Kama Diamond anashindwa kumsitiri baba yake kwenye ukata utajiri wake una faida gani?

Kama Diamond anashindwa kumsitiri baba yake kwenye ukata utajiri wake una faida gani?

Siyo yeye Diamond bali huo ni mkwara wa mama yake, yaani dogo kanunua ugomvi wa wanandoa. Pia unaweza kuta financials zote mama ndiye muamuzi, so kijana hapaswi kulaumiwa, baba anapaswa akapige magoti kwa mkewe ili yaishe asaidiwe.
 

Attachments

  • IMG-20201221-WA0053.jpg
    IMG-20201221-WA0053.jpg
    69.4 KB · Views: 2
  • IMG-20201221-WA0023.jpg
    IMG-20201221-WA0023.jpg
    69 KB · Views: 2
Diamond mnamlaumu bure..sumu aliyomezeshwa ni mbaya sana...na uskute kashaambiwa ukimsaidia tu babako nakupa laana...kama ungekua ww ungefanya na laana ya mama ni kali sana!?

Ogopa sumu za akina mama type ile
 
Bora akahonge kuliko kumsaidia yule mzee asiyeridhika. Kuna kipindi akashikamana na Mobeto ha ha ha! Chibu yeye kakausha tu na ndo inatakiwa hivyo
 
Sisi wanaiume kazi yetu ni kukujoa na kuhudumia watoto au la,ila usitegemee chochote kutoka kwa watoto,we piga mishe zako tu ikitokea watoto wamekusaidia napo sawa ila sio kutegemea

Kiasili,mtoto ni wa mama.
 
Mkuu humu zaidi wapo upande wa Mond kwasababu ya mahaba waliyonayo juu yke hivyo hawaangalii uzito wa hili jambo...! Huwezi kutoa msaada nje wakati kwako kunateketea..kuhusu kuumwa huyo mzee keshaumwa mara nyingi na hatujawahi kuona akipewa uzito si na Mond wala Mwajuma...! Akifa watamuweka kwenye kurasa zao Instagram na kwingineko wakijutia maamuzi yao (,japo kiunafki)...Dunia tunapita yatupasa kutengeneza mema na kuyaishi kuliko visasi.
Wakinsaidia mpaka wakwambie!!?? We nani!!??
 
Hahaha absolutely not! He is my Father bro... Na hali yake ni kawaida sana ivyo namuhudumia kwa kila kitu bro natimiza wajibu wakutunza wazazi wangu!!!
Inawezekana wewe ndiye ulikuwa maskini na baba yako tajiri ukaamua urudi kivulini baada ya kuungua jua sana.
 
Huyo baba au sperm donor???? Hata ningekuwa mimi kama haujanifaa wakati nikiwa na shida sasa hivi unanitakia nini???? Sometimes watoto wanahitaji mtu wa kumuita baba na sio pesa zako au mali zako, just love.
 
Hii iwefundisho kwa wengine, mtu anafyatua watoto kama mbuzi then anawatelekeza. Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Niliona baba mzazi wa barnaba anahojiwa kuhusu barnaba
Mzee alimdis Sana mwanae akasema jamaa hasaidii kabisa familia yeye ni kuhonga tu mademu kwa kuwalipia Kodi za nyumba pamoja na kuwanunulia magari
Hawa wasanii wanapenda Sana sifa za kijinga kumbe wazushi tu
Yaani kama ukisikiliza ile interview ya baba yake barnaba inashangaza Sana yaani Hadi mzee akasema barnaba akifa atazikwa na wahuni wenzake wa huko kinondoni alipopanga inasikitisha sana
 
Kadiri ninavyoongeza miaka ndivyo nami nagundua siri nyingi mno za kiroho ambazo mungu ametupa sisi binadamu wake. Mungu ametuumba kwa upendo wa hali ya juu sana, hakuna mtu anapenda mtoto wake wa kumzaa ateseke makusudi au bila sababu nasisitiza hakuna. Ukiona mzazi wako ana utajiri na ww hakupi huduma yoyote ile jaribu kuulizia majirani ambao walikuona tangia utoto wako hao ndio watakupa picha halisi hasa wazee (wanawake kwa wanaume) hao watakupa ABC ya kilichopelekea mzazi wako asitishe huduma juu yako. MFANO halisi ni Mimi mwenyewe hapa. NIMESOMA KWA SHIDA SANA, HAIWEZI SIMULIKA NA BABA YANGU ALIKUWA MWENYE UWEZO MKUBWA TU (WIZARANI) yes hata kula yangu ni shida sana maana mama yangu alikuwa mjasiriamali ambaye uwezo wake kwa siku ni 3000 hadi 5000 kwa siku na tuko kama watoto wa3 hivi. Niliishi hayo maisha mpaka nafikia level ya UNIVERSITY ndio nikaanza kuona kwa mbali msaada wa BABA YANGU, wakati huu tayari amestaafu yupo tu kihome. Nilipomaliza chuo mungu nae akanisogezea bahati yake ya kupata kazi sehemu nzuri tu. Hapo sasa nikaanza kukaa na mama kiutu uzima anipe kisa na mkasa kwann tuishi maisha yale na baba alikuwa na uwezo mkubwa wa kutuhudumia. Alinielekeza vyema tu, sikuishia hapo nikaenda kwa majirani wa mzee nao wakatoa ya kwao, sikuishia hapo nikaenda kwa pande zote mbili za baba na mama kuulizia tatizo ni nini hasa ili nijue labda mahusiano yao ndio chanzo cha sisi kunyanyasika vile. HATIMAYE NILIPATA MAJIBU SAHIHI KABISA. Ndipo niliporudi kwa mama yangu tena ambaye kwa kweli ameteseka sana kunilea pekeyake. Mama aliniambia tu MTU MBORA DUNIANI NI YULE ANAYESAMEHE KWA LOLOTE BAYA NA KULIPA WEMA WAKE. Nikajipa muda wa kusoma kitabu changu cha dini (QURAN) na umuhimu wa Wazazi iwe ulizaliwa ndani au nje ya ndoa. Lkn pia nikajifunza ni kwa namna gani unaweza rejesha fadhila kwa wazazi kwa ulinganifu usio sahihi kimaono ila kiroho uko sawa kabisa. Hapo nikamjengea mama NYUMBA nzuri kabisa angalua na yy atoke kulala kwenye nyumba ya MATOPE (UDONGO) kisha nikaenda kwa BABA nikaenda mrekebishia nyumba yake ila nae ahisi yuko dunia ya leo. Mwisho kabisa upatapo changamoto kubwa ni muhimu sana kumshirikisha mungu.
Diamond amechukua story ya upande mmoja na hakutaka kutafuta suluhu akidhani kuwa maisha ameyapatia bila kuwa na radhi ya mzazi mmoja pia.
 
Masharti akimsaidia wanarudi tandale kupigwa tena na jua
 
Kwa sababu iwayo yyte Ile, kutomsaidia Baba yake ni strictly ridiculous , na ni absolute foolish ,.... Baba ni Baba Tu hata kama ilikuwaje ..... Ngoja ashuke kaburini ndo atakuja kumbuka why sikumsaidia Baba angu akiwa hai .....
 
Back
Top Bottom