Monstgala
JF-Expert Member
- Aug 25, 2009
- 1,079
- 1,036
Naomba kuuliza mkuu,
Vipi kuhusu kuzaliana kwa viumbe kama binadamu na wanyama wengine, tukiangalia tu kwa upande wa binadamu tunaona population growth kila kukicha, je hii haiwezi kuongeza uzito wa dunia?
Mkuu Dreadnought, Kwa logic ile ya chembe ndogo kabisa zinazounda matter na kwa case hii tunazungumzia mwili au mwili wa kiumbe ukiangaliwa umeundwa kwa kitu gani basi tunakuta element zilizoko hapa hapa duniani. Wataalam wanakuta asilimia 99 ya mwili wa binadamu umeumbwa kwa Oxgen, Hydrogen na Carbon. Wala hatuna tofauti na mimea inagawa yenyewe mpangilio wa molecules unakuwa tofauti kidogo. Hivyo population ya watu na viumbe inatoka kwenye materials au elements za material ziliopo hapa hapa duniani. Kunakuwa na ongezeko la nishati kutoka kwenye mwanga wa jua(mostly). Kwa hiyo miili ya viumbe ni kama recyclable tu, maji yale yale yanazunguka hewa ile ile na madini kutoka kwenye udongo na tukifa yanarudi kule kule.
Last edited by a moderator: