Kama Hesabu rahisi (Fedha,idadi,muda) za kila siku zina eleweka , Basi hii Hapa ni Mbinu rahisi ya kuelewa Programming Kupitia Websites na Mobile App

jikuTech

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2023
Posts
227
Reaction score
292
Programming tafsiri rahisi ni kutengeneza programu ,kwamba baada ya kufanya programming ndio inapatikana programu ya kompyuta, undani wa kujua programming ni kufahamu sayansi ya kompyuta.

LAI : Maelezo haya ni ya kiswahili lakini kwa neno ambalo hauja lielewa kabla ya kuendelea chukua muda lifuatilie kwenye intaneti ama AI yoyote ili uelewe maana yake, bila kuelewa neno lolote ni sawa umepoteza muda wako bure.

Programming ni kutengeneza programu za kompyuta. Ili kuelewa programming kwa undani unaotakiwa ili kuleta matokeo yake yanayo staili ni muhimu kufahamu sayansi ya kompyuta.

Baada ya kufahamu sayansi ya kompyuta hapo ndio unaweza kufahamu zaidi kipengele cha programming kina kaa wapi katika kompyuta na jukumu lake ni lipi hasa.

Ili kufahamu sayansi ya kompyuta kwa ajili ya programming ni sawa na kumwambia mtu kuhusu somo la hesabu, kama ilivyo somo la hesabu halipendwi na sio kupendwa tu hata kuweza wanaweza watu wachache.

Lakini wote bila kujali kuweza au kuto kuweza hesabu, wakiwa mtaani wanajua vipimo, hesabu za hela , hesabu za idadi ya vitu , na hata hesabu za muda pamoja na urefu ambapo zote hizi ni hesabu ambazo wengi shuleni wanashindwa na hawaziwezi.

Hivyo utaratibu wa kawaida wa kujifunza programming ni sawa na utaratibu mgumu wa hesabu, mbinu mbadala ambayo inaweza kusaidia kujifunza sayansi ya kompyuta ni kujifunza matumizi rahisi ya programming yanayo onekana na ambayo tunayo kwenye maisha ya kila siku.

Baada ya kuelewa matumizi rahisi yanayo onekana, mtu anaweza kujiongeza mwenyewe katika safari ya programming kama ilivyo kwa mtu kufahamu matumizi na hesabu rahisi huweza kupanga bajeti nyumbani kwake bila msaada wa mwalimu wa hesabu.

Utaratibu wa kawaida wa kuelewa programming unatutaka tufahamu hesabu ngumu kama boolean aljebra,binary number system, Logic Gates, Circuits na hapo ndio utaelewa programming.

Tukifuata utaratibu huu wakati tunajua ni ngumu kama utaratibu wa kawaida wa kujifunza hesabu ni kama kuhamasisha watu wakimbie taaluma hii.

Bahati nzuri matumizi rahisi ya hesabu watu wanafahamu na wanaishi nazo hiz hesabu kwenye vipimo idadi, idadi,kulinganisha , fedha ,muda na mambo mengine mengi sana hadi bajeti za kila siku nyumbani. Tofauti na matumizi rahisi ambayo pamoja ni rahisi lakini bado wanaofahamu ni wachache kwenye jamii ya kiswahili na hao wanao fahamu wengi wao wanaona fahari kwamba wengine hawajui wanacho kujua wakati ni matumizi rahisi ya programming.

Sasa kujifunza matumizi rahisi ya programming mtu anapata uwezo wa kujiongeza katika programming kutoka kuwa wakawaida hadi kuwa mtaalamu kiasi cha kunufaika katika fursa nyingi unazo ziona kama ilivyo katika kufahamu matumizi rahisi ya hesabu kujiongeza kuna leta fundi ujenzi, wafanya biashara wadogo na wakubwa.

Ukijifunza matumizi haya rahisi kwa vitu vinavyo onekana na tunavyo tumia unapata imani kubwa ya urahisi huu unafanya haya je kwa ukubwa inafanya vitu gani.

Maisha ya matumizi rahisi ambayo yanaweza fanya mtu akaelewa programming ni Webs na Mobile Apps, hivyo ni muhimu mtu kujifunza ama Web Stacks technology ( Web Stacks namaanisha teknolojia za websites ) au Mobile App Development ( utengenezaji wa programu za simu) kwa kuwa ndio vitu ambavyo ni matunda ya programming tunayo tumia kila siku na manufaa yake tunayaona ,, mfano jamii forums, facebook, instagram, tiktok, bbc,whatsapp wana web na app wafanyabiashara wanawapa pesa kuweka matangazo ya biashara yao kulingana na tangazo lao litaonekana na watu wangapi kitu ambacho zamani wafanya biashara walitumia redio na magazeti kwenye jamii yetu ya kiswahili,, hivyo kwa mtu kujifunza teknolojia hizi kunamwezesha kufahamu programming ni kitu gani , inaleta nini na nini kwa kufanyaje na manufaa yake ni haya, Baadaye ndio mtu atapanua mawazo na kuitumia na kujiongezea maarifa zaidi nayo mpaka kujiongeza mwenyewe iwaje kulingana na yeye mwenyewe kama ilivyo hesabu rahisi zina wafanikisha watu katika biashara na maisha ya kila siku licha ya walikuwa wanapata maksi za chini darasani wakiwa shule.

Changamoto ya kujifunza programming hata hii rahisi katika jamii ya kiswahili ni pale mtu kidogo lugha ya kiingereza ni changamoto sana kuielwa , wakati vyanzo vingi vyenye elimu hii vimeandika kwa kiingereza,, changamoto hii baadhi ya wataalamu wameiona na wamejitahidi kuelewesha kwa lugha ya jamii ya kiswahili.

Mfano ( Masomo ya Kiswahili )
Jiku Tech Tips inakupa Elimu hii kwa namna ya
Videos Youtube { Jiku Tech Tips },,
MAKALA,, Jamii forums {jikutechtips} ,,
kwenye Tovuti .. Jiku Tech Tips..{Jiku Tech Tips }

Bongoclass {Ict }

Hivyo kupitia vyanzo vingine vingi ama Jiku Tech Tips ama Bongoclass ama sehemu nyingine unaweza kujifunza Teknolojia za web, yaani tovuti(websites) na teknolojia za programu za simu (Mobile App) . Baada ya hapo ndio unaweza kuelewa zaidi habari ya Boolean Aljebra , binary number system, embedded systems, Robotics, Machine Code n.k teknolojia ambazo hadi saizi zinafanya maajabu yote mfano katika sayansi ya anga na Strong Artificial Intelligence.



Ni ngumu kuandika kila kitu katika andiko moja , Karibu ujifunze kwa vitendo masomo maalumu katika vitabu hivi vimefundisha kwa kiswahili.

Vitabu vya Mobile App Development (Android): PDFs kama "ANDROID PROGRAMMING.pdf", "UTANGULIZI WA ANDROID PROGRAMMING.pdf", na "ANDROID NETWORKING.pdf" kwa wanaoanza.
Jifunze mambo mengi hapa kama kuweka Android Studio kwenye kompyuta , UI design (sehemu ya mtumiaji), data storage (k.m. SQLite,MySQL na Room), na networking na web servers. Masomo yamepangwa kwa wiki (k.m. wiki 1-5), ni mazoezi ya vitendo kwa kutumia Java. Hii ni muhimu kwa wanaoanza ambao hawapendi Kiingereza.

Kitabu cha Web Development ("WEB DEVELOPMENT MASTERY.pdf"): Utajifunza mambo mambo kama HTML, CSS, front-end na back-end (k.m. PHP?), responsive design, na security. Ina episodes au sehemu zinazotosha kutengeneza tovuti rahisi.

Web Mastery

WEB DEVELOPMENT MASTERY.pdf - 15,000/=

Mobile App Development

ANDROID PROGRAMMING.pdf, 10,000/=

UTANGULIZI WA ANDROID PROGRAMMING.pdf, - 5,000/=

ANDROID NETWORKING.pdf) = 5,000/=

Fanya Malipo kwenye LIPA NAMBA

Jina LIPA JIKU TECH - 67580023 , mara baada ya malipo tuma Screenshot ya muamala wako kwenye WhatsApp ya namba 0682329852 ili kutumiwa Kitabu kwenye WhatsApp Yako Muda huo huo.

Na ukilipia kitabu chochote Jiku Tech Tips kama umejisajili kwenye jikutechtips.com Basi unaingia kwenye watu maalumu wanao jifunza masomo maalumu ya Tehama.
 

Attachments

  • Screenshot 2025-09-20 125336.png
    226 KB · Views: 51
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…