Kama hamtojali naomba Ufafanuzi wa haraka juu ya haya mambo Matatu tu ya Umuhimu

Kama hamtojali naomba Ufafanuzi wa haraka juu ya haya mambo Matatu tu ya Umuhimu

Akaunti yangu ya CRDB Iliwahi kukaa dormant bila kuweka wala kutoa pesa kwa kipindi 2011-2015 nilipopata kazi mpya...na haikuwa na hata sh mia!

Nikawapa account hiyo hiyo kampuni mpya.... Wakawa wanaingiza mshahara, na mshahara ulipitia hapo na nikawa natoa kawaida tu.

Nikahamishwa kikazi kwenda Lubumbashi 2016... Nilikuwa nikitoa hela nikiwa huko huko Lubumbashi kwa kadi yangu ya CRDB bila tatizo wala mkwamo wowote.

Kifupi kwa bongo, nawakubali sana hawa jamaa CRDB mpaka sasa, Sijawahi kufikiria kuwahama.

Mwenye uzoefu na benki tofauti ataongezea... Kwangu ni hayo tu.
 
Je! Kampuni ya simu iliyokuuzia line na kuisajili Tcra kwa particular zako ikiwepo kadi ya Nida na ukaisajili kwenye mambo yako mbalimbali kama sehemu ya address na utambulisho wako, kama ku recover email zako, usipoitumia muda mrefu kwenye upande wa kupiga simu, Wakimuuzia ile namba mtu mwingine unaweza kuobiruza mahakamani kampuni hiyo ya simu?
 
Mh yaani unamaanisha Baba zako watatu kwa mama mmoja ukapatikana kwa lugha ya kitaalamu ni tri-sperms combination kumbe we ni mtoto wa kishua.

Anyway ong
Mh yaani unamaanisha Baba zako watatu kwa mama mmoja ukapatikana kwa lugha ya kitaalamu ni tri-sperms combination kumbe we ni mtoto wa kishua.

Anyway ongera!
Mtoto haramu huyo
 
1. Je, ukiwa na Akaunti ya Benki fulani ila hukuitumia kwa miaka kati ya 5 hadi 10 ukitaka Kuendelea nayo inawezekana (japo najua itakuwa Imeshafungwa) Kuihuisha au Kuiamsha (Activate) au uachane na haya yote na Ufungue tu Akaunti mpya?

Tafadhali Wataalamu / Wabobezi wa Benki GENTAMYCINE naomba Msaada wenu wa Kiufafanuzi wa haraka na Nitawashukuruni.

2. Je, ukiwa na Akaunti kutoka Benki zetu za hapa Tanzania (Local kama NBC na CRDB) unaweza kuzitumia kwa Kuingiziwa Pesa zako (Mshahara) ukiwa unafanya Kazi nje ya Tanzania na ukazitoa ukiwa huko huko?

3. Naomba kujua Nchi (hasa za hapa Afrika Mashariki) ambazo Benki hizi Mbili za NBC na CRDB zina Matawi yake huko na unaweza bado ukaendelea Kuzitumia hata ukiwa huko huko Kimajukumu.

Natanguliza Shukran kwa Ufafanuzi.
1. Mara nyingi akaunti ikikaa muda mrefu bila kutumika hulala na baadaye kufungwa. Akaunti iliyofungwa huweza kuombewa special approval kama kuna ulazima huo haswa kwa mambo ya kisheria na ikafunguliwa.

Pia kuna wale ambao unakuta ana mkopo unao husiana na akaunti hiyo, na labda anataka kuongeza/top up lakini akaunti ya disbursement ndiyo hiyo imefungwa. Kwa kesi hizi, afisa wa benki anaweza omba ifunguliwe.

Kinyume na hapo, mteja anaweza shauriwa kufungua akaunti mpya tu.

2. Inawezekana kabisa hela yako ikawa inaingizwa kupitia akaunti ya Tanzania hata kams ukiwa nje ya nchi na bado ukaweza kuzitumia kupitia ATMs za benki mbalimbali kwenye nchi utakayo kuwa kwa wakati huo.

Angalizo ni kwamba, kila mwezi inamaana muajiri atalazimika kufanya transfers kwenda kwenye akaunti yako iliyoko Tanzania, kisha wewe kufanya matumizi kupitis ATMs. Hii inaweza kuwa ni gharama kwa muajiri na wewe pia unayetumiwa maana inachukuliwa kuwa ni miamala ya kimataifa/international transactions/transfers.

3. CRDB wana Burundi na Congo, NBC sidhani kama wana tawi nje ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom