Jamaa mmoja kaniambia kuwa kufungiwa kwa radio imani kumeondoa nafasi ya kujua mawazo ya waislamu yakoje, maana mtu unena yaujazayo moyoni mwake. hatari iliyopo ni kuwa sasa itakuwa vigumu kujua wanawaza nini? mtu mkimya siku zote ni shujaa sana bali anayepiga kelele ni dhaifu. mfano adui anayekufukuza usiku kimyakimya ujue atakuua, lakini anayepiga kelele sio muuaji. taifa kubwa na hodari kwa vita ni Isareli, na siri kubwa yao ni watu wa kunyamaza, yaani wa siri kali. mfano ni wale 10 walivyomuuza Yusufu waliyunza ile siri zaidi ya miaka 20 wakisema kuwa Yusufu kaliwa na wanyama wakali. Nafikiri Radio ingekuwa ni fursa nzuri kwa kuueleza uzuri wa dini yako ili wengine wavutwe, na sio ubaya wa dini ya mwenzako. kinachokupa ubora sikuzote ni ule uzuri wako na si ubaya wa mwenzako.
Anyway nimalizie kwa kusema kwa hili hata wakifunguliwa radio Imani na Radio Neema, bado ule umuhimu wao wa kueleza uzuri wao umechafuka, hivyo ni vigumu kufikia malengo yao ya kuwavuta wengine wa dini tofauti. Naam kurudishwa kwao ni sawa na kuuziwa soft copy na sio hard copy