GE2025 Kama Eng Hersi Said ameenda kugombea Kongwa naanza kuona harufu fulani puani kwangu

GE2025 Kama Eng Hersi Said ameenda kugombea Kongwa naanza kuona harufu fulani puani kwangu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa nini wasichukuliwe wale wagombea waliofuatia kwa kura ili wapitishwe kugombea hilo Jimbo? Kwa Injinia Hersi ametokea Kongwa? Au kuna watu wanataka kuleta mauza uza kama yale ya Arusha mjini na Makonda?
Naona unamtomasa rais
 
Kama huyu jamaa kaamua kwenda Kongwa basi naamini kuwa we are done .


==

Mwananchi wameeleza kuwa baadhi ya majina ya wanachama 24 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliochukua fomu kuwania uteuzi wa kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa kufuatia kifo cha aliyekuwa hayati Job Ndugai yameanza kufahamika, likiwamo la Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said. Fomu za kuomba kugombea ubunge zilichukuliwa na kurudishwa juzi baada ya CCM kutangaza mchakato huo kufanyika kwa siku moja. Hersi ni miongoni mwa majina manne mapya yaliyoingia katika orodha ya watiania hao 24, ambao wamejitokeza kuomba ridhaa ya CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Awali, Hersi alikuwa miongoni mwa wagombea waliochukua fomu kuwania kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na watiania wengine 40. Kati ya hao waliorejesha fomu walikuwa 39 na mchujo wa vikao vya CCM ulirudisha majina sita kwa wajumbe wa jimbo kupiga kura za maoni huku jina la Injinia Hersi likiwa limechujwa na vikao vya juu vya CCM. Mbali na Hersi, wengine waliothibitisha kuchukua fomu kwa mara ya pili ni Deus Seif na Elias Mdao, ambao katika matokeo ya awali walishika nafasi ya tatu na sita mtawalia.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa, Joyce Mkaugala, alipoulizwa majina ya waliochukua fomu alitaja jina la Hersi huku akiahidi kutaja mengine baadaye atakapomaliza kikao. Amesema mchakato wa vikao bado unaendelea, lakini kila hatua itafanyika kwa haki kwa mujibu wa kanuni za chama. Mkaugala pia aliwahimiza waandishi wa habari kusubiri taratibu za chama ili kutangazwa hatua itakayofuata, huku akithibitisha kuwa Hersi anaungana na wagombea wengine kuomba nafasi hiyo kwa mara ya pili, tofauti na awamu ya kwanza aliyoomba Jimbo la Kigamboni ambapo jina lake halikurudishwa.

Machakato ya awali yalionesha kuwa baadhi ya wagombea waliokuwa wamepita mchujo walishika nafasi tofauti za kura, ikiwemo Ndugai aliyekuwa akiongoza kwa kura nyingi, Isaya Mngurumi, Deus Seif, Dk Samora Mshang’a, Dk Simon Ngatunga, Elias Mdao, Philip Chiwanga, Paschal Mahinyila, Balozi Emmanuel Mbennah na Ngaya Mazanda. Kurudiwa kwa mchakato huo wa kura za maoni umetokana na kifo cha Ndugai kilichotokea Agosti 6, 2025, na alizikwa Agosti 10, 2025, kijijini kwao wilayani Kongwa, hali iliyosababisha CCM kuanzisha upya mchakato wa kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya chama katika Jimbo hilo.

Katibu Mkaugala pia alifafanua kuwa taratibu za chama zitafuatwa kwa wagombea hao, ikiwamo kulipia Sh500,000 kwa kila fomu kama ilivyokuwa awali, na kura za maoni zinatarajiwa kupigwa siku ya Jumapili ya Agosti 17, 2025. Hali hii inaonesha CCM inaendelea kwa uwazi na kufuata taratibu za kikanuni ili kuhakikisha mchakato wa uteuzi unafanyika kwa haki na uwazi, huku wananchi wakifuatilia kwa karibu wagombea wapya wa Jimbo la Kongwa.

Soma: GE2025 - Hers Said ajitokeza kugombea Jimbo la Kongwa kwa tiketi ya CCM
Ndiyo maana kahonga 100M.
 
Hivi siku hizi mtu anachukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo lolote tu, hata kama sio mkazi wa huko Kongwa, unaenda kuchukua tu fomu?
 
Sio tu miaka mitano ijayo, bali next generation. Wamejipanga kuwarithisha watoto wao madaraka. Vyombo vyote muhimu vya nchi wamevikamata na mzalendo yoyote akitokea anaondolewa. Kama kamati kuu ya CCM, TISS, jeshi lipo kimya.
Kama ulichokiandika kipo sahihi, unadhani huko TISS na Jeshini hakuna watu wao?
 
Hivi siku hizi mtu anachukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo lolote tu, hata kama sio mkazi wa huko Kongwa, unaenda kuchukua tu fomu?
Mbona hata miaka ya nyuma olikuwa hivi hivi!
 
Hamfuatilii tu,Hersi alitarajiwa kutia nia Kongwa toka mwanzo na alishaanza kujipitisha huko ila Ndugai alipobadili maamuzi yake ya kupumzika siasa ndipo Hersi kuelekea Kigamboni.
 
Back
Top Bottom