Pre GE2025 Kama CCM Itamsimamisha Rais Samia 2025, Mnaonaje Freeman Mbowe Awe Mgombea wa Upinzani? Atapiga Ndege 3 kwa Jiwe Moja, Atavuna Wabunge Wengi ila...

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Webg
wengi wanakiri CCM walishindwa vbaya sana ule uchaguzi ila ndio hivyo mabavu.

CCM kura za wananchi hawezi kushinda yaani na hawezi kukubali .
Kwenye mabavu atashinda ila sio kura za wananchi
 
Um
Umesahau kuweka namba yako teuzi kenge wewe
 
Mbona Mbowe hana degree atagombea VIP?
 
Ni ajabu wafuasi wa chama Cha mboga mboga kujipa uhalali wa kutoa ushauri kwa vyama vipinzani hii ipo Tanzakiza tu.

Hakika unafiki ni sehemu ya maisha ya mwafrika.
 
Bila tume huru wala katiba mpya siwezi kuona huo utakua ni uchaguzi bali upuuzi mkuu wa kila baada ya miaka 5.

CHADEMA wajitathmini itakua ni ujinga wa kwenda kwenye mechi ambayo referee ana hisa nyingi katika timu hiyo wanayoenda kucheza nayo, kwenye hili siungi mkono hata kidogo.
 
Wanabodi!
Hao ndege 3 ambao Freeman Mbowe atawatungua kwa jiwe moja ni ndege gani hao?

Paskali
Hao ndege 3 ambao Freeman Mbowe akiamua kugombea urais wa 2025 kama mgombea wa umoja wa wapinzani
  1. Kufuatia kuvunjika kwa maridhiano, kati ya CCM na Chadema, hii maana yake ni hakuna tena kugawana nusu mkate, hivyo Freeman Mbowe asipogombea urais angegombea ubunge jimbo la Hai, nusu mkate ndio ingemrudisha Mbowe bungeni, bila hiyo nusu mkate, then uchaguzi wa 2025 utakuwa kama ule wa. 2020, hivyo kugombea urais ndio the best honorable execuse ya kutogombea jimbo la Hai.
  2. Freeman Mbowe na Rais Samia, wanajuana vema, Mbowe alipofutiwa kesi ya ugaidi, break yake ya kwanza ikawa ni Ikulu, na Chadema ilijuwa inakabiliwa na hali fulani, mara ghafla Chadema mambo yake yakawa super, mara wakawa na uwezo wa kufanya kikao cha Baraza Kuu, mara viongozi wakaanza kupiga trips za ulaya, Mbowe akawa haeshi Ikulu. Hivyo Freeman Mbowe akimchalleng Samia, then it's a clash of titan, hivyo Freeman Mbowe atamtikisa Samia na upinzani utavuna kura nyingi na kupata wabunge na madiwani wa kutosha.
  3. Kufuatia Freeman Mbowe ku overstay kwenye Uenyekiti wa Chadema, kugombea urais kutampa Freeman Mbowe an honorable exit.
Paskali
 
Tanzania hakuna uchaguzi, bali Kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura. Mtu mjinga, au anayefaidika na chaguzi hizi za kihayawani ndio atajitokeza kupiga kura kwa muundo huu wa uchaguzi. Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio tutapata mabadiliko ya kweli.
 
Tanzania hakuna uchaguzi, bali Kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura.
Naomba niheshimu maoni yako
Mtu mjinga, au anayefaidika na chaguzi hizi za kihayawani ndio atajitokeza kupiga kura kwa muundo huu wa uchaguzi.
Nitanote idadi ya wajinga na mahayawani kisha nitasema kitu.
Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio tutapata mabadiliko ya kweli.
Watanzania ni watu poa sana, sio watu wa fujo na machafuko, na jeshi la Tanzania ni JWTZ sio jeshi la kufanya mapinduzi!, hivyo kama unasubiri mabadiliko ya machafuko ama mapinduzi ya kijeshi, then utasubiri sana!

P
 
Machafuko ama mapinduzi kutokea hayo mambo mengine, lakini ndio njia pekee zitakazoleta mabadiliko ya kweli.Mazombie tu ndio watajitokeza kupiga kura kwa mazingira hata. Subiri uone chaguzi zetu zitakavyokuwa na idadi ndogo ya wapiga kura ambayo haijawahi kutokea. Hakuna atayekuwa na muda wa kushiriki chaguzi za kipuuzi.
 
Shida ni kuwa hata wakijitokeza wachache kupiga kura, mwisho wa siku kuna maarifa yatafanyika kujazia kura.... wala hutajua zimetokea wapi... ila utaambiwa walijitokeza wananchi wa kutosha na matokeo ndio hayo 99% ushindi.
Labda ziwekwe camera kwenye vituo vya kupiga kura vinginevyo hakutakuwa na jinsi ya kuhakiki...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…