Wakuu
Anheuser na
alhajry na wengine wote
kwanza ningependa "tujadili" kidogo kuhusu tungamo na uzito(mass and weight)
Kwa watu tunaoishi duniani tu hizo ni nadharia tu lakini kwa wenzetu wanaoenda kwenye anga za mbali,mwezini na kwingineko hivi vitu kwao wanavishuhudia
Mass(tungamo) ni kiasi cha maada kilichopo ndani ya maada fulani,yaani mfano atom flani ina particles kiasi gan hiyo ni mass.Mass haibadiliki popote unapoenda ulimwenguni iwe kwenye anga au mwezini kwasababu hata ukienda huko "damu yako,ubongo na kila kitu atoms vitabaki ndani ya mwili wako tu haviwezi kutoka...
Tukija upande wa pili weight(uzito) ni kile kiasi ambacho unakua unavutwa na gravity..yaani ni kwa kiasi gani gravity inaact kwako...ndio maana hua uzito unabadilika unapotoka duniani na kwenda mwezini hipungua na unapoenda kwenye space weight inaweza kua sifuri kabisa yani huna uzito
Na hiyo ndiyo tofauti ya mass na weight
NB:inawezekana hayo maneno ya kiswahili(tungamo na uzito) nikawa nimekosea ikawa ni kinyume si mnaelewa elimu yetu wakuu ni ya "kingelesa" lakin nadhani nipo sawa.