Kama CHADEMA hawakuwapitisha Mdee na wenzake kwanini hawafungulii kesi ya kugushi?

Kama CHADEMA hawakuwapitisha Mdee na wenzake kwanini hawafungulii kesi ya kugushi?

Kwa covid kuna ngonjera ndiomana unaona mapichapicha.
Kikulacho kinguoni mwako kunamtu ndani ambae anayumbisha dishi ndiomaana chenga haziishi.

Anawachora tu.
Sasa hayo mapicha ndugu yangu yanatokea wapi?
Katiba ya nchi inatamka wazi kabisa ili uwe mbunge lazima utokane na chama cha siasa.chama kimekufukuza uanachama kwa mujibu wa taratibu zake. Anatokea mpuuzi anasema ulikosea kuwafukuza hivyo hajitambui ( ndugai) chama kinafuata hatua inayofuata bado watu wapo bungeni yule bibi anasema anangoja maamuzi ya mahakama . Mahakama yanaamua bado wapo bungeni.
Nani anacheza sarakasi hapo???
Huwezi kwenda mbinguni bila kufa na huwezi kuwa shekhe kama siyo muislamu
 
..kwa kumbukumbu zangu Dr.Mashinji aliondoka muda mrefu kabla ya uchaguzi.

..Dr.Mashinji aliondoka wakati kesi ya maandamano ya uchaguzi mdogo wa Kinondoni ikiunguruma.

..Na Dr.Mashinji alifungwa wakati akiwa tayari ni mwana-Ccm.

..John Mnyika ndiye Katibu Mkuu aliyesimamia uchaguzi mkuu wa 202O.

NB:

..Kama Kamati Kuu ya Cdm haikuteua wabunge wa Viti maalum.

..Na kama Katibu Mkuu wa Cdm amekana kujaza fomu za uteuzi.

..Na kama Tume haijatoa ushahidi kwamba imepokea fomu za viti maalum toka Cdm.

..Itoshe kusema Halima na wenzake walikwenda bungeni wakaapishwa bila kuthibitishwa na Cdm na kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi.

Cc Tindo, Erythrocyte

Kama jambo hili lilifanywa kwa hila, uliyosema yote katika Nota Benne yanawezekana. Ninaona wabunge wakitoshwa na NEC pamoja na Mahakama, kuliko njia za hila kuthibitishwa katika hadhara.
 
Kama jambo hili lilifanywa kwa hila, uliyosema yote katika Nota Benne yanawezekana. Ninaona wabunge wakitoshwa na NEC pamoja na Mahakama, kuliko njia za hila kuthibitishwa katika hadhara.

..waliofanya hila hiyo, wana watu wao kila mahali kuanzia mahakamani, bungeni, mpaka hawa watetezi wao hapa JF.
 
Kwenye civil case hulazimiki kuitika wito wa mahakama kama unaamini utetezi wako hautabadili outcome ya shauri. Kwenda kutoa utetezi ni kupoteza muda. Kama ni kusema Mdee na wenzake sio wanachama wa CDM, mmeshasema zaidi ya mara elfu moja!

Ndio wameenda na mahakamani kusema mara ya elfu moja na moja. Au unaumia?
 
Back
Top Bottom