Ungepitia katiba kwanza kabla ya kutoa maoni haya.
40.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote ambaye ni Rais anaweza kuchaguliwa tena kushika kiti hicho.
(2) Hakuna mtu atakayechaguliwa zaidi ya mara mbili kushika kiti cha Rais.
(3) Mtu aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar hatapoteza sifa za kuweza kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa
sababu tu kwamba aliwahi kushika madaraka ya Rais Zanzibar.
(4) Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.
Ibara ya 37(5) inayorejelewa hapo kwenye ibara ndogo ya 4 inasema hivi:
(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu
kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwakutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Raisataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindicha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopunguaasilimia hamsini ya Wabunge wote.
Rais Samia kachukua madaraka mwezi March 2021, Magufuli alichaguliwa na kuapishwa November 5, 2020, hivyo amekuwa rais kikatiba miezi 4 na siku 17 assuming alikufa tarehe 17 March 2021. Kwa hiyo Rais Samia ana miaka 4 na miezi 8 na siku 13 za kutawala, kipindi ambacho tayari kinazidi muda uliotajwa katika ibara ndogo ya 4 hapo juu. Kikatiba hiki ni kipindi sawa na miaka 5 na hivyo Rais Samia ataruhusiwa (kama atataka) kugombea kipindi kingine kimoja tu.
Nashauri watanzania tuisome katiba yetu hata kama ni mbovu kwa sababu ndiyo inayotuongoza kwa sasa.