GE2025 Kama Eng Hersi Said ameenda kugombea Kongwa naanza kuona harufu fulani puani kwangu

GE2025 Kama Eng Hersi Said ameenda kugombea Kongwa naanza kuona harufu fulani puani kwangu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Huyu ameshakatwa kigamboni hawezi tena kupitishwa hadi 2030
Umesoma wapi mzee na ni kwa mjibu wa nini? Ila usije nambia eti ni kwa mjibu wa katiba ya CCM maana navyojua kwa sasa wana CCM hawatendi kwa mjibu wa katiba maana ilishastaafishwa toka February badala yake wako na ile ya Chief Hangaya

Type jibu mkuu
 
Wale waliomwambia Ndugai astaafu baada ya kusema nchi itapigwa mnada ndo wako nyuma ya kila kitu r.i.p Ndugai bora usingetangaza kugombea Ubunge kongwa
 
Wacha waendelee kuwaaminisha watu kuwa Ndugai aliuawa kwa ujinga wao. Ndugai kafariki, wajumbe wapigie kura majina ya wale waliojitokeza awali ( hao ndio hasaa walidhamiria kutaka kuwa wabunge wa hilo jimbo na sio kuleta watu wapya.
sheria na taratibu zinafuatwa
 
Kwa nini wasichukuliwe wale wagombea waliofuatia kwa kura ili wapitishwe kugombea hilo Jimbo? Kwa Injinia Hersi ametokea Kongwa? Au kuna watu wanataka kuleta mauza uza kama yale ya Arusha mjini na Makonda?
Bilioni10
 
Kama huyu jamaa kaamua kwenda Kongwa basi naamini kuwa we are done .


==

Mwananchi wameeleza kuwa baadhi ya majina ya wanachama 24 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliochukua fomu kuwania uteuzi wa kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa kufuatia kifo cha aliyekuwa hayati Job Ndugai yameanza kufahamika, likiwamo la Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said. Fomu za kuomba kugombea ubunge zilichukuliwa na kurudishwa juzi baada ya CCM kutangaza mchakato huo kufanyika kwa siku moja. Hersi ni miongoni mwa majina manne mapya yaliyoingia katika orodha ya watiania hao 24, ambao wamejitokeza kuomba ridhaa ya CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Awali, Hersi alikuwa miongoni mwa wagombea waliochukua fomu kuwania kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na watiania wengine 40. Kati ya hao waliorejesha fomu walikuwa 39 na mchujo wa vikao vya CCM ulirudisha majina sita kwa wajumbe wa jimbo kupiga kura za maoni huku jina la Injinia Hersi likiwa limechujwa na vikao vya juu vya CCM. Mbali na Hersi, wengine waliothibitisha kuchukua fomu kwa mara ya pili ni Deus Seif na Elias Mdao, ambao katika matokeo ya awali walishika nafasi ya tatu na sita mtawalia.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa, Joyce Mkaugala, alipoulizwa majina ya waliochukua fomu alitaja jina la Hersi huku akiahidi kutaja mengine baadaye atakapomaliza kikao. Amesema mchakato wa vikao bado unaendelea, lakini kila hatua itafanyika kwa haki kwa mujibu wa kanuni za chama. Mkaugala pia aliwahimiza waandishi wa habari kusubiri taratibu za chama ili kutangazwa hatua itakayofuata, huku akithibitisha kuwa Hersi anaungana na wagombea wengine kuomba nafasi hiyo kwa mara ya pili, tofauti na awamu ya kwanza aliyoomba Jimbo la Kigamboni ambapo jina lake halikurudishwa.

Machakato ya awali yalionesha kuwa baadhi ya wagombea waliokuwa wamepita mchujo walishika nafasi tofauti za kura, ikiwemo Ndugai aliyekuwa akiongoza kwa kura nyingi, Isaya Mngurumi, Deus Seif, Dk Samora Mshang’a, Dk Simon Ngatunga, Elias Mdao, Philip Chiwanga, Paschal Mahinyila, Balozi Emmanuel Mbennah na Ngaya Mazanda. Kurudiwa kwa mchakato huo wa kura za maoni umetokana na kifo cha Ndugai kilichotokea Agosti 6, 2025, na alizikwa Agosti 10, 2025, kijijini kwao wilayani Kongwa, hali iliyosababisha CCM kuanzisha upya mchakato wa kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya chama katika Jimbo hilo.

Katibu Mkaugala pia alifafanua kuwa taratibu za chama zitafuatwa kwa wagombea hao, ikiwamo kulipia Sh500,000 kwa kila fomu kama ilivyokuwa awali, na kura za maoni zinatarajiwa kupigwa siku ya Jumapili ya Agosti 17, 2025. Hali hii inaonesha CCM inaendelea kwa uwazi na kufuata taratibu za kikanuni ili kuhakikisha mchakato wa uteuzi unafanyika kwa haki na uwazi, huku wananchi wakifuatilia kwa karibu wagombea wapya wa Jimbo la Kongwa.

Soma: GE2025 - Hers Said ajitokeza kugombea Jimbo la Kongwa kwa tiketi ya CCM
Huyu jamaa anautafuta sana ubunge.
 
CCM wakimpitisha watupe na sababu kwanin kigamboni walimkata.
 
CCM wakimpitisha watupe na sababu kwanin kigamboni walimkata.
Nakupa mfano wenye kufanana na hili:
Je mwanamke akikukataa kisha ukamhonga kwa kufuru ili umpate, akikukubali kwa ajili ya pesa zako, sasa unaye penzini,ukaja kumuuliza kisa cha kukukataa awali, unategemea anaweza kutoa jibu la kimantiki?
 
Kwa nini wasichukuliwe wale wagombea waliofuatia kwa kura ili wapitishwe kugombea hilo Jimbo? Kwa Injinia Hersi ametokea Kongwa? Au kuna watu wanataka kuleta mauza uza kama yale ya Arusha mjini na Makonda?
We ndio una mauzauza kichwani, umejaa ukabila, hovyo kabisa we bwege. Kwa taarifa yako we banyamulenge Arusha mjini haijulikani Mwarusha lini alikuwa mbunge. Mbn hamjiulizi majimbo ya Dms? Mbn akili yako ina funza hivyo? Dsm wanaogombea ni wenyeji? Au Dsm haina wazawa? We hujawahi kuwa na akili post zako zote ni uchafu. Nchi hii unagombea popote ili mradi unakubalika. We km siyo msukuma ni mchaga ndio wenye tabia za kipuuzi za ubaguzi
 
Back
Top Bottom