Kama DPP haondolewi ofisini mpaka afanye makosa au awe na tatizo la kiafya, Rais kamuondoa katika mazingira gani?

Kama DPP haondolewi ofisini mpaka afanye makosa au awe na tatizo la kiafya, Rais kamuondoa katika mazingira gani?

Nimesoma mtandaoni kuhusu taratibu za kisheria zinazotakiwa kufuata ili kumuondoa DPP ofisini, ambapo sheria imetamka wazi kuwa DPP hapaswi kuondolewa ofisini isipokuwa tu kama ana tatizo la kiafya(illness) au amekwenda kinyume na maadili ya kazi.

View attachment 1782394


Hata katika hili la kwenda kinyume na maadili ya kazi/ professional yake, Rais atapaswa kuunda tribunal kumchunguza kabla ya kumuondoa.

Sasa kama haya yana ukweli, Rais Samia amemuondoa DPP ofisini kwa kigezo gani?

Kama ana makosa, kwanini asichunguzwe kama sheria inavyotaka na badala yake anapewa ujaji?

Wanasheria tusaidieni kuhusu jambo hili.

Najaribu kuweka hicho kipande chenye hizo sheria kinachozunguka mitandaoni ila bado sijafanikiwa.
Ukisoma kifungu hicho cha 19(1) na (2) utagundua kwamba kuteuliwa kwake kuwa judge wa mahakama kunatokana na kukidhi sifa za kuwa DPP vile.Kwa tafsiri nyepesi,hana tatizo lolote ndo maana kateuliwa kuwa judge.
 
Ni muendeleze wa kutoiheshimu katiba yetu, Mwendazake naye alifanya hivi hivi kumwondoa Prof. Asad.
 
Back
Top Bottom