili itumike au la, na itumikeje, eti anayejadili hayo eti awe anajua kusoma na kuandika tu..!! Yaani anayepitisha au kukwamisha kilicholetwa na mwanasheria ni yule anayejua kusoma na kuandika tu..!! BOOLSHIT
Bunge ni la wananchi. Wabunge ni wawakilishi tu. Yaani ilitakiwa huyo mwanasheria ailete kwetu wananchi wote tuijadili maana sisi ndio tutaitumia, kwa kuwa wote hatuwezi kwenda bungeni ndio mwakilishi wetu (mbunge) anajadili kwa niaba yetu. Hata hivyo bunge hutoa nafasi ya wananchi kutuma maoni, japo taarifa hiyo huwa ya kificho na ya muda mfupi sana
 
Siyo Sheria zote huanza hivi, nyingine huletwa tu na Serikali, kwa mfano kodi ya miamala ya bank ilianzia wapi?
 
Mkuu ipo hivi, kwanza Bunge lina vitengo/ofisi tofauti tofauti. Na sio kweli kwamba wabunge wanatunga sheria. Wabunge hawatungi moja kwa moja sheria.

Japo ni kweli wabunge wengi sio wanasheria japo wanafanya sehemu kubwa na uwepo wa sheria zetu Tz.

Sheria kabla ya kuwa sheria huwa zinakuwa miswada. Sasa ni nani mtunga Mswada?. Wapo watu wawili wa kwanza ni wizara husika mfano sheria ya makosa ya mtandaoni ni wizara inayohusika na mawasiliano.

Mtu wa pili anayeweza kuleta mswada ni mbunge binafsi, yaani mfano mbunge wa jimbo lenu anaweza akaja na mswada bungeni. Ila hadi leo hakuna sheria iliyotokanana njia hii ya pili.

Sasa baada ya mswada kujadiliwa na baraza la mawaziri na kupewa baraka na raisi ndio huo mswada sasa unaletwa bungeni ambapo unaweza kuletwa na waziri/naibu waziri au Mwanasheria Mkuu wa serikali ambapo utasomwa bungeni.

Haya, sasa hapa ndio wabunge sasa wanaingia ndani kwenye kufanya mswada kuwa sheria, kumbuka wao hawajatunga huo mswada.

Sasa kwanini waupitishe?, wanapataje kuufahamu huo mswada kama unafaa kuwa sheria ili hali wao sio wanasheria?

Ipo hivi, bungeni kuna mtu anaitwa Mwanasheria wa Bunge 'PLC' Huyu ndio anayewaandalia wabunge maelezo juu ya sheria husika na kama mbunge hajaelewa huyu ndio wakumuelewesha huyo mbunge.

Hapa usimchanganye Mwanasheria wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali hawa ni watu wawili tofauti kabisa, japo huyu Mwanasheria wa Serikali kunamuda anaombwa atoe ufafanuzi wa jambo la kisheria kwa wabunge ila hayo ni makosa sababu sio kazi yake. Yupo kwenye hiyo kazi ambaye ni Mwanasheria wa Bunge ambaye kimsingi ndiye Mwanasheria wa Spika wa Bunge pia.

Mchakato wote huu unaweza kuupata kwa Kusoma Kanuni za Kudumu za Bunge.

Google utazipata hizo kanuni.
 
Sawa, lakini, sheria imetungwa na msomi mwanasheria, halafu kwenye kujadili itumike au la, na itumikeje, eti anayejadili hayo eti awe anajua kusoma na kuandika tu..!! Yaani anayepitisha au kukwamisha kilicholetwa na mwanasheria ni yule anayejua kusoma na kuandika tu..!! BOOLSHIT
Wabunge wanafafanuliwa hizo sheria na wanasheria wa bunge, kumbuka kuwa bunge ni mhimili wa dola wenye ofisi nyingi ndani yake sio wabunge pekee yao. Kuna wanasheria wa bunge, kuna waandishi wa sheria, kuna raisi na hao wabunge sasa. Usishangae raisi ni sehemu ya Bunge.
 
Ndio imepita hiyo aisee - wananchi wenye madigrii wanasema hawataki kujihusisha na siasa, hawashiriki hata kupiga kura matokeo yake tunapata wabunge wa darasa la pili halafu wananchi wenye madigrii wanaanza kubeza wabunge wao (maana mbunge akichaguliwa anakuwa wa wote).. na wanaanza kulalamika kuona wanapangiwa maisha na wasomi wa darasa la pili

Watu wenye elimu wanajihusisha na siasa, lakini mfumo umeharibika toka mwanzo, wanaofanikiwa kushinda ni wenye hila zaidi kuliko wenye uwezo.
 
Bunge ni la wananchi. Wabunge ni wawakilishi tu. Yaani ilitakiwa huyo mwanasheria ailete kwetu wananchi wote tuijadili maana sisi ndio tutaitumia, kwa kuwa wote hatuwezi kwenda bungeni ndio mwakilishi wetu (mbunge) anajadili kwa niaba yetu. Hata hivyo bunge hutoa nafasi ya wananchi kutuma maoni, japo taarifa hiyo huwa ya kificho na ya muda mfupi sana

Hakuna sheria yoyote inatungwa na bunge, bali sheria zinatungwa na serikali kisha zinapelekwa bungeni kupata uhalali wa hadaa.
 
Back
Top Bottom