Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huwezi kusema "Tungamo ni kiasi cha maada kilichopo ndani ya maada..." !!Mass(tungamo) ni kiasi cha maada kilichopo ndani ya maada fulani
Si kweli kwamba tungamo halibadiliki.Mass haibadiliki popote unapoenda ulimwenguni iwe kwenye anga au mwezini
Okay, Kiswahili sio lugha yako, kwa hiyo kwa lugha yako wewe mass ni nini?Mkuu Anheuser,
Kiswahili ni sio lugha yangu
Kwa kua hapa ni suala la fikra zaidi na wengine Jiografia ilitupita pembeni, naomba kujuzwa yafuatayo:-
1- Hiyo gravity inavuta vitu kuelekea katikati ya dunia?
2 - Hiyo grafity force ipo kwenye sayari ya dunia tu au kila sayari ina gravity force yake?
3 - Jua nalo linavuta vitu kuelekea kwake, namaanisha sayari zote zinavutwa kuelekea katikati (jua liliko)?
Natanguiza shukrani
Dunia inazunguka kwenye muhimili wake na ndiyo maana unaona kujaa na kupwa kwa maji ya bahari, usiku na mchana nk. Vilevile dunia inazunguka jua so on the process unapata majira mbalimbali.Kuna vitu vinanitatiza sana sijui ni sababu ya kutaka kujua kila kitu Mimi sio mtaalam wa Geography japo wakati nipo sekondari tu kwa nadharia na kuna concept inasema dunia huwa inazunguka au inajizungusha kwenye mhimili wake. Ila maswali ninayojiuliza inazunguka vipi? Na kwanini isifike kipindi leo tujione tupo upande huu kesho upande mwingine? au mwaka huu tupo upande huu mwaka kesho tupo upande mwingine.
Na pia pia kama inazunguka nilitegemea kwa hali ya kawaida kama unavyozungusha kitu chochote chenye maji kisicho na mfuniko maji yale yatamwagika lakini maji ya bahari mbona hayamwagiki? au ndio hiyo gravity? Na pia effect ya miamba na milima hainokeni labda kupomoka zaidi ya ile wanayosema plate movement kwenye Physical Geography.
Swali la msingi kama inazunguka Je, kwanini kila siku tunajiona tupo sehemu ileile?​
jamaa anataka aamukue akiwa marekani - ha ha haJibu ni rahisi: Kuwa Dunia inazunguka na vitu vyake vikiwa static. (ww, bahari, milima, nk mnazungushwa kwa pa1, mf hii Tz unayo iona leo huenda imekaa eneo la Malawi). Elewa, hizi nchi zote zipo duniani hivyo huwezi kungundua kama imehama.
Kwa kua hapa ni suala la fikra zaidi na wengine Jiografia ilitupita pembeni, naomba kujuzwa yafuatayo:-
1- Hiyo gravity inavuta vitu kuelekea katikati ya dunia?
2 - Hiyo grafity force ipo kwenye sayari ya dunia tu au kila sayari ina gravity force yake?
3 - Jua nalo linavuta vitu kuelekea kwake, namaanisha sayari zote zinavutwa kuelekea katikati (jua liliko)?
Natanguiza shukrani
Huwezi kusema "Tungamo ni kiasi cha maada kilichopo ndani ya maada..." !!
Ni sawa sawa na kusema damu ni kiminika chekundu kinachopatikana ndani ya damu. Haileti maana.
Si kweli kwamba tungamo halibadiliki.
Chembechembe za maada zinabadilika tungamo kwa kadiri nishati yake inavyobadilika. Kumbuka Tungamo = Nishati gawanya kwa mwendokasi wa mwanga kipeo cha pili.
Okay, Kiswahili sio lugha yako, kwa hiyo kwa lugha yako wewe mass ni nini?
Je Unyoya nao haupo kwenye hii kitu mvutano? maana huwa hauna direction
seanherms, ahsante kwa maelezo mujarab,
Kwa mantiki hiyo, kama jua lisingekua la moto na chombo kikaweza kutua kwenye uso wake, ina maana kitahitaji nguvu kubwa sana kitakapotaka kuondoka kwenye nguyu ya uvutano ya jua kuliko ile ambayo kingeitumia kuondoka kwenye nguvu ya uvutano ya dunia?
Samahani kwa maswali mengi ndugu, Jiografia niliishia kidato cha pili tena kipindi kilikua mara moja kama sio mara mbili kwa wiki achilia mbali siku nilizokua nakosa kuhudhuria kipindi.
Je, katika sayari zote, ni ipi yenye nguvu ya uvutano kubwa?
Nashukuru
......
Hivyo basi gravity huchangiwa na mass na density.
Sayari ni Jupiter.
Ninachojua Density ni expression ya mass na volume. hivyo nadhani ni sahihi kusema gravity huchangiwa na mass na volume badala ya mass na density. ama useme gravity inachangiwa na density basi.
ikirudi kwenye hoja iliyoletwa....(kama hili litakuwa halijasemwa na wengine hapo juu..maana sija soma post zote)...inasemakana kuwa jinsi unavyokariabia kitovu cha dunia ndivyo nguvu ya mvunato-/gravity uongezeka....kwa kuwa maji na mawe yako aridhini/aribu na kitovu cha dunia basi hayawezi kumwagika maana yameshikiliwa na kani ya kuvuta kubwa ya dunia.
Okay, Kiswahili sio lugha yako, kwa hiyo kwa lugha yako wewe mass ni nini?
Ulishawahi ufuatilia? kuna mmoja niliufuatilia hadi nikachoka mimi nilikuwa mdadisi sana utotoni... hata kivuli nilikuwa najaribu kukikimbia... hivi nacho vipi? maana kipo down nacho!
seanherms umefunguka vizuri kabisa japo naomba ufafanuzi hapo unaposema ulimwengu unafanana kila mahali, ukatoa mfano wa nyota, ni kweli kuwa popote utakapokuwa mpangilio wa nyota utauona vilevile, mi nadhani hii ni kwa sababu nyota nazo ziko.kwenye mwendo sambamba na dunia
Ningependa kuanza jibu langu kwa kuhakikisha kuwa wewe unatambua kwamba kupoteza mvutano wa Ardhi (Earth Gravity) haitatokea kamwe. Ardhi ina uzito (mass), pia kila kitu kingine imara chenye uzito (ikiwa ni pamoja na wewe). Ni uzito wa Ardhi yenye kusababisha kuwa na mvutano, na hivyo ili Ardhi iwe bila mvuto basi Ardhi yenyewe isingekuwepo pia.
Baada ya kusema hayo, hebu sasa tufikirie kwamba tunaweza magically kuutoa mbali mvuto wa Ardhi wakati kuacha Ardhi nyuma. Matokeo gani yangetokea Ardhini, inategemea jinsi viombo vilivyomo juu ya Ardhi vile vimeambatana na hii Ardhi. Kama unavyo jua, Ardhi inazunguka kwa kasi kabisa (sote na vyote vilivyomo ndani ya Ardhi tunazunguka katika speedi ya kilo meter elfu moja na mia sita katika ikweta kutokana na mzunguko wa Ardhi peke yake). Sasa kama wewe utazungusha kitu kilicho fungwa na kamba juu ya kichwa chako, kitaendelea kuzunguka katika mduara mpaka utakapo achia kamba. Basi ndipo kitachomoka katika njia iliyo nyooka.
"Kuzima" mvuto wa Ardhi ni sawa na kuruhusu kwenda kwa kamba (mfano wa juu). Viombo na vitu vyote vilivyomo Ardhini vilivyo kuwa havijashikamana na Ardhi pamoja na maji pia hewa vita anza kuacha Ardhi katika njia iliyo nyooka na kuelekea mbinguni katika kila sehemu, ndani ya nyumba watu na vyote vilivyo loose vitaanza kupaa hadi sakafuni na vitabakia pale vimezuiwa na sakafu, vile vilivyo ambatana na Ardhi kama miti vimeshikwa na Ardhi kwa njia ya mizizi, milima na hata majumba yatabakia. Kwa kweli, nguvu inayohitajika kushikilia na kujiweka kuto kuruka mbali na kutoka duniani ni dhaifu sana, ni juu ya 0.3% kama nguvu ya mvuto wa Ardhi (na hata kuwa dhaifu zaidi kila ukiwa mbali na ikweta). Na hata hivyo, vyote vile vilivyo shikamana kabisa na Ardhi vingepata shida kubwa kubakia, kwani hata Ardhi yenyewe ingeanza kupasuka na kuachana vipande vipande na kusambaa angani mwa ulimwengu.