Kama dunia inazunguka, kwanini miamba na milima haiporomoki? Na kwa nini bahari isimwage maji yake?

Kama dunia inazunguka, kwanini miamba na milima haiporomoki? Na kwa nini bahari isimwage maji yake?

Annuity

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2013
Posts
338
Reaction score
198
Kuna vitu vinanitatiza sana sijui ni sababu ya kutaka kujua kila kitu Mimi sio mtaalam wa Geography japo wakati nipo sekondari tu kwa nadharia na kuna concept inasema dunia huwa inazunguka au inajizungusha kwenye mhimili wake. Ila maswali ninayojiuliza inazunguka vipi? Na kwanini isifike kipindi leo tujione tupo upande huu kesho upande mwingine? au mwaka huu tupo upande huu mwaka kesho tupo upande mwingine.
images.jpg

Na pia pia kama inazunguka nilitegemea kwa hali ya kawaida kama unavyozungusha kitu chochote chenye maji kisicho na mfuniko maji yale yatamwagika lakini maji ya bahari mbona hayamwagiki? au ndio hiyo gravity? Na pia effect ya miamba na milima hainokeni labda kupomoka zaidi ya ile wanayosema plate movement kwenye Physical Geography.

Swali la msingi kama inazunguka Je, kwanini kila siku tunajiona tupo sehemu ileile?​
 
Mkuu Annuity
Ni kweli dunia huzunguka jua pia kujizungusha kwenye mhimili wake,swali lako kua kwanini maji hayamwagiki au vitu haviporomoki umeshajijibu mwenyewe..naam gravity ndio sababu ya kila kitu kutegemea dunia kua kama mhimili wake mkuu,yani kila kitu kinavutwa toward the centre of the earth.Jinsi ulivyodhani kua dunia yaweza kua kama "chupa ya chai isiyo na mfuniko" kua ukiigeuza juu chini chai itamwagika ki kua unapogeuza vile ile chai isiyo na kizuizi inavutwa kuelekea katika dunia ndio sababu itatoka na kwenda ardhini wala haiwezi toka ikamwagika angani..nadhani umeona tofauti ya chupa ya chai na dunia kua dunia huvuta kulakitu ikiwemo hiyo chupa ya chai ndio maana unapotoa mfuniko na kugeuza chai huenda inapovutwa...kuhusu kutokujihisi kua upo upande wa pili wa dunia ni hivi;
Wote viumbe na sayari na kila kitu kingine vipo ndani ya universe(ulimwengu) na ulimwengu unafanana kila mahali..ndiomaana ukiwa Singida ukiangalia nyota ni vilevile na utakapoenda Tanga nyota ni zilezile hivyo hata unapogeuzwa upande wa pili kitu ni kilekile au juu na chini ya dunia kitu ni kile kile....

it is he who created the night and the
day, and the sun and the moon. they swim
along, each in an orbit 21:33 quran.
 
Last edited by a moderator:
seanherms umefunguka vizuri kabisa japo naomba ufafanuzi hapo unaposema ulimwengu unafanana kila mahali, ukatoa mfano wa nyota, ni kweli kuwa popote utakapokuwa mpangilio wa nyota utauona vilevile, mi nadhani hii ni kwa sababu nyota nazo ziko.kwenye mwendo sambamba na dunia
 
mkuu Lukansola
sina maana kua nyota ni zile zile kila mahali..bali jinsi zilivyosambaa ni vile vile kila mahali,kwa macho ya kawaida huwezi kuona tofauti kati ya nyota za sehemu moja na za sehemu nyingine ndio maana kwa kutumia macho yetu hatuwezi kuona jinsi dunia inavyo zunguka mkuu...
 
Last edited by a moderator:
Kuna vitu vinanitatiza sana sijui ni sababu ya kutaka kujua kila kitu ​

Labda kwa kutumia mifano rahisi unaweza kujenga picha.

Mimi sio mtaalam wa Geography japo wakati nipo sekondari tu kwa nadharia na kuna concept inasema dunia huwa inazunguka au inajizungusha kwenye mhimili wake. Ila maswali ninayojiuliza inazunguka vipi? Na kwanini isifike kipindi leo tujione tupo upande huu kesho upande mwingine? au mwaka huu tupo upande huu mwaka kesho tupo upande mwingine.

Swali la msingi kama inazunguka Je, kwanini kila siku tunajiona tupo sehemu ileile?​

Yule panya mdogo aliyeko kwenye meli kubwa sana ya mizigo unadhani anaweza akaona kwamba sasa yuko Atlantic na baadae bahari ya hindi? Nadhani panya yule kuona tofauti hizo ni ngumu. Yet; Dunia ni kubwa maradufu sana ya mfano huo na mzuguko wake tunauona kwa macho kila siku. Tunapokuwa upande "huu" hatuoni Jua na tunapokuwa upande "ule" tunaliona Jua. Hivyo kwa siku mara moja tunakuwa upande huu na baadae upande ule.

Na pia pia kama inazunguka nilitegemea kwa hali ya kawaida kama unavyozungusha kitu chochote chenye maji kisicho na mfuniko maji yale yatamwagika lakini maji ya bahari mbona hayamwagiki? au ndio hiyo gravity? Na pia effect ya miamba na milima hainokeni labda kupomoka zaidi ya ile wanayosema plate movement kwenye Physical Geography.​

Maji ya bahari na miamba katika milima na kila kitu hakianguki/mwagiki/poromoki = Gravity (i.e. Kila kitu kilichoduniani kinashikiliwa na Earth's gravity), lakini kwa kuwa dunia inazunguka = "angular momentum & inertia"... basi wapi effect ya mzunguko? Ipo inaitwa Coriolis effect ingawa ni ndogo saaaana na inazidiwa mbali sana na nguvu ya gravity. Kwa lugha nyingine mzunguko wa dunia katika mhimili wake (spinning) sio wa mwendo mkali. Hii ina sababisha mambo kibao madogo madogo angani kama baadhi ya vimbunga (Huricannes), na baharini ndio zaidi kuna baadhi ya mikondo ya maji inayotokana na effect hii, mawimbi fulani ya aina mbali mbali, na mambo mengine mengi sana mfano ulekeo wa hewa inavyosafiri katika Northern hemisphere ni clockwise na Southern hemisphere ni counter clockwise. list inaendelea mbali sana.
 
Ningependa kuanza jibu langu kwa kuhakikisha kuwa wewe unatambua kwamba kupoteza mvutano wa Ardhi (Earth Gravity) haitatokea kamwe. Ardhi ina uzito (mass), pia kila kitu kingine imara chenye uzito (ikiwa ni pamoja na wewe). Ni uzito wa Ardhi yenye kusababisha kuwa na mvutano, na hivyo ili Ardhi iwe bila mvuto basi Ardhi yenyewe isingekuwepo pia.
Baada ya kusema hayo, hebu sasa tufikirie kwamba tunaweza magically kuutoa mbali mvuto wa Ardhi wakati kuacha Ardhi nyuma. Matokeo gani yangetokea Ardhini, inategemea jinsi viombo vilivyomo juu ya Ardhi vile vimeambatana na hii Ardhi. Kama unavyo jua, Ardhi inazunguka kwa kasi kabisa (sote na vyote vilivyomo ndani ya Ardhi tunazunguka katika speedi ya kilo meter elfu moja na mia sita katika ikweta kutokana na mzunguko wa Ardhi peke yake). Sasa kama wewe utazungusha kitu kilicho fungwa na kamba juu ya kichwa chako, kitaendelea kuzunguka katika mduara mpaka utakapo achia kamba. Basi ndipo kitachomoka katika njia iliyo nyooka.
"Kuzima" mvuto wa Ardhi ni sawa na kuruhusu kwenda kwa kamba (mfano wa juu). Viombo na vitu vyote vilivyomo Ardhini vilivyo kuwa havijashikamana na Ardhi pamoja na maji pia hewa vita anza kuacha Ardhi katika njia iliyo nyooka na kuelekea mbinguni katika kila sehemu, ndani ya nyumba watu na vyote vilivyo loose vitaanza kupaa hadi sakafuni na vitabakia pale vimezuiwa na sakafu, vile vilivyo ambatana na Ardhi kama miti vimeshikwa na Ardhi kwa njia ya mizizi, milima na hata majumba yatabakia. Kwa kweli, nguvu inayohitajika kushikilia na kujiweka kuto kuruka mbali na kutoka duniani ni dhaifu sana, ni juu ya 0.3% kama nguvu ya mvuto wa Ardhi (na hata kuwa dhaifu zaidi kila ukiwa mbali na ikweta). Na hata hivyo, vyote vile vilivyo shikamana kabisa na Ardhi vingepata shida kubwa kubakia, kwani hata Ardhi yenyewe ingeanza kupasuka na kuachana vipande vipande na kusambaa angani mwa ulimwengu.
 
Ningependa kuanza jibu langu kwa kuhakikisha kuwa wewe unatambua kwamba kupoteza mvutano wa Ardhi (Earth Gravity) haitatokea kamwe. Dunia ina uzito (mass), pia kila kitu kingine imara chenye uzito (ikiwa ni pamoja na wewe). Ni uzito wa dunia yenye kusababisha kuwa na mvutano, na hivyo ili Ardhi iwe bila mvuto basi Dunia yenyewe isingekuwepo pia.

Great Thinker alhajry
nimefurahiya mchango wako pamoja na swali la mtoa mada Annuity, mengi uliyoyaeleza kwa upande mmoja nayakubali au nayaona yanalogic japo pia yana walakini hapa na pale,
tatizo langu kubwa lipo hapo kwenye Nyekundu, ki ukweli ningependa kutofautiana na wewe kwamba kupoteza mvutano wa Ardhi (Gravity force) HAITATOKEA KAMWE. kwa sababu ifuatayo:

Dunia hipo kwenye position iliyopo kutoka Centre of Gravity kwa sababu ya uzito wake (Mass), badiliko lolote la uzito kwenye Dunia litaathiri position ya Dunia either ielekee karibu na centre of Gravity au iende mbali na Centre ya Gravity

Dunia inawezaje Kupata uzito wa Ziada?
Tuna ushahidi mwingi wa foreign Rock mass (jiwe la Mbozi) ambazo hazikuwa kwenye Dunia lakini zilikuja duniani na sasa ni part ya Dunia, Jiwe la Mbozi ni Dogo sana lakini ikitokea Jiwe/Kimondo-Metiorite Kubwa ikadondokea ndani ya Dunia automatically weight ya Dunia itaongezeka na Dunia itamove kwenda kwenye Stability point Ku compensate extra weight iliyoongezeka, hivyo hii Gravity tuliyonayo haitakuwa hii na Dunia haitakuwa kwenye hii position iliyopo,

Dunia inawezaje Kupoteza uzito wake?
1. Dunia itapoteza uzito ikiwa tu kuna vitu vyenye uzito vilivyo part ya Dunia vikitoka ndani ya Dunia,
Mfano, Kuna research nyingi sana za space na kwenye Sayari zingine zinafanywa na nchi Kubwa America, Russia, China, Japan, India nk. Hizo research zina involve kutuma vyombo ambavyo havirudi tena Duniani.

Mfano Wamerekani walipeleka Chombo Mass mwaka 2012 (Mars Exploration Rover), Jumla ya uzito wake ukichanganya component zote (Rover yenyewe, lander, Backshell, Instruments nk) ilikuwa na total mass ya 1,063 kg (Tani moja), huo uzito Haurudi tena Duniani yaani Dunia imeshapoteza (tani moja) uzito huo moja kwa moja.

Kwa mass ya Dunia huo Uzito wa Rover ni Insignificant, lakini swali la muhimu ni Vyombo vingapi na vyenye uzito kiasi gani vinaenda space kila Mwaka?, kuna saterilte Ngapi na zenye uzito kiasi ngapi zinaenda space kila mwaka?

Kwa Dunia kupoteza uzito itafikia point huo Uzito utakuwa significant na Dunia itakuwa Nyepesi, hivyo itatoka hii position iliyopo sasa kwenda kwenye Stability inayofanana na Uzito wake

Karibuni kwa Changamoto
seanherms, Monstgala
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kituko

Kwanza kabisa naomba tuongelee kuhusu centre of gravity,inafahamika kua centre of gravity ni ile point katika kitu fulani ambayo inapoegemea kwingine kitu hicho kinakua balanced(yaani hakianguki au kusogea kutokana na uzito wake),swali ni kua je..dunia imejiegemeza mahali?

Na kama dunia imekua ikiedemea mahali basi haitokua ni kitu chenye kuonekana kua ndicho kimeshikilia dunia katika centre of gravity ili dunia isiponyoke...

Tunakuja kujua kua hii ni kazi ya centrifugal force inayosababishwa na mzunguko wa dunia katika jua ndio inayosababisha dunia iwe stable kutokucollapse na jua.

Sasa kutakana na kua kinachoshikilia dunia ni hiyo force je unapoongezeka uzito dunia itaponyoka?

Nadhani hapana,labda ikitokea umeongezeka uzito mkubwa sana ambao hauwezi sababisha dunia kupoteza gravity bali utasababisha badiliko la mwendo wa dunia kuzunguka jua..

Au inawezekana force hiyo iliyosababishwa na uzito ulioongezeka ikawa ni kubwa sana kiasi cha kuzidi ile force inayoshikilia vitu vyote duniani(gravity) na kufanya dunia kugawanyika katika vipande kadiri ya force hiyo...

Na hapo tunaona kua utakua ni muendelezo wa explotion za Big bang kwasababu dunia haina maana ya kubaki namna hii milele..

Kuna uwezekano wa miaka mingi sana ijayo ikamezwa na jua au labda ikitokea collition itakayosababisha dunia kuperish

NB:kwa kiasi kikubwa haya ni mawazo yangu wakuu
Monstgala na wengine.
 
Last edited by a moderator:
Vp kuhusu ndege ikipaa huwa inakuwa wap dunian au wap? , km dunia inazunguka kwa nini ndege huwa azikose lengo wakat zinatua? Na je ni kweli tupo up side down?
 
Great Thinker alhajry
nimefurahiya mchango wako pamoja na swali la mtoa mada Annuity, mengi uliyoyaeleza kwa upande mmoja nayakubali au nayaona yanalogic japo pia yana walakini hapa na pale,
tatizo langu kubwa lipo hapo kwenye Nyekundu, ki ukweli ningependa kutofautiana na wewe kwamba kupoteza mvutano wa Ardhi (Gravity force) HAITATOKEA KAMWE. kwa sababu ifuatayo:

Dunia hipo kwenye position iliyopo kutoka Centre of Gravity kwa sababu ya uzito wake (Mass), badiliko lolote la uzito kwenye Dunia litaathiri position ya Dunia either ielekee karibu na centre of Gravity au iende mbali na Centre ya Gravity

Dunia inawezaje Kupata uzito wa Ziada?
Tuna ushahidi mwingi wa foreign Rock mass (jiwe la Mbozi) ambazo hazikuwa kwenye Dunia lakini zilikuja duniani na sasa ni part ya Dunia, Jiwe la Mbozi ni Dogo sana lakini ikitokea Jiwe/Kimondo-Metiorite Kubwa ikadondokea ndani ya Dunia automatically weight ya Dunia itaongezeka na Dunia itamove kwenda kwenye Stability point Ku compensate extra weight iliyoongezeka, hivyo hii Gravity tuliyonayo haitakuwa hii na Dunia haitakuwa kwenye hii position iliyopo,

Dunia inawezaje Kupoteza uzito wake?
1. Dunia itapoteza uzito ikiwa tu kuna vitu vyenye uzito vilivyo part ya Dunia vikitoka ndani ya Dunia,
Mfano, Kuna research nyingi sana za space na kwenye Sayari zingine zinafanywa na nchi Kubwa America, Russia, China, Japan, India nk. Hizo research zina involve kutuma vyombo ambavyo havirudi tena Duniani.

Mfano Wamerekani walipeleka Chombo Mass mwaka 2012 (Mars Exploration Rover), Jumla ya uzito wake ukichanganya component zote (Rover yenyewe, lander, Backshell, Instruments nk) ilikuwa na total mass ya 1,063 kg (Tani moja), huo uzito Haurudi tena Duniani yaani Dunia imeshapoteza (tani moja) uzito huo moja kwa moja.

Kwa mass ya Dunia huo Uzito wa Rover ni Insignificant, lakini swali la muhimu ni Vyombo vingapi na vyenye uzito kiasi gani vinaenda space kila Mwaka?, kuna saterilte Ngapi na zenye uzito kiasi ngapi zinaenda space kila mwaka?

Kwa Dunia kupoteza uzito itafikia point huo Uzito utakuwa significant na Dunia itakuwa Nyepesi, hivyo itatoka hii position iliyopo sasa kwenda kwenye Stability inayofanana na Uzito wake

Karibuni kwa Changamoto
seanherms, Monstgala

Nashukuru kwa mwaliko Kituko

Kwenye Dunia kupoteza au kuongeza uzito, ni kweli yote mawili yanaendelea hata dakika hii. Labda cha msingi ni kipi kati ya matukio haya mawili yanafanyika kwa uwingi zaidi ya kingine na impact yake ni ipi eventually? Katika kupoteza uzito umegusia man made crafts ambazo hazirudi duniani (satellites, space shuttles etc). Impact yake katika Dunia kupungua uzito ni ndogo sana (negligible) lakini ni mojawapo ya matukio yanayopunguza uzito "technically". Lakini hii sio natural occuring hivyo haiwezi kuwa inaendelea tu yenyewe. Mimi ntaongezea katika frame yako hii.

Vipi kuhusu hydrogen inayopotelea angani kila siku? Hii ndio kubwa zaidi katika kupotea uzito kwa Dunia. Hewa hii iko ndani ya atmoshpere na inapenya nje na kupotelea nje yake. Of-course ikishatoka nje haiwezi kurudi. Kwa mwaka hydrogen inayopotea ni tani takribani laki moja kwa mwaka.

Katika kuongezeka uzito kuna vumbi linaloingia duniani kwa kiasi kikubwa sana kutoka nje ya atmosphere. Vumbi hili kisayansi ni part ya vimwondo kwa kuwa ni vitu vilivyo na asili ya nje vinaingia Duniani. Vumbi hili ni takribani tani elfu arobaini kwa mwaka.

Kwa factors hizi mbili kubwa Dunia inapoteza uzito zaidi ya kuongeza. Lakini hewa hii ya hydrogen ina ukomo hivyo ukiweka scenario kwamba imeendelea kupungua mpaka ikaisha. Dunia imekuwa nyepesi na haina hewa. Kwa upande mwingine vumbi linalogia duniani halina ukomo au litaendelea kuingia Duniani kwa kipindi kirefu sana hata baada ya hydrogen kupotelea huko outer space.

Lakini haya yote hayaleti msimamo wa asilimia mia wa situation ya dunia baada ya kipindi kirefu. Kuna unexpexted outside force (Mfano kimwondo kikubwa sana) ambayo inaweza ikabadili mwenendo wa factors hizi na mambo yakawa tofauti sana.
 
Last edited by a moderator:
Vp kuhusu ndege ikipaa huwa inakuwa wap dunian au wap? , km dunia inazunguka kwa nini ndege huwa azikose lengo wakat zinatua? Na je ni kweli tupo up side down?

Labda niongelee swala la kua upside down hayo mengine nikitoka maktaba..

Unaposema upside down lazima ujue wapi ni juu na wapi ni chini,na hii ni nadharia tu kua kuna juu na chini kwa mfano..ukitoboa dunia ukatokea upande wa pili je watu wanaoishi huko juu kwao ni wapi na chini kwao ni wapi?

Kwa hiyo ishu ya kua kuna juu na chini ni nadharia za kidunia ili kurahisisha mawasiliano na mambo mengine lakini universely hakuna juu na chini kwasababu kila kitu kinaelea na hakiegemei kingine

Na ili kue na juu na chini kwa kawaida unapoegemea ni chini..je dunia inaegemea kitu hadi ifike mahali tunasema hapa ni juu na hapa ni chini?

La hasha..hakuna juu na chini katika ulimwengu bali kuna juu na chini katika viumbe wa duniani kwasababu wanaegemea ardhi basi ardhi ni chini na anga ni juu.
 
Nashukuru kwa mwaliko Kituko

Kwenye Dunia kupoteza au kuongeza uzito, ni kweli yote mawili yanaendelea hata dakika hii. Labda cha msingi ni kipi kati ya matukio haya mawili yanafanyika kwa uwingi zaidi ya kingine na impact yake ni ipi eventually? Katika kupoteza uzito umegusia man made crafts ambazo hazirudi duniani (satellites, space shuttles etc). Impact yake katika Dunia kupungua uzito ni ndogo sana (negligible) lakini ni mojawapo ya matukio yanayopunguza uzito "technically". Lakini hii sio natural occuring hivyo haiwezi kuwa inaendelea tu yenyewe. Mimi ntaongezea katika frame yako hii.

Vipi kuhusu hydrogen inayopotelea angani kila siku? Hii ndio kubwa zaidi katika kupotea uzito kwa Dunia. Hewa hii iko ndani ya atmoshpere na inapenya nje na kupotelea nje yake. Of-course ikishatoka nje haiwezi kurudi. Kwa mwaka hydrogen inayopotea ni tani takribani laki moja kwa mwaka.

Katika kuongezeka uzito kuna vumbi linaloingia duniani kwa kiasi kikubwa sana kutoka nje ya atmosphere. Vumbi hili kisayansi ni part ya vimwondo kwa kuwa ni vitu vilivyo na asili ya nje vinaingia Duniani. Vumbi hili ni takribani tani elfu arobaini kwa mwaka.

Kwa factors hizi mbili kubwa Dunia inapoteza uzito zaidi ya kuongeza. Lakini hewa hii ya hydrogen ina ukomo hivyo ukiweka scenario kwamba imeendelea kupungua mpaka ikaisha. Dunia imekuwa nyepesi na haina hewa. Kwa upande mwingine vumbi linalogia duniani halina ukomo au litaendelea kuingia Duniani kwa kipindi kirefu sana hata baada ya hydrogen kupotelea huko outer space.

Lakini haya yote hayaleti msimamo wa asilimia mia wa situation ya dunia baada ya kipindi kirefu. Kuna unexpexted outside force (Mfano kimwondo kikubwa sana) ambayo inaweza ikabadili mwenendo wa factors hizi na mambo yakawa tofauti sana.

Jamani naomba tu kuuliza...
Hivi ukiacha hayo yote mliyosema kuwa yanaongeza au kupunguza uzito wa dunia. Vip kuhusu mimea na viumbe vingine? Mimi ninachojua ni kuwa mmea unatumia mwanga, hewa, maji na nutrients kutengeneza biomass. Mwanga na hewa is almost weight less, maji yanatoka through stomata, lakini mmea unakuja kuwa gogo kubwa sana (for case of trees) Huo uzito uliongeza ulikuwa part ya dunia? Hizo nutrients zilikuwa na volume au weight nyingi kiasi hicho sawa na ya mti? Najua maji yatarudi kwenye atmosphere kwa evapotranspiration, now hiyo biomass (stem or gogo Zima) ni nutrients? kama sivyo then mamilioni ya hectare za misitu duniani haziongezi uzito wa dunia? Siamini kama weight of biomass is inaweza kuwa sawa na intake (water, nutrients, air etc), lazima ardhi ingekuwa na mapango makubwa sana.....

Nawakilisha
 
Mkuu Njaa

Kwanza hongera kwa kuishighulisha akili yako na kuwaza kitu ambacho tulikisahau

Kuhusu hicho ulichosema tunajua kua kila kitu ulimwenguni kimeundwa na atoms,hivyo hata nutrients pia zimeundwa na atoms.Atoms kawaida haziwezi kua created from nothing lakini zinakua created from pre existing atoms through nuclear emmision..kwa hiyo tunaona kua hata hayo "magogo" nayo pia yameundwa kwa atoms

Kwa kiasi kikubwa sana dunia yetu imetawaliwa na organic compounds(compounds of carbon) na pia mimea nayo ni organic compounds...hivyo ni atoms zilizokuepo na zitaendelea kuwepo japokua zinaweza kubadilika tu na kua atoms zingine through hiyo njia niliyotaja hapo juu(nuclear chemistry inahusika)

Hata kwa wanyama pia unamuona tembo kawa mkubwa kweli lakini zote hizo ni atoms zilizomo ndani ya cells ambazo atoms hizo zinaunda compounds mbalimbali

Kinachotokea tu ni kua baada ya kua na genetic material kwa mmea au mnyama basi consuption ya hivyo vitu kutoka katika mazingira huongezeka kutokana na uwepo wa maisha

Na kuhusu hayo "mapango" unayosema ni hivi ngudu yangu Njaa

Kuna theory inaitwa isostacy ikiwa na maana equal balance theory
Hii inasema kua dunia ipo katika equal balance ndio maana hutoona pango linatokea kutokana na kupoteza uzito kwa njia za asili mainly

HOW DOES IT WORK?
Isostacy theory inaeleza kua chini ya crust kuna layer inayoitwa asthenosphere inayokua kama plastic flani hivi..yaani crust inaelea on molten plastic-like layer...

Hivyo kama unavyojua plastic ukiiminya upande mmoja inajaa mwingine vivyo hivyo kwa hii layer...

Pale uzito unapoongezeka sehemu moja basi layer hii husogea na kuinua sehemu uzito ule ulipotoka na utaona kua pako vile vile

Mfano:kuna mmomonyoko wa udongo milimani je?uliona mlima umepungua urefu?
 
Last edited by a moderator:
Jamani naomba tu kuuliza...
Hivi ukiacha hayo yote mliyosema kuwa yanaongeza au kupunguza uzito wa dunia. Vip kuhusu mimea na viumbe vingine? Mimi ninachojua ni kuwa mmea unatumia mwanga, hewa, maji na nutrients kutengeneza biomass. Mwanga na hewa is almost weight less, maji yanatoka through stomata, lakini mmea unakuja kuwa gogo kubwa sana (for case of trees) Huo uzito uliongeza ulikuwa part ya dunia? Hizo nutrients zilikuwa na volume au weight nyingi kiasi hicho sawa na ya mti? Najua maji yatarudi kwenye atmosphere kwa evapotranspiration, now hiyo biomass (stem or gogo Zima) ni nutrients? kama sivyo then mamilioni ya hectare za misitu duniani haziongezi uzito wa dunia? Siamini kama weight of biomass is inaweza kuwa sawa na intake (water, nutrients, air etc), lazima ardhi ingekuwa na mapango makubwa sana.....

Nawakilisha

Mass ya mmea inatokana zaidi sana na Carbondioxide(CO[SUB]2[/SUB]) na kidogo maji (H[SUB]2[/SUB]0). Hizi zote ziko ndani ya dunia kabla hujatoka nje ya atmosphere. Ndio kuna Nishati ya Jua inayowezesha ukuaji wa mti kupitia photosynthesis na hapo ndipo CO[SUB]2[/SUB] inaonekana kutukika zaidi sana kuliko molecules nyingine zote. Gogo lile ni carbon iko zaidi pale. Angalia chemical composition ya Mkaa utaona ni carbon kwa wingi sana.
 
Naomba kuuliza mkuu,

Vipi kuhusu kuzaliana kwa viumbe kama binadamu na wanyama wengine, tukiangalia tu kwa upande wa binadamu tunaona population growth kila kukicha, je hii haiwezi kuongeza uzito wa dunia?
 
Back
Top Bottom