Kama dunia inazunguka, kwanini miamba na milima haiporomoki? Na kwa nini bahari isimwage maji yake?

Kama dunia inazunguka, kwanini miamba na milima haiporomoki? Na kwa nini bahari isimwage maji yake?

Jibu ni rahisi: Kuwa Dunia inazunguka na vitu vyake vikiwa static. (ww, bahari, milima, nk mnazungushwa kwa pa1, mf hii Tz unayo iona leo huenda imekaa eneo la Malawi). Elewa, hizi nchi zote zipo duniani hivyo huwezi kungundua kama imehama.
 
Mass(tungamo) ni kiasi cha maada kilichopo ndani ya maada fulani
Huwezi kusema "Tungamo ni kiasi cha maada kilichopo ndani ya maada..." !!

Ni sawa sawa na kusema damu ni kiminika chekundu kinachopatikana ndani ya damu. Haileti maana.


Mass haibadiliki popote unapoenda ulimwenguni iwe kwenye anga au mwezini
Si kweli kwamba tungamo halibadiliki.

Chembechembe za maada zinabadilika tungamo kwa kadiri nishati yake inavyobadilika. Kumbuka Tungamo = Nishati gawanya kwa mwendokasi wa mwanga kipeo cha pili.



Mkuu Anheuser,

Kiswahili ni sio lugha yangu
Okay, Kiswahili sio lugha yako, kwa hiyo kwa lugha yako wewe mass ni nini?
 
Monstgala, seanherms na wengine Salute sana wakuu kwa uchambuzi wenu makini.
 
dunia inazunguka kwenye muhimili wake kila baada ya masaa takriban 24. gravity ya dunia inatutosha kutuweka sisi stable kwenye hii dunia lakini kumbuka dunia inapozunguka inakuwa na speed yake katika kuzunguka huko na speed hiyo inatofautiana katika equator na poles yani at differents points in lattitudes.
mfano kwenye equator speed ni 465.1 m/s, 1,674.4 km/h or 1,040.4 mi/h
na ukitaka kujua umuhimu wa kuzunguka kwa dunia ni kwamba mfano dunia isimame ghala bila kuzunguka kwenye muhimili wake manake vitu vyote vilivyo katika uso wa dunia vitasukumwa mbele yani eastwards kwa speed ie ile ya dunia mfano vitu vya equator vitasukumwa eastwards kwa speed ya dunia at the equator kwa maana hiyo hapo hata hiyo gravity inayotuvuta duniani haitofaa.
halafu pia kuhusu suala la vitu kuanguka sisi kwa akili zetu ndo tumeweka juu na chini kwenye space hakuna juu wala chini kwa hivyo kitaalamu kuanguka ni kurudi katika uso wa dunia sasa mtu akiwa north pole akirusha coin itaarudi chini yani kwenye uso wa dunia na akiwa south pole akirusha coin pia itarudi chini yani kwenye uso wa dunia kwa maana hiyo ile akili ya kufiri labda dunia itakuja kuanguka pia chini si kweli kwani universe haina mwisho ,juu, mwanzo wala chini wala katikati.
 
Kwa kua hapa ni suala la fikra zaidi na wengine Jiografia ilitupita pembeni, naomba kujuzwa yafuatayo:-

1- Hiyo gravity inavuta vitu kuelekea katikati ya dunia?
2 - Hiyo grafity force ipo kwenye sayari ya dunia tu au kila sayari ina gravity force yake?
3 - Jua nalo linavuta vitu kuelekea kwake, namaanisha sayari zote zinavutwa kuelekea katikati (jua liliko)?

Natanguiza shukrani

1. ndio
2.kila sayari ina gravity yake inayovuta vitu vyake na kwa kiwango chake na pia kuna mvutano kati ya vyombo au sayari angani baina ya vyenyewe yani kuna mvutano baina ya vyombo (au sayari ) vyovyote viwili .
3. ndio
 
Kuna vitu vinanitatiza sana sijui ni sababu ya kutaka kujua kila kitu Mimi sio mtaalam wa Geography japo wakati nipo sekondari tu kwa nadharia na kuna concept inasema dunia huwa inazunguka au inajizungusha kwenye mhimili wake. Ila maswali ninayojiuliza inazunguka vipi? Na kwanini isifike kipindi leo tujione tupo upande huu kesho upande mwingine? au mwaka huu tupo upande huu mwaka kesho tupo upande mwingine.

Na pia pia kama inazunguka nilitegemea kwa hali ya kawaida kama unavyozungusha kitu chochote chenye maji kisicho na mfuniko maji yale yatamwagika lakini maji ya bahari mbona hayamwagiki? au ndio hiyo gravity? Na pia effect ya miamba na milima hainokeni labda kupomoka zaidi ya ile wanayosema plate movement kwenye Physical Geography.

Swali la msingi kama inazunguka Je, kwanini kila siku tunajiona tupo sehemu ileile?​
Dunia inazunguka kwenye muhimili wake na ndiyo maana unaona kujaa na kupwa kwa maji ya bahari, usiku na mchana nk. Vilevile dunia inazunguka jua so on the process unapata majira mbalimbali.

Swali: kwa nini muda huu hapa Tanzania ni saa tano na dakika 37 wakati Marekani watu wamelala? umejiuliza hilo?? na kwa nini wewe ukiwa umelala usiku wa manane lakini nchi zingine ni mchana kweupe?

Kuhusu vitu kumwagika - jaribu kujiuliza unaporusha kitu kwa nini kinarudi chini? kwa nini kisiende juu moja kwa moja? Hapa kuna nguvu ya Uvutano iliyoko katikati ya dunia (Gravitational force 9.81) hii tulisoma form two, sasa inaonekana wewe ulikuwa mtoro wakati mwalimu wa phizikia akiingia darasani kwenu pia hukutaka kujifunza zaidi kwa kujisomea.

Kutuojua sayansi kunaweza kukuondelea ufahamu wa mambo mengi sana hapa duniani, jitahidi kujifunza mambo haya kwani yamo kwenye mitandao buree - usije ukamuuliza baba mkwe wako swali kama hilo lazima atakunyanganya mwanawe fasta.



Soma hapa acha uvivu wa kujifunza:

Nguvu mvutano (Gravitational force) ni kani ya uvutano iliyopo kati ya magimba yote ya ulimwengu. Kila gimba lenye masi linavuta magimba yote mengine yenye masi. Hii ni sababu ya kwamba tunatembea duniani badala ya kuelea kwa sababu masi ya dunia inatuvuta kuelekea kitovu chake. Sisi tuna uvutano wa dunia pia lakini hali halisi kani hii ni ndogo mno kulingana na nguvu ya masi kubwa ya dunia. Wakati huohuo dunia yetu inavutwa na jua na hii ni sababu ya kwamba dunia inazunguka jua na haiwezi kukimbia mbali nayo.
Tukitupa jiwe hewani itaanguka tena chini. Hii ni kwa sababu kani ya mkono ilipeleka jiwe kwa njia ya kwenda juu lakini kani ya uvutano wa dunia inairudisha.
Tabia ya kuvutana inaonekana vema ati ya unia na mwezi. Dunia ni ubwa inaivuta mwezi na kuushika kwenye njia yake ya kazunguka. Lakini wakati huohuo mwezi unavuta pia dunia na hii inaonekana baharini katika mabadiliko ya maji kupwa na maji kujaa. Maji ya bahari inavutwa na mwezi kiasi cha kwamba sehemu ya bahari iliyo moja kwa moja chini ya mwezi iko nusu mita juu ya wastani.

u2l1d2.gif
 
Jibu ni rahisi: Kuwa Dunia inazunguka na vitu vyake vikiwa static. (ww, bahari, milima, nk mnazungushwa kwa pa1, mf hii Tz unayo iona leo huenda imekaa eneo la Malawi). Elewa, hizi nchi zote zipo duniani hivyo huwezi kungundua kama imehama.
jamaa anataka aamukue akiwa marekani - ha ha ha
 
Kwa kua hapa ni suala la fikra zaidi na wengine Jiografia ilitupita pembeni, naomba kujuzwa yafuatayo:-

1- Hiyo gravity inavuta vitu kuelekea katikati ya dunia?
2 - Hiyo grafity force ipo kwenye sayari ya dunia tu au kila sayari ina gravity force yake?
3 - Jua nalo linavuta vitu kuelekea kwake, namaanisha sayari zote zinavutwa kuelekea katikati (jua liliko)?

Natanguiza shukrani

Mkuu Samaritan

Sikuhudhuria jamii intelijensia kwa mda kidogo nilikua kule MMU si unajua tenaa...

Ningependa kukupa majibu kama ifuatavyo

1:ndio Gravity huvuta vitu kuelekea katikati ya dunia kwani ndio gtavity inapoanzia huko ndani
2:Gravity ipo kwenye sayari na nyota zote mkuu na ndio maana zinakua na shape na hata kua kama kitu kimoja...yaani haziathiriwi na mzunguko
3:ndio mkuu jua nalo linavuta vitu...tena gravity ya jua at the surface ni mara 28 zaidi ya gravity ya dunia at the surface.

Karibu.
 
Last edited by a moderator:
Huwezi kusema "Tungamo ni kiasi cha maada kilichopo ndani ya maada..." !!

Ni sawa sawa na kusema damu ni kiminika chekundu kinachopatikana ndani ya damu. Haileti maana.


Si kweli kwamba tungamo halibadiliki.

Chembechembe za maada zinabadilika tungamo kwa kadiri nishati yake inavyobadilika. Kumbuka Tungamo = Nishati gawanya kwa mwendokasi wa mwanga kipeo cha pili.



Okay, Kiswahili sio lugha yako, kwa hiyo kwa lugha yako wewe mass ni nini?

Mkuu Anheuser

Nashukuru kwa mchango wako

Lakini labda hujanielewa kwa sababu kuu mbili..1:labda sijui kuelezea au 2:hujaelewa wengine wameelewa.

Ngoja nijaribu kurudia
Mass(tungamo)ni kiasi cha maada kilichopo katika object(kitu fulani)..kwa nini badala ya kusema object nikasema tena maada?kwa sababu kitu chochote chenye uzito na kinachochukua nafasi ni maada..je hiyo object(kitu tunachokiongelea kua na mass fulani) si maada?ndio maana nikasema hivyo mkuu wangu...au labda niandike hivi..MASS is a quantity of matter in an object.

Kama hapo nimeeleweka ntashukuru mkuu

Kuhusu hilo la mass kuchange ni hivi:-

Umetafuta mass kwa kutumia Einstein's equation mkuu na hapo ni kua unatafuta mass ya 'photon' kwenye light(duality concept of light) ambayo utaitumia kutafuta mass ya wave-particle behavior of light only.....

Je,tunapata vipi mass kama hatutumii Einstein's equation?

Kwanza unaweza kupata kwa kutumia ujazo(volume) na density(nashindwa kuielezea vizury kwa kiswahili samahani) yaani:-
Mass=density kuzidisha na volume.
Je volume ya kitu inabadilika?hapana
Je density ya kitu inabadilika?hapana
Sasa iweje mass ibadilike?tunapata kua mass haiwezi kubadilika popote

Lakini kuna njia ya kupata mass kwa kutumia weight:-

Mass=weight/gravity kwa hiyo hapa tunaona pia kuna uwezekano wa kupata mass kupitia gravity na weight..ukigawanya weight(force) na gravity utapata mass
Je weight inabadilika?ndiyo
Je gravity inabadilika?ndiyo
Kwa nini sasa mass isibadilike?kwa sababu inabadilika weight na gravity hivyo husababisha kuleta mass ile ile ya mwanzo.

Mkuu wewe ulitumia speed of light na energy of photon hapo utapata mass ya photon iliyopo kwenye light.

Lakini hata kwa hiyo kanuni pia iko hivi..

Kwa nini umesema mass itabadilika kwa sababu energy itabadilika?kumbuka katika hiyo 'photon' hiyo ni energy yenyewe ambayo unasema itabadilika hivyo kuathiri mass,inamana labda hiyo energy ikibadilika labda ni kua itageuka na kua aina nyingine ya energy(hii ni kutokana na sheria za energy kua haiwezi kupotea bali inabadilika kua aina nyingine) so ikibadilika na kua nyingine hatutakua tena na hiyo 'photon' yaani hapo hutoona huo mwanga tena kwani hauna nishati....

Kwa nini nimesema hiyo photon ndiyo mwanga?

Kwa sababu imepatikana pale atom inapopoteza nishati kwa njia ya particles(photons) hivyo mwanga hutokea.

Karibu tujadili mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Kwa wale mliouliza kuhusu ndege kupaa na mtu kuruka kwenda juu

Ni kwamba dunia huzunguka na anga pamoja..yaani dunia inazunguka with the 'atmosphere'..kwa hiyo basi kama ndege ikiruka juu huwezi kusema inaweza kusimama pale pale ili dunia ikizunguka ijikute imefika ilipokua inaenda...hapana,itazunguna na dunia pamoja!!kwa hiyo ndio maana ndege inakua na spidi yake ili kuovertake dunia ambayo inaiforce kwenda nayo

Kuhusu kuruka ili ujikute kwingine labda kama utaruka na kuacha dunia na anga yake yani uende mbali kabisa na earth's gravity ili mzunguko wa dunia usiathiri eneo lako...

Nilikua MMU wakuu kule kukanisahaulisha intelijensia ya huku kidogo.
 
seanherms, ahsante kwa maelezo mujarab,

Kwa mantiki hiyo, kama jua lisingekua la moto na chombo kikaweza kutua kwenye uso wake, ina maana kitahitaji nguvu kubwa sana kitakapotaka kuondoka kwenye nguyu ya uvutano ya jua kuliko ile ambayo kingeitumia kuondoka kwenye nguvu ya uvutano ya dunia?

Samahani kwa maswali mengi ndugu, Jiografia niliishia kidato cha pili tena kipindi kilikua mara moja kama sio mara mbili kwa wiki achilia mbali siku nilizokua nakosa kuhudhuria kipindi.
Je, katika sayari zote, ni ipi yenye nguvu ya uvutano kubwa?

Nashukuru
 
Last edited by a moderator:
Je Unyoya nao haupo kwenye hii kitu mvutano? maana huwa hauna direction
 
seanherms, ahsante kwa maelezo mujarab,

Kwa mantiki hiyo, kama jua lisingekua la moto na chombo kikaweza kutua kwenye uso wake, ina maana kitahitaji nguvu kubwa sana kitakapotaka kuondoka kwenye nguyu ya uvutano ya jua kuliko ile ambayo kingeitumia kuondoka kwenye nguvu ya uvutano ya dunia?

Samahani kwa maswali mengi ndugu, Jiografia niliishia kidato cha pili tena kipindi kilikua mara moja kama sio mara mbili kwa wiki achilia mbali siku nilizokua nakosa kuhudhuria kipindi.
Je, katika sayari zote, ni ipi yenye nguvu ya uvutano kubwa?

Nashukuru

Kuhusu kutua kwenye jua kama lisingekua la moto ni kweli mkuu..kwasababu utakua mzito sana mara 28 ya uzito wako hapa duniani

Sayari yenye gravity kubwa zaidi kwenye solar system ni Jupiter mkuu.Na hiyo ni kwasababu ni massive sana na ina density kubwa..kuna sayari zina mass kubwa lakini zina density ndogo hivyo gravity hupungua...gravity inachangiwa na mass pamoja na density..sayari inaweza kua ina mass kubwa lakini na volume yake ikawa kubwa sana hivyo hupungua density na gravity pia...na nyingine ni ndogo na mass ya kawaida lakini zina density kubwa na gravity hua kubwa pia

Hivyo basi gravity huchangiwa na mass na density.

Sayari ni Jupiter.
 
Last edited by a moderator:
......

Hivyo basi gravity huchangiwa na mass na density.

Sayari ni Jupiter.

Ninachojua Density ni expression ya mass na volume. hivyo nadhani ni sahihi kusema gravity huchangiwa na mass na volume badala ya mass na density. ama useme gravity inachangiwa na density basi.

ikirudi kwenye hoja iliyoletwa....(kama hili litakuwa halijasemwa na wengine hapo juu..maana sija soma post zote)...inasemakana kuwa jinsi unavyokariabia kitovu cha dunia ndivyo nguvu ya mvunato-/gravity uongezeka....kwa kuwa maji na mawe yako aridhini/aribu na kitovu cha dunia basi hayawezi kumwagika maana yameshikiliwa na kani ya kuvuta kubwa ya dunia.
 
Ninachojua Density ni expression ya mass na volume. hivyo nadhani ni sahihi kusema gravity huchangiwa na mass na volume badala ya mass na density. ama useme gravity inachangiwa na density basi.

ikirudi kwenye hoja iliyoletwa....(kama hili litakuwa halijasemwa na wengine hapo juu..maana sija soma post zote)...inasemakana kuwa jinsi unavyokariabia kitovu cha dunia ndivyo nguvu ya mvunato-/gravity uongezeka....kwa kuwa maji na mawe yako aridhini/aribu na kitovu cha dunia basi hayawezi kumwagika maana yameshikiliwa na kani ya kuvuta kubwa ya dunia.

Asante mkuu

ni sawa.
 
Okay, Kiswahili sio lugha yako, kwa hiyo kwa lugha yako wewe mass ni nini?


Mass kwa jinsi ninavyo fahamu ni uzito wa kitu isio badilika kwa mvutano wa gravity, kwa mfano ikiwa mimi uzito wangu hapa Duniani ni kilo gramu 60, basi kwenye Mwezi uzito wangu utakuwa kilo gramu 10 tu, na nikiwa mfano kwenye sayari ya Jupita uzito wangu utakuwa kilo gramu 140. Wakati mass yangu haitabadilika popote pale kwa muujibu wa taathiri ya gravitational force. Mass yangu kwa uzito huo kwa kutumia formula W(Weight) = M (Mass) x G (Gravitational force) itakuwa kilo gramu 6.12 na itabaki hivyo hivyo haibadiliki popote pale nilipo.
 
Mkuu Mlaleo

Lakini mwisho wake hutua chini si eti eeh?
Ulishawahi ufuatilia? kuna mmoja niliufuatilia hadi nikachoka mimi nilikuwa mdadisi sana utotoni... hata kivuli nilikuwa najaribu kukikimbia... hivi nacho vipi? maana kipo down nacho!

Kuna vitu kama Moto na Moshi huwa unavutwa juu tu au ndahani vitu visivyo na uzito au uzito mwepesi zaidi huvutwa juu?

Hata Gesi za aina nyingi hukimbilia juu
 
seanherms umefunguka vizuri kabisa japo naomba ufafanuzi hapo unaposema ulimwengu unafanana kila mahali, ukatoa mfano wa nyota, ni kweli kuwa popote utakapokuwa mpangilio wa nyota utauona vilevile, mi nadhani hii ni kwa sababu nyota nazo ziko.kwenye mwendo sambamba na dunia

Ungeisoma quotation ya Qur'an aliyoiweka mwishoni wa maandiko yake ungemuelewa zaidi, hiyo ime summarize kila alichoandika na imejibu swali lako kwake.
 
Ningependa kuanza jibu langu kwa kuhakikisha kuwa wewe unatambua kwamba kupoteza mvutano wa Ardhi (Earth Gravity) haitatokea kamwe. Ardhi ina uzito (mass), pia kila kitu kingine imara chenye uzito (ikiwa ni pamoja na wewe). Ni uzito wa Ardhi yenye kusababisha kuwa na mvutano, na hivyo ili Ardhi iwe bila mvuto basi Ardhi yenyewe isingekuwepo pia.
Baada ya kusema hayo, hebu sasa tufikirie kwamba tunaweza magically kuutoa mbali mvuto wa Ardhi wakati kuacha Ardhi nyuma. Matokeo gani yangetokea Ardhini, inategemea jinsi viombo vilivyomo juu ya Ardhi vile vimeambatana na hii Ardhi. Kama unavyo jua, Ardhi inazunguka kwa kasi kabisa (sote na vyote vilivyomo ndani ya Ardhi tunazunguka katika speedi ya kilo meter elfu moja na mia sita katika ikweta kutokana na mzunguko wa Ardhi peke yake). Sasa kama wewe utazungusha kitu kilicho fungwa na kamba juu ya kichwa chako, kitaendelea kuzunguka katika mduara mpaka utakapo achia kamba. Basi ndipo kitachomoka katika njia iliyo nyooka.
"Kuzima" mvuto wa Ardhi ni sawa na kuruhusu kwenda kwa kamba (mfano wa juu). Viombo na vitu vyote vilivyomo Ardhini vilivyo kuwa havijashikamana na Ardhi pamoja na maji pia hewa vita anza kuacha Ardhi katika njia iliyo nyooka na kuelekea mbinguni katika kila sehemu, ndani ya nyumba watu na vyote vilivyo loose vitaanza kupaa hadi sakafuni na vitabakia pale vimezuiwa na sakafu, vile vilivyo ambatana na Ardhi kama miti vimeshikwa na Ardhi kwa njia ya mizizi, milima na hata majumba yatabakia. Kwa kweli, nguvu inayohitajika kushikilia na kujiweka kuto kuruka mbali na kutoka duniani ni dhaifu sana, ni juu ya 0.3% kama nguvu ya mvuto wa Ardhi (na hata kuwa dhaifu zaidi kila ukiwa mbali na ikweta). Na hata hivyo, vyote vile vilivyo shikamana kabisa na Ardhi vingepata shida kubwa kubakia, kwani hata Ardhi yenyewe ingeanza kupasuka na kuachana vipande vipande na kusambaa angani mwa ulimwengu.

Soma hii sura: 77. SURAT AL-MURSALAAT

Tunaahidiwa kuwa yatatokea.
 
Back
Top Bottom