Kama haujawahi kunywa energy drinks Hongera na Jiepushe nazo. Kama umezoea kuzitumia Tafadhali weka mpango wa kupunguza na kuacha

Peace,

Awali ya yote niweke wazi andiko langu halina kusudi la kuhafifisha au kuathiri biashara ya mtu yeyote ila ni ushuhada wa kweli na dhairi wa watu wanaonizunguka.

Nimekua nikisikia na kuona vijana wengi wakipendelea vinywaji vya kusisimua mwili alimaarufu "energy drinks" ziko za aina mbali mbali na bei tofauti. Vijana kama boda boda, wanafunzi na vibarua wa kazi za mikono wamekua watumiaji sana wa vinywaji hivi.

Nilipata kusikia na kwa sasa nimeshuhudia kua vinywaji hivi vina uraibu mkali sana na pia athari za moja kwa moja kwa watumiaji wa mara kwa mara. Nina mifano mingi ila nitataja michache kwa lengo la kujenga hoja na kujifunza kwa pamoja.

Kuna vijana kwenye maegesho ya boda boda nimekua nawasikia kua ili siku iende sawa lazima wanywe energy wengine wamekua hata na utaratibu wa kununua za ziada na kuifadhi ili anapoamka tu cha kwanza ni kunywa energy ndio hujiisi utayari wa kuanza kazi.

Mwezi uliopita nilikua na project ya ujenzi nikawa napita kutazama mradi unakwendaje kulinganisha na report ya msimamizi wa mradi ajabu pale site palikua na makopo ya mo-energy na azam energy mengi sana wala sikujali ila cha kushangaza kuna siku nilikuta wamepiga kazi kwa makisio ya kua mbele ya estimated target kwa zaidi ya kama 25% nilifurahi sana nikaamua kuwalipia bili zao za chakula kwa siku tatu.

Mshangao ulikua wangu waliponisihi sana sana niwaongezee bajeti kucover pia "energy" nilipohoji kulikoni msisitizo ule wakajibu "yani hata chakula hakina maana kama hakuna energy" looo !! Nikasema sawa nitaongeza bajeti ya kinywaji hicho kwa kila mmoja aise shangwe walilopiga ni kubwa mara dufu ya nilipowapatia ahadi ya kulipia chakula. Vijana wako adicted mbaya.

Kuna classmate wangu kwa sasa ni muajiriwa shirika fulani la uma kama afisa manunuzi anakiri bila kunywa energy drink anajihisi kupoteza umakini na uwezo wa kuconcetrate mpaka apate vinywaji hivi.

Sasa hivi karibuni amekua analalamika kuhisi kutetemeka hasa kipindi cha usiku na kifua kuuma na kuhisi moyo kwenda mbio sana hasa anapopata wasiwasi wa jambo hata dogo tu na kuhisi kizunguzungu mda wa jua kali akanishirikisha basi nikajaribu kubrowse mtandaoni ya kwamba nini hasa kinaweza kupelekea matatizo haya ajabu ajabu kote majibu yanahusishwa na matumizi ya kupindukia ya energy drinks.

Nikamshirikisha jamaa akasema pia yeye alikua anahisi watatizo hayo yanahusiana na vinywaji ya kusisimua mwili kwa kua matatizo yote hayo yanapomkuta na basi akapata fursa na akipiga energy mbili chap chap anakua fresh kabisa aise jamani tujihadhari.

Nikaona nifanye ufuatiliaji wa jambo hili nikawafuata boda boda nikawauliza kama kuna nyakati wanajihisi kutetemeka mikono, au kuhisi moyo kwenda mbio au kuhisi kupoteza umakini au kifua kuuma na kizunguzungu.

Kwa mshangao wakasema yote hayo yanawakuta kwa nyakati tofauti ila wakanishangaza kwa mara nyingine kwa kuniambia yote hayo yanapowakuta hununua energy ya baridiiii na kunywa na shida zote na mashwahibu hayo hupotea kwa sekunde chache tu.

Ikumbukwe vinywaji hivi havina hata muda wa miaka 10 sokoni lakini madhari yake yameanza kushuhudiwa punde tu mtumiaji anapotumia je matumizi ya muda mrefu yatakua na madhara kiasi gani ?!

Mimi sio daktari wala sina ujuzi wowote wa kitabibu lakini naona viashiria dhahiri vya madhara ya vinywaji hivi. Niliwahi kuona clip fupi ya Mo Dewji akisema hajawahi kuonja ladha ya vinywaji vyake, (jambo fikirishi sana)

Karibuni tujadili nini uzoefu wako katika matumizi ya vinywaji hivi ?

View attachment 2906241
Mkuu kwanza kabisa naomba nikueleweshe kuwa, kwa sasa hakuna kinywaji kinaitwa mo energy. Kuna kinywaji kinaitwa mo xtra tu. Na mo xtra siyo energy drink, ni soft drink ya kawaida ila inaladha ya energy. Nikama vile ilivyo Baritika ni kinywaji chenye ladha ya bia ila hakileweshi. Kama huamini chukua chupa ya mo xtra soma maelekezo yake ukikuta kunasehem umeandikiwa usinywe zaidi ya mbili au mama anaenyonyesha haruhusiwi kutumia niite D.O.G
 
Acha ubishi usiokuwa na kichwa wala miguu mzee mo energy wakati zinatoka ziliandikwa kwa maandishi kabisa mekundu kuwa

Haruhusiwi kunywa mja mzito
Mtu mwenye matatizo na caffein
Mtu anayenyonyesha
usimwe zaid ya mbili
Na usinywe wakati wa kulala
Then baadae mo wakatoa hayo maelezo kwenye chupa zao.

Na moja ya madhara ya moja kwa moja ni kukosa kabisa usingizi kama unasafiri na gari usiku kunywa hutalala ngo na kama utakunywa then ulale basi hutopata usingizi na hata ukipata usingizi unaweza kufa kwa shinikizo la damu

Mkuu mo energy haipo sokoni, kilichopo sokoni ni mo xtra mbona jambo liko wazi kaka au kusoma hujui? Azam energy ni energy drink ila mo xtra ni caborneted soft drink. Kabla hujanywa chochote weka utaratibu wa kusoma kwanza maandishi yaliyoandikwa kwenye kinywaji ya namaana si mapambo Yale.
 
Madereva wa masafa marefu huwaambii kitu kuhusu energy drinks unakuta ana vikopo viwili/vitatu!

Mi hivyo vinywaji vilinishinda mwanzoni tu vilipotoka

Nina jamaa yangu kila siku lazima atwange mbili mbaya zaidi kawazoesha na watoto wake hiyo kitu!
 
Acha ubishi usiokuwa na kichwa wala miguu mzee mo energy wakati zinatoka ziliandikwa kwa maandishi kabisa mekundu kuwa

Haruhusiwi kunywa mja mzito
Mtu mwenye matatizo na caffein
Mtu anayenyonyesha
usimwe zaid ya mbili
Na usinywe wakati wa kulala
Then baadae mo wakatoa hayo maelezo kwenye chupa zao.

Na moja ya madhara ya moja kwa moja ni kukosa kabisa usingizi kama unasafiri na gari usiku kunywa hutalala ngo na kama utakunywa then ulale basi hutopata usingizi na hata ukipata usingizi unaweza kufa kwa shinikizo la damu
Ile energy halisi kabisa m mwenyewe nakumbuka hayo maneno yalikuwepo pia
 
Peace,

Awali ya yote niweke wazi andiko langu halina kusudi la kuhafifisha au kuathiri biashara ya mtu yeyote ila ni ushuhada wa kweli na dhairi wa watu wanaonizunguka.

Nimekua nikisikia na kuona vijana wengi wakipendelea vinywaji vya kusisimua mwili alimaarufu "energy drinks" ziko za aina mbali mbali na bei tofauti. Vijana kama boda boda, wanafunzi na vibarua wa kazi za mikono wamekua watumiaji sana wa vinywaji hivi.

Nilipata kusikia na kwa sasa nimeshuhudia kua vinywaji hivi vina uraibu mkali sana na pia athari za moja kwa moja kwa watumiaji wa mara kwa mara. Nina mifano mingi ila nitataja michache kwa lengo la kujenga hoja na kujifunza kwa pamoja.

Kuna vijana kwenye maegesho ya boda boda nimekua nawasikia kua ili siku iende sawa lazima wanywe energy wengine wamekua hata na utaratibu wa kununua za ziada na kuifadhi ili anapoamka tu cha kwanza ni kunywa energy ndio hujiisi utayari wa kuanza kazi.

Mwezi uliopita nilikua na project ya ujenzi nikawa napita kutazama mradi unakwendaje kulinganisha na report ya msimamizi wa mradi ajabu pale site palikua na makopo ya mo-energy na azam energy mengi sana wala sikujali ila cha kushangaza kuna siku nilikuta wamepiga kazi kwa makisio ya kua mbele ya estimated target kwa zaidi ya kama 25% nilifurahi sana nikaamua kuwalipia bili zao za chakula kwa siku tatu.

Mshangao ulikua wangu waliponisihi sana sana niwaongezee bajeti kucover pia "energy" nilipohoji kulikoni msisitizo ule wakajibu "yani hata chakula hakina maana kama hakuna energy" looo !! Nikasema sawa nitaongeza bajeti ya kinywaji hicho kwa kila mmoja aise shangwe walilopiga ni kubwa mara dufu ya nilipowapatia ahadi ya kulipia chakula. Vijana wako adicted mbaya.

Kuna classmate wangu kwa sasa ni muajiriwa shirika fulani la uma kama afisa manunuzi anakiri bila kunywa energy drink anajihisi kupoteza umakini na uwezo wa kuconcetrate mpaka apate vinywaji hivi.

Sasa hivi karibuni amekua analalamika kuhisi kutetemeka hasa kipindi cha usiku na kifua kuuma na kuhisi moyo kwenda mbio sana hasa anapopata wasiwasi wa jambo hata dogo tu na kuhisi kizunguzungu mda wa jua kali akanishirikisha basi nikajaribu kubrowse mtandaoni ya kwamba nini hasa kinaweza kupelekea matatizo haya ajabu ajabu kote majibu yanahusishwa na matumizi ya kupindukia ya energy drinks.

Nikamshirikisha jamaa akasema pia yeye alikua anahisi watatizo hayo yanahusiana na vinywaji ya kusisimua mwili kwa kua matatizo yote hayo yanapomkuta na basi akapata fursa na akipiga energy mbili chap chap anakua fresh kabisa aise jamani tujihadhari.

Nikaona nifanye ufuatiliaji wa jambo hili nikawafuata boda boda nikawauliza kama kuna nyakati wanajihisi kutetemeka mikono, au kuhisi moyo kwenda mbio au kuhisi kupoteza umakini au kifua kuuma na kizunguzungu.

Kwa mshangao wakasema yote hayo yanawakuta kwa nyakati tofauti ila wakanishangaza kwa mara nyingine kwa kuniambia yote hayo yanapowakuta hununua energy ya baridiiii na kunywa na shida zote na mashwahibu hayo hupotea kwa sekunde chache tu.

Ikumbukwe vinywaji hivi havina hata muda wa miaka 10 sokoni lakini madhari yake yameanza kushuhudiwa punde tu mtumiaji anapotumia je matumizi ya muda mrefu yatakua na madhara kiasi gani ?!

Mimi sio daktari wala sina ujuzi wowote wa kitabibu lakini naona viashiria dhahiri vya madhara ya vinywaji hivi. Niliwahi kuona clip fupi ya Mo Dewji akisema hajawahi kuonja ladha ya vinywaji vyake, (jambo fikirishi sana)

Karibuni tujadili nini uzoefu wako katika matumizi ya vinywaji hivi ?

View attachment 2906241
Nakunywa napojisikia at least chupa mbili kwa mwezi! sijapata uraibu wowte mpka sasa
 
Back
Top Bottom