Mkuu hapa naomba utupe ufafanuzi kidogo, ni kwa jinsi gani walimzuia kiroho, na ni wakina nani
Ni kwamba kampuni ya Apple ilianzishwa na Jobs, Wozniak na Wayne.
Wayne akaja akamuuzia hisa zake Jobs, kwa hivyo Jobs akawa na karibia 45% ya umiliki wa Apple Inc, wakaendelea Steve kaenda kumchukua John Sculey nadhani kutoka Pepsi ili aje kusaidia kwenye mauzo, Sculey alipokuja Wakamfanyia figisu Jobs hadi wakamfukuza Apple, na Steve akauza hisa zake karibia zote.
Steve akaenda kuanzisha kampuni inaitwa NEXT, na akawekeza kwenye kampuni ya Animation inaitwa Pixar, sasa, NEXT ya Steve ikawa na Technology bora sana (ndio hiyo ilitumika kutengeza bidhaa kama ipod zilizopendwa sana).
Upande wa Apple wakati Jobs akiwa NEXT kampuni ya Apple ilianza kufilisika, ndio wakamfuata Steve wakainunua NEXT(Technology) wakamuajiri Steve kuwa C.E.O wa kulipwa mshahara wa kawaida...
Steve anakufa ana hisa hazizidi asilimia 1(1%) katika Apple.
Na ukumbuke wakati anaianzisha Apple alipouziwa hisa na Wayne alikuwa na zaidi ya 45% hisa za Apple.
Sasa chukua thamani ya Apple Inc leo alafu uangalie 45% ya thamani ya Apple ni lazima Steve angekuwa Top 3 na hata jina la Bill Gates lisingevuma sana.
Steve Jobs alikuwa na tabia kuwafokea wakati mwingine kujibizana na wafanyakazi wake, jambo hili naamini alikuwa na vita kubwa ya kiroho, hii ikichagizwa na upande wake mmoja kuwa ni muarabu.
Angekuwa mzungu mwenzao bila shaka asingeteseka vile.
Kuhusu nani alikuwa akimloga, naomba nisitaje mtu, ila baada ya kifo cha Steve Jobs, katika Interview moja Bill Gates anajigamba anasema maneno yanayofanana na haya "Steve Jobs alikuwa mchawi, ila mimi nilikuwa mchawi zaidi yake".