Kadiri ninavyoongeza miaka ndivyo nami nagundua siri nyingi mno za kiroho ambazo mungu ametupa sisi binadamu wake. Mungu ametuumba kwa upendo wa hali ya juu sana, hakuna mtu anapenda mtoto wake wa kumzaa ateseke makusudi au bila sababu nasisitiza hakuna. Ukiona mzazi wako ana utajiri na ww hakupi huduma yoyote ile jaribu kuulizia majirani ambao walikuona tangia utoto wako hao ndio watakupa picha halisi hasa wazee (wanawake kwa wanaume) hao watakupa ABC ya kilichopelekea mzazi wako asitishe huduma juu yako. MFANO halisi ni Mimi mwenyewe hapa. NIMESOMA KWA SHIDA SANA, HAIWEZI SIMULIKA NA BABA YANGU ALIKUWA MWENYE UWEZO MKUBWA TU (WIZARANI) yes hata kula yangu ni shida sana maana mama yangu alikuwa mjasiriamali ambaye uwezo wake kwa siku ni 3000 hadi 5000 kwa siku na tuko kama watoto wa3 hivi. Niliishi hayo maisha mpaka nafikia level ya UNIVERSITY ndio nikaanza kuona kwa mbali msaada wa BABA YANGU, wakati huu tayari amestaafu yupo tu kihome. Nilipomaliza chuo mungu nae akanisogezea bahati yake ya kupata kazi sehemu nzuri tu. Hapo sasa nikaanza kukaa na mama kiutu uzima anipe kisa na mkasa kwann tuishi maisha yale na baba alikuwa na uwezo mkubwa wa kutuhudumia. Alinielekeza vyema tu, sikuishia hapo nikaenda kwa majirani wa mzee nao wakatoa ya kwao, sikuishia hapo nikaenda kwa pande zote mbili za baba na mama kuulizia tatizo ni nini hasa ili nijue labda mahusiano yao ndio chanzo cha sisi kunyanyasika vile. HATIMAYE NILIPATA MAJIBU SAHIHI KABISA. Ndipo niliporudi kwa mama yangu tena ambaye kwa kweli ameteseka sana kunilea pekeyake. Mama aliniambia tu MTU MBORA DUNIANI NI YULE ANAYESAMEHE KWA LOLOTE BAYA NA KULIPA WEMA WAKE. Nikajipa muda wa kusoma kitabu changu cha dini (QURAN) na umuhimu wa Wazazi iwe ulizaliwa ndani au nje ya ndoa. Lkn pia nikajifunza ni kwa namna gani unaweza rejesha fadhila kwa wazazi kwa ulinganifu usio sahihi kimaono ila kiroho uko sawa kabisa. Hapo nikamjengea mama NYUMBA nzuri kabisa angalua na yy atoke kulala kwenye nyumba ya MATOPE (UDONGO) kisha nikaenda kwa BABA nikaenda mrekebishia nyumba yake ila nae ahisi yuko dunia ya leo. Mwisho kabisa upatapo changamoto kubwa ni muhimu sana kumshirikisha mungu.
Diamond amechukua story ya upande mmoja na hakutaka kutafuta suluhu akidhani kuwa maisha ameyapatia bila kuwa na radhi ya mzazi mmoja pia.