Kama hakuna Wamarekani waliouawa katika mashambulizi ya makombora ya Iran, basi Marekani haitokuwa na haja ya kujibu mashambulizi

Kama hakuna Wamarekani waliouawa katika mashambulizi ya makombora ya Iran, basi Marekani haitokuwa na haja ya kujibu mashambulizi

:44 p.m.
U.S. ambassador to Israel says few U.S. casualties
JERUSALEM — U.S. Ambassador to Israel David Friedman said that early assessments of Iran’s missile strikes against U.S. forces suggested U.S. casualties may be limited.
“Initial assessments are positive and we pray these reports are true,” Friedman said before he addressed a forum on U.S. policy on Israeli settlements in Jerusalem Wednesday


Hahaha @ The washington post


22 a.m.
Iran claims dozens of U.S. deaths in missile strike
DUBAI — Iran’s Revolutionary Guard claimed Wednesday that dozens of U.S. soldiers were killed in a missile attack on Al-Asad base in Iraq. The U.S. military has said it is still assessing casualties.
In a statement to state television the elite Revolutionary Guard said 15 missiles hit 20 critical points killing 80 soldiers, wounding 200 and destroying large quantities of military equipment, including helicopters, according to the Mehr news agency.
Mkuu hapa nimeambulia "Asad" pekee, huko kwingine ni kama nimepita tu
 
Kwahiyo, unataka kusemaje?

Kwamba Osama hakuuawa?

Obama alidanganya kuhusu kifo chake?
Namaanisha kama kifo chake hakikuonyeshwa kwenye vyombo vya habari kwa sababu walizoona zinafaa kwao what if na kwa hawa wa kwenye hizo base mbili imekuwa hivo! Kama iliwezekana na Osama inashindikanaje hapa, si kote mwenye access ya eneo la tukio na Mmarekani?
 
Hukuona footage ya Ile operation!
Nenda youtube!

Sent using Jamii Forums mobile app
okay wacha USA atuwekee footage ya ISIS leader na mtoto wa bin laden kwanza.

Afu swali halikubiwa mpaka sasa na Trump alisema Iran akishamvulua base za USA watapiga target 54 mbona mpaa hakuna hata target kapiga?

Hivi mnawamini sana USA lini walikuwa wa kweli.
 
IMG_20200113_192113.jpg

Uhalibifu wa kambi,Askari wa marekani walifichwa kwenye handaki baada ya kupata taarifa ya kuwepo kwa mashambulizi
 
Mara tu baada ya mashambulizi kutekelezwa katika kambi mbili za kijeshi zinazotumika na majeshi ya Marekani nchini Iraq, Rais wa Marekani, Donald Trump alikuwa alihutubie taifa la Marekani kwa mujibu wa taarifa rasmi lakini mara baada ya kikao maalumu na maafisa wa ngazi za juu wa masuala ya ulinzi na usalama katika ikulu ya Marekani, White House alisitisha mpango wa kutoa hotuba hiyo.

Lakini hakuishia hapo bali Trump ali-tweet akisema kuwa;


"Kila kitu kipo sawa, kambi zetu mbili za kijeshi zilizopo Iraq zimeshambuliwa na Iran, tunafanya tathmini kujua kama kuna madhara yaliyopatikana au uharibifu wowote wa mali, yote kwa yote tuna vifaa bora vya kivita kuliko nchi yoyote ile Duniani, kwa mbali! Nitatoa tamko kesho asubuhi"

Mpaka sasa taarifa kutoka Marekani zinadai kuwa hakuna taarifa za vifo kwa wanajeshi wao huku Iraq pia ikisema vivyo hivyo, lakini Iran imedai kuwa mashambulizi yao yamefanikiwa kuwaua wanajeshi wa Marekani. Muda upo na tuendelee kuzisubiri taarifa zaidi hususani baada ya hiyo tathmini.

Ila kama hakuna Wamarekani waliouawa katika mashambulizi ya makombora ya Iran, basi sidhani kama Marekani atakuwa na haja ya kuyajibu kijeshi mashambulizi hayo kama Pentagon ilivyokuwa ikiweka wazi hapo awali na kama jambo hili ni kweli, basi wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kimataifa wanayaita mashambulizi haya yanayotajwa kama "kisasi" yaliyofanywa na jeshi la Iran kama hatua ya kuokoa nyuso zao (save face) mbele ya wananchi na dunia kwa ujumla.

Tuendelee kusubiri!

Mods sidhani kama kuna haja ya kuunganisha huu uzi, ni vyema ukabaki hivi hivi kama ulivyo.

Pia pitia mabandiko haya hapo chini kwa taarifa zaidi:


Iran lazima apigwe!
 
Back
Top Bottom