Kama hamkubali mtoto wako Acha tu haitabadilisha kitu.

Kama hamkubali mtoto wako Acha tu haitabadilisha kitu.

Mwanangu nilimfunga nepi kuanzia uchanga, alipoweza kukaa tu nikawa namvisha vikaptula, simfungi tena labda usiku,tena ni kwa siku za baridi tu..siku nyingine namtandikia mpira,

Nawashangaa sana wanaowafungafunga watoto, eti mtoto wa mwaka anashinda na midiaper au nepi, tuwaache wapumue.....kama hutaki mikojo ulizalia nini?
Ha ha wa picha istagram
 
Product nyingi zinazoletwa huku kwetu zinakuwa na viwango vya chini ndiooooooo maana madhara ni mengi. Bidhaa za viwango vya juu wengi hatuwezi bei. Nawashauri akina mama tutumie vya asili hasa vyakula tuepushe familia zetu na magonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema kweli ulimbukeni wanaona usipomvika mwanao pampers kuwa maskini kumbe kumtwika mtoto mizigo isiyo na ulazima
 
Kingine mtu analoweka Nguo za mtoto siku nzima bila hata kubadilisha maji yaani akija kufua hizo nguo maji yote yanatoa harufu jamaniiii sijui wamama wako je? Khaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera miss chaga hii mada inafunda hasaa
 
Mwanangu analala uchi, anakojoa mara mbili tu usiku nikishtuka namkojolesha, asubuhi akiamka tu namtenga anapoo hizo sijui Ni diapers anazijua tukiwa safari ya mbali tu hizi za hapahapa namvisha nepi. Wamama acheni uvivu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Day ya kwanza kumvalisha chalii alitoka mapele ndani ya dk 10 nikamwambia mama watoto kuanzia leo ni mwendo wa nepi tu ukishindwa kuvua ntakua nafua mwenyewe hatujui hayo madude yanakotoka wanaweka kikali zip

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miss Chagga umeongea ukweli.
Hizi pampas sijui nyingi zinamadhara tu.
Waeza mkuta mtoto kajaa rashes kibao kunako but mama yupo tu na pampas

Nepi ni nzuri Zaidi na ukiwa home mama muache wazi mtoto mashine zipumue.

Thumb up miss chaga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sorry miss chagga unamtoto au umeolewa.....??? kama bado naomba tutafutane kwamaana nimesoma nyuzi zako nyingi sana JF unaoneka uko vzr kuwa mke ila kama una mtu kwenye mahusiano usinitafute kwani uwa sitaki kivunja au kuharibu mahusiano ya watu.
Acha kutongoza kwa uoga. Kama Unataka wa peke yako muumbe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu

Leo nimekutana na jambo hospital ikanibidi tukumbushane wakuu.. mama alikuwa anambadili diaper mtoto wake me nipo karibu mtoto kanangozi kama ya mamba huku akianimbia kwa madaha yani mwanangu kila diaper inamkataa. Nikamwangalia nikapata hasira nikamwambia si lazima kuvaa hizo disposable diaper... nikaona na huku niwakumbushe tu...

Kwanza tukubaliane tunatesa watoto kisa ubussy wa kutafuta pesa na pia vipesa vyetu tukivipata ndiyo hatari zaidi...

Adhabu ambayo tayari na naona inatosha Kumwacha mtoto na dada wa kazI na kutuona wazazi weekend tu. Huku hatujui wanaishi vipi ila tunamwachia Mungu hili..

Kingine kumvalisha mtoto diaper hasa hizi za kutupa 24/7 mtoto kafungwasha mzigo huko hasa maeneo ya joto ni mateso sana kwa watoto embu imagine tukiwa mp tu kero yake .. lakini sijui tunahisi mtoto anakuwa tofauti? May be.

Haya madaiper yanaletea watoto UTI, michubuko vipele lakini tumekomaa tu na kubadilisha brand... tuache kufanyia watoto majaribio.

Kama mtoto yupo nyumbani mnunulie vikaptula vya pamba vya kutosha abadilishwe kila anapojisaidia na asubuhi kabla ya kwenda kazini fua anika ondoka akiwa analala avalishwe nepi au hiyo diaper sasa..
Kama ni lazima mtoto avae diaper basi usiwe mkali dada anapombadili mtoto mara kwa mara unakuta una mbajetia dada atumie tatu may be kwa siku na akitumia zaid unamind as if kavaa yeye. Mwisho wa siku tunaumiza mtoto kwa kuachwa na uchafu muda mrefu ili boss aridhishwe jamani embu tubadilike.

Wenzetu wanaangalia ubora kuliko wingi .. ila sisi tunaangalia wingi kuliko ubora .. nyingi zinazokuja kwetu hazipo katika ubora huo tunaofikiria...

SI LAZIMA KUMVALISHA MTOTO HIZO DISPOSABLE DIAPER HATA KAMA UNAINGIZA MILIONI ISHIRINI KWA SIKU KAMA HAI MKUBALI MWANAO ACHA MAVALISHE NEPI FUA HUTABADILIKA NA KUWA MASKINI.. .

Siku njema msalimie mwanao..
Sawa
 
Back
Top Bottom