Juzi kati nilikuwa nasoma majina ya Wachezaji walioitwa kwenye Timu ya Taifa ya Zambia na Kocha Mkuu wa timu hiyo Bw. Micho. Nilistaajabu nilipoona jina la mchezaji na kiungo pendwa wa ligi yetu kutokuwemo kwenye orodha ya wachezaji wa timu hiyo. Pia, kiungo mwingine fundi Larry Bwalya naye hakuwemo kwenye orodha hiyo. Nikajiuliza mpira wetu una tatizo gani?
Iweje leo kiungo tunayemwona kuwa asipokuwepo kwenye mechi ya Simba na timu nyingine tuanona kama hakuna timu, leo anakosekana kwenye timu yake ya taifa. Kwa kweli sikuyaamini macho yangu kuhusu hilo. Chama huyu huyu aliyeimpandishia dau la kumsajili timu yake ya Simba baada ya kutakiwa na mahasimu wao Yanga anakosa hata kuwa kwenye wachezaji wa akiba (Reserve)?
Nilipoendelea kushangaa nikakutana na mchambuzi mmoja mahiri alikuwa akieleza kuhusu ubora na udhaifu wa timu ya Simba inapocheza uwanjani. Kwa kumnukuu mchambuzi huyo alieleza kuwa "Timu ya Simba ni bora kwa kuchezea mpira hasa wa pasi fupi za kufurahisha mashabiki (wenyewe wanaita pira biriani) lakini ni dhaifu ikikutana na timu zinazocheza mpira wa nguvu".
Akaendelea kusema ubora wa Simba unamtegemea zaidi Cloutus Chama, ingawa naye hana uwezo wa kucheza mpira wa nguvu. Sehemu kubwa ya mpira anaocheza Chama anatumia unyumbufu wa mwili wake kuwadanganya wapinzani wake kwa vyenga vya hapa na pale.
Hivyo, kama taifa yatupasa tujitathmini kuhusu Ubora wa Ligi yetu ambayo ina wachezaji wanaoimbwa midomoni kama Chama na wengine.
Mkuu,, kwenye inchi ya watu vipofu ikitokea mtu mwenye Jicho moja,,
huwa mfalme..
Chama nilishagunduwa muda mrefu hakuna kitu mle.
Wachezaji wengi wa Malawi,Zimbabwe, Zambia, Botswana, Mozambique, Congo,,Lesotho,Swaziland.. Ghana,Nigeria..
Dreams zao ni kucheza south Africa..
Na ukiona tupo nae huku Africa mashariki ,,elewa bado hajafikia viwango vya south Africa..
Tatizo bongo tuna overrate wachezaji wa nje,,na kuwapa mishahara minono,,huku tuki wa underrate wachezaji wetu wazawa kwa kuwapa mishahara kiduchu..
Pamoja na viwango vyao kufanana uwanjani..