Tanzania ni bwana mdogo hapa East Africa.
Miundo-mbinu, lugha, watangazaji, matangazo ya kibiashara, promotion wapo kimya kimya kimataifa hawajimwambafai kama wenzetu wa Uganda na Kenya kuhusu uwezo wa kuanda AFCON 2027.
Habari zote za AFCON 2027 zinatolewa Uganda na Kenya kwa ki English sisi huku tunasumulia ujenzi wa viwanja kwa kiSwahili kwa jumuiya ya kimataifa, hivyo hakuna habari zozote kwa kiEnglish zitokazo Tanzania zilizoandaliwa na waTanzania kuelezea nchi ilivyo tayari mbali ya mpira malazi watalala wapi, wataburudika vipi, mawasiliano ya TEHAMA ni rahisi kiasi gani, usafiri wa ndege mabasi maboti nchini upo vipi. Matangazo ya beer, usafiri, malazi kwa kiEnglish ? Hakuna habari hizo mtambuka kusapoti uwenyeji wetu ili mechi ya fainali ifanyike Tanzania
Wapenzi wetu wa mpira ni wengi ila mahojiano yao yote ni kwa kiSwahili hakuna kijiwe mtaani wala studio katika kituo cha televisheni wala online wanaoendesha mijadala kwa kiEnglish mashabiki wakaelewa Tanzania kupo vipi kimpira na masuala mtambuka.
Hakuna kiEnglish Azam TV, Uhuru FM, Wasafi wala Clouds Media n.k Matangazo ya kibiashara yaliyosukwa Tanzania kwa kiEnglish hakuna, corporate CEO wanaoongea kiEnglish hawapo ktk TV Stations main media wala Online media. Wote wanatema kiSwahili muda wote hata katika mikutano ya kimataifa inayofanyika Tanzania iwe Arusha, Dar es Salaam na Zanzibar hadi wanaohudhuria wanaumia masikio kwa kuvaa headphones wakati Tanzania lugha ya kiingereza ni lugha rasmi ya biashara, mahakama na serikali...
Ushawishi / Lobbying katika masuala ya kimataifa Tanzania inategemea hisani haina juhudi kimataifa kuji brand
View: https://m.youtube.com/watch?v=fPnSlGBfqGY&pp=ygUOU2hhYmlraSAgU2ltYmE%3D