Kama Bunge ni chombo cha kutunga sheria kwanini wabunge wengi sio Wanasheria?

Kama Bunge ni chombo cha kutunga sheria kwanini wabunge wengi sio Wanasheria?

nje ya mada,CCM kuweni silias,hivi kweli mnapitisha darasa la saba ndani ya chama kuja kuwa wabunge wa wananchi?,hata kama mnapita bila kupingwa basi tuleteeni wabunge wenye upeo mpana sio hawa kina Babu Tale!
 
Katiba mpya yaweza kuwa dawa mujarabu ya matatizo haya!

Tuwakilishwe na wasomi bwana.Tatizo tunapenda kujificha ktk kivuli cha ujamaa!
 
Bunge ni la wananchi. Wabunge ni wawakilishi tu. Yaani ilitakiwa huyo mwanasheria ailete kwetu wananchi wote tuijadili maana sisi ndio tutaitumia, kwa kuwa wote hatuwezi kwenda bungeni ndio mwakilishi wetu (mbunge) anajadili kwa niaba yetu. Hata hivyo bunge hutoa nafasi ya wananchi kutuma maoni, japo taarifa hiyo huwa ya kificho na ya muda mfupi sana

Bunge linapaswa kuwa la wananchi, lakini kutokana na katiba mbovu, na siasa chafu, unakuta bunge ni la chama kinacholazimisha kukaa madarakani. Kinacholindwa ndani ya bunge sio maslahi ya wananchi kwanza, bali ni serikali ya chama chao.

Ni nadra bunge lililotokana na wizi wa kura kulinda maslahi ya wananchi kwanza dhidi ya mahitaji ya serikali yao. Hapo ndio unakutana na miswada ya sheria kandamizi ikipita ili kulinda maslahi ya serikali na chama kimoja.
 
Uko sahihi kwa asilimia 70
Jamani wanajf habari. Jamani samahani naomba ufafanuzi Kama tunasema Bunge Ni chombo Cha kutunga sheria kwa Nini wabunge wengi sio Wanasheria?

Watungaje sheria wakati hawajui sheria ??Mimi nafkiri kungekuwa na vigezo maalum vya kuwa mbunge kigezo mojawapo angalau mtu awe na certificate ya sheria.

Naomba kuwasilisha.
 
Bunge bora lazima liwe na idadi kubwa ya wanasheria wabobevu.
 
Ok Asante kwa ufafanuzi mzuri lakini huwa naona baadhi yao tangu waende mjengoni Ni kusinzia tu mkuu mpaka Miaka mitano inaisha
Ndio maana tozo zinakuwa sehemu ya maisha yetu.
 
Bunge bora lazima liwe na idadi kubwa ya wanasheria wabobevu.
Hapana, bunge bora linaitaji balance ya wabunge kutoka chama tawala na upinzani na spika aliyekomaa kisiasa.

Ndio maana hadi leo bunge la Marehemu Sitta ni mfano wa bunge bora kuwahi kutokea Tz.
 
Back
Top Bottom