Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Seanherms,
Nielewe ndio wakati unaandika vitu potofu????
Ukisema density ya kitu haibadiliki watu wakakukosoa sema kwanza ulikosea katika maelezo yako halafu jirekebishe.
Usiseme "elewa ninachoongelea." Nielewe nini wakati umepotoka?
Anyhow, mass sio uzito, na mass ya kitu huweza kubadilika. Na density pia hubadilika.
Karibu mkuu tuelimishane
Kuna vitu vinanitatiza sana sijui ni sababu ya kutaka kujua kila kitu Mimi sio mtaalam wa Geography japo wakati nipo sekondari tu kwa nadharia na kuna concept inasema dunia huwa inazunguka au inajizungusha kwenye mhimili wake. Ila maswali ninayojiuliza inazunguka vipi? Na kwanini isifike kipindi leo tujione tupo upande huu kesho upande mwingine? au mwaka huu tupo upande huu mwaka kesho tupo upande mwingine.
Na pia pia kama inazunguka nilitegemea kwa hali ya kawaida kama unavyozungusha kitu chochote chenye maji kisicho na mfuniko maji yale yatamwagika lakini maji ya bahari mbona hayamwagiki? au ndio hiyo gravity? Na pia effect ya miamba na milima hainokeni labda kupomoka zaidi ya ile wanayosema plate movement kwenye Physical Geography.
Swali la msingi kama inazunguka Je, kwanini kila siku tunajiona tupo sehemu ileile?
Nashangazwa kuambiwa eti nyota ni zina ukubwa sawa au zaidi yadunia sasa universe inaishia wap kukiangalia nyota zote zile mbinguniseanherms umefunguka vizuri kabisa japo naomba ufafanuzi hapo unaposema ulimwengu unafanana kila mahali, ukatoa mfano wa nyota, ni kweli kuwa popote utakapokuwa mpangilio wa nyota utauona vilevile, mi nadhani hii ni kwa sababu nyota nazo ziko.kwenye mwendo sambamba na dunia
Gravity ya Jua ndio inafanya Dunia pamoja na sayari nyingine zote ziwe hapo zilipo. Ni gravitational force iliyonyuma ya vitu hivi. Hata jua liko hapo pamoja na nyota nyingine zote katika galaxy tuliyomo kwa mvuto (gravity) wa super massive blackhole katikati ya Milkyway.
Asante kwa elimu yako nzuri, hakika nimejua mambo magumu kwa wepesi, rabda km ningepataga mwalimu mzuri km wewe basi nisingekimbia physics. Samahani naomba unieleweshe juu ya galaxy na universe
Shukrani tamadunimusic. Kuna mada kadhaa tofauti niliwahi kupost lakini hii ambayo kwa sasa ni closed topic kuhusu nyota na galaxies inaweza kuwa muafaka kwa ombi lako. Click hapa
What will happen kama dunia ikipoteza force of gravity;je vitu vitangukia wapi
Nashukuru kwa mwaliko Kituko
Kwenye Dunia kupoteza au kuongeza uzito, ni kweli yote mawili yanaendelea hata dakika hii. Labda cha msingi ni kipi kati ya matukio haya mawili yanafanyika kwa uwingi zaidi ya kingine na impact yake ni ipi eventually? Katika kupoteza uzito umegusia man made crafts ambazo hazirudi duniani (satellites, space shuttles etc). Impact yake katika Dunia kupungua uzito ni ndogo sana (negligible) lakini ni mojawapo ya matukio yanayopunguza uzito "technically". Lakini hii sio natural occuring hivyo haiwezi kuwa inaendelea tu yenyewe. Mimi ntaongezea katika frame yako hii.
Vipi kuhusu hydrogen inayopotelea angani kila siku? Hii ndio kubwa zaidi katika kupotea uzito kwa Dunia. Hewa hii iko ndani ya atmoshpere na inapenya nje na kupotelea nje yake. Of-course ikishatoka nje haiwezi kurudi. Kwa mwaka hydrogen inayopotea ni tani takribani laki moja kwa mwaka.
Katika kuongezeka uzito kuna vumbi linaloingia duniani kwa kiasi kikubwa sana kutoka nje ya atmosphere. Vumbi hili kisayansi ni part ya vimwondo kwa kuwa ni vitu vilivyo na asili ya nje vinaingia Duniani. Vumbi hili ni takribani tani elfu arobaini kwa mwaka.
Kwa factors hizi mbili kubwa Dunia inapoteza uzito zaidi ya kuongeza. Lakini hewa hii ya hydrogen ina ukomo hivyo ukiweka scenario kwamba imeendelea kupungua mpaka ikaisha. Dunia imekuwa nyepesi na haina hewa. Kwa upande mwingine vumbi linalogia duniani halina ukomo au litaendelea kuingia Duniani kwa kipindi kirefu sana hata baada ya hydrogen kupotelea huko outer space.
Lakini haya yote hayaleti msimamo wa asilimia mia wa situation ya dunia baada ya kipindi kirefu. Kuna unexpexted outside force (Mfano kimwondo kikubwa sana) ambayo inaweza ikabadili mwenendo wa factors hizi na mambo yakawa tofauti sana.