Kama hewa itatoka katika eneo lililo na uwazi, je ni kitu gani huzuia hewa isitoke nje ya uso wa dunia?

Kwa mujibu wa NASA, dunia haipo closed, viumbe na vitu vyote vipo nje ya uso wa dunia,dunia inaelea katika space ambayo ipo wazi pande zote
HIYO SPACE YOTE IMEJAZWA NA HEWA , LAKINI OXYGEN IPO KWENYE USO WA DUNIA PEKEE KWA SABABU NDIPO HUZALISHWA NA MIMEA, IKIPANDA JUU KUNA PRESSURE YA KUISHUSHA CHINI.
 
Habari za jioni wadau....

Kama mnakumbuka nilileta mada kuhusu chanzo au asili ya Oxygen, Nashukuru wadau walinipa elimu nzuri kuhusu Oxygen na nikaelewa vyema.

Leo pia nina swali kuhusu Oxygen au hewa.

Kwa mujibu wa sayansi, asili ya hewa au mazingira yake ni lazima iwe katika eneo ambalo limefungwa, ndani yake kuwe na pressure na kizuizi ili hewa hiyo isitoke.

Kwa mujibu wa NASA, dunia haipo closed, viumbe na vitu vyote vipo nje ya uso wa dunia,dunia inaelea katika space ambayo ipo wazi pande zote na haina mwisho.

Je, inakuwaje mpaka duniani panakuwa na mgandamizo wa hewa ingali pande zote zipo wazi?

View attachment 3057848

Naomba wadau wa sayansi ya mazingira mnijuze kuhusu hili....
Kwanza unahisi tuko ndani ya Dunia au juu ya Dunia?
 
Kama ambavyo ukirusha jiwe juu linarudi kwa gravity force ndio ambavyo hewa inabaki kwenye uso wa dunia.

Mbona hujiulizi kama dunia ipo wazi kwanini wewe hudondokei kwenye space au sayari ya karibu? 🤔
 
Bro ,umeshajibiwa kuwa ni Gravity...
Gravity ina effects kulingana na uzito wa matter....Heavier the matter,the more it is affected.....
Nimeambiwa ni Gravity, lakini sijaambiwa inafayaje kazi hiyo Gravity
 
Kwa mujibu wa NASA, dunia haipo closed, viumbe na vitu vyote vipo nje ya uso wa dunia,dunia inaelea katika space ambayo ipo wazi pande zote
HIYO SPACE YOTE IMEJAZWA NA HEWA , LAKINI OXYGEN IPO KWENYE USO WA DUNIA PEKEE KWA SABABU NDIPO HUZALISHWA NA MIMEA, IKIPANDA JUU KUNA PRESSURE YA KUISHUSHA CHINI.
Mh ndo mwalim alikufundiaha hivo 😂😂
 
Kama ambavyo ukirusha jiwe juu linarudi kwa gravity force ndio ambavyo hewa inabaki kwenye uso wa dunia.

Mbona hujiulizi kama dunia ipo wazi kwanini wewe hudondokei kwenye space au sayari ya karibu? 🤔
Siwezi kudondoka kwani nipo katika uwanja mkubwa ambao umezungukwa na milima, mabonde, bahari
 
Mizunguko wa dunia unahusika kivipi na kutunza au kuzuia hewa isitoroke?
Mzunguko wa dunia husaidia katika kutunza na kusambaza hewa kwa njia zifuatazo:

1. Athari ya Coriolis: Mzunguko wa dunia husababisha athari ya Coriolis, ambayo inaathiri mtiririko wa hewa na maji kwenye uso wa dunia. Athari hii husaidia kusambaza hewa kwenye maeneo mbalimbali ya dunia, na hivyo kusaidia kusawazisha shinikizo la hewa na kuzuia hewa kutoroka kirahisi.

2. Mizunguko ya Hewa: Mzunguko wa dunia huchangia katika kuunda mifumo ya hali ya hewa kama vile mizunguko ya hewa ya Hadley, Ferrel, na Polar. Mifumo hii inahusisha mzunguko wa hewa kutoka maeneo ya ikweta kuelekea ncha za dunia na kurudi, kusaidia kusambaza hewa kwenye tabaka za angahewa na kuhakikisha kuwa hakuna eneo lenye ukosefu mkubwa wa hewa.

3. Usawazishaji wa Joto: Mzunguko wa dunia husaidia kusambaza joto kwa usawa, kwani uso wa dunia unapata joto kutoka kwa jua mchana na kupoa usiku. Usawazishaji huu wa joto husaidia kudumisha hali ya hewa thabiti, kuzuia upotevu wa gesi kutoka kwenye tabaka za chini za angahewa.
images (1) (30).jpg
 
Habari za jioni wadau....

Kama mnakumbuka nilileta mada kuhusu chanzo au asili ya Oxygen, Nashukuru wadau walinipa elimu nzuri kuhusu Oxygen na nikaelewa vyema.

Leo pia nina swali kuhusu Oxygen au hewa.

Kwa mujibu wa sayansi, asili ya hewa au mazingira yake ni lazima iwe katika eneo ambalo limefungwa, ndani yake kuwe na pressure na kizuizi ili hewa hiyo isitoke.

Kwa mujibu wa NASA, dunia haipo closed, viumbe na vitu vyote vipo nje ya uso wa dunia,dunia inaelea katika space ambayo ipo wazi pande zote na haina mwisho.

Je, inakuwaje mpaka duniani panakuwa na mgandamizo wa hewa ingali pande zote zipo wazi?

View attachment 3057848

Naomba wadau wa sayansi ya mazingira mnijuze kuhusu hili....
Waislam halitupi shida sana kuelewa hilo.

Kuna "barzak" baina ya "axis" zisizotakiwa ziingiliane.

Anza kwa kusoma kuhusu "barzak" utapata pakuanzia "research" ya maana sana.
 
Kwa mujibu wa NASA, dunia haipo closed, viumbe na vitu vyote vipo nje ya uso wa dunia,dunia inaelea katika space ambayo ipo wazi pande zote
HIYO SPACE YOTE IMEJAZWA NA HEWA , LAKINI OXYGEN IPO KWENYE USO WA DUNIA PEKEE KWA SABABU NDIPO HUZALISHWA NA MIMEA, IKIPANDA JUU KUNA PRESSURE YA KUISHUSHA CHINI.
Wakati hewa inashushwa chini, inafika chini kivipi na wakati huo dunia inazunguka kwa kasi?
 
Waislam halitupi shida sana kuelewa hilo.

Kuna "barzak" baina ya "axis" zisizotakiwa ziingiliane.

Anza kwa kusoma kuhusu "barzak" utapata pakuanzia "research" ya maana sana.
Kwa ufupi naomba unijuze, 'barzak' ni nini?
 
Mzunguko wa dunia husaidia katika kutunza na kusambaza hewa kwa njia zifuatazo:

1. Athari ya Coriolis: Mzunguko wa dunia husababisha athari ya Coriolis, ambayo inaathiri mtiririko wa hewa na maji kwenye uso wa dunia. Athari hii husaidia kusambaza hewa kwenye maeneo mbalimbali ya dunia, na hivyo kusaidia kusawazisha shinikizo la hewa na kuzuia hewa kutoroka kirahisi.

2. Mizunguko ya Hewa: Mzunguko wa dunia huchangia katika kuunda mifumo ya hali ya hewa kama vile mizunguko ya hewa ya Hadley, Ferrel, na Polar. Mifumo hii inahusisha mzunguko wa hewa kutoka maeneo ya ikweta kuelekea ncha za dunia na kurudi, kusaidia kusambaza hewa kwenye tabaka za angahewa na kuhakikisha kuwa hakuna eneo lenye ukosefu mkubwa wa hewa.

3. Usawazishaji wa Joto: Mzunguko wa dunia husaidia kusambaza joto kwa usawa, kwani uso wa dunia unapata joto kutoka kwa jua mchana na kupoa usiku. Usawazishaji huu wa joto husaidia kudumisha hali ya hewa thabiti, kuzuia upotevu wa gesi kutoka kwenye tabaka za chini za angahewa.View attachment 3057897
Wote tunafahamu upepo ukiwa mkali unaweza kusogeza au kuyumbisha vitu, lakini kwa mujibu wa sayansi, dunia inazunguka kwa 1,040mph, mzunguko huo ni wa kasi kubwa lakini hatujawahi kuhisi au kuona kitu chochote kikisogea au kuyumba.

Je ni sababu zipi zinafanya tusihisi au kuona dalili za mzunguko wa dunia?
 
Habari za jioni wadau....

Kama mnakumbuka nilileta mada kuhusu chanzo au asili ya Oxygen, Nashukuru wadau walinipa elimu nzuri kuhusu Oxygen na nikaelewa vyema.

Leo pia nina swali kuhusu Oxygen au hewa.

Kwa mujibu wa sayansi, asili ya hewa au mazingira yake ni lazima iwe katika eneo ambalo limefungwa, ndani yake kuwe na pressure na kizuizi ili hewa hiyo isitoke.

Kwa mujibu wa NASA, dunia haipo closed, viumbe na vitu vyote vipo nje ya uso wa dunia,dunia inaelea katika space ambayo ipo wazi pande zote na haina mwisho.

Je, inakuwaje mpaka duniani panakuwa na mgandamizo wa hewa ingali pande zote zipo wazi?

View attachment 3057848

Naomba wadau wa sayansi ya mazingira mnijuze kuhusu hili....
Kuna wale wanajikuta hawaamini MUNGU waelezee na hii sayansi sasa 😂😂
 
Sawa kuna matabaka ya hewa, lakini sayansi inasema ni lazima eneo liwe limefungwa na pasiwe na nafasi ya kutoka
Mgandamizo wa hewa wala hautegemei kwamba hewa hiyo lazima iwe imefungiwa kwenye chombo au eneo fulani lililozibwa pande zote.

Shinikizo au mgandamizo ni kugandamiza (kama neno lenyewe lisomekavyo).

Kitu kimoja kikiwa juu ya kingine, hapo tayari kuna mgandamizo.

Hewa inakuwa na mgandamizo kwa sababu molekyuli moja ya hewa inakandamiza nyingine na nyingine nayo inakandamizwa na nyingine.

Molekyuli za hewa zinakandamizana kwa sababu zina uzito. Molekyuli zina uzito kwa sababu zinavutwa na kani ya dunia.

Mchawi hapa ni uvutano wa dunia. Isipokuwepo kani ya uvutano wa dunia, vitu vinakosa uzito.

Dunia haiwezi tena kushikamana kama ilivyo.

Na wala hakuna kitu chochote kinachoweza kusalia kwenye uso wake -- vyote huachana na kusambaratika.

Nguvu hii au kani ya uvutano ndiyo ambayo akina Albert Einstein na wanasayansi wabobevu wa nadhari gidamu (string theory) wamejaribu kuchunguza asili na chanzo chake bila mafanikio.
 
Nimeambiwa ni Gravity, lakini sijaambiwa inafayaje kazi hiyo Gravity
Weee jamaaa unabisha kama waha wenye asili ya Kirundi.
Anyway

Mvuto wa dunia (gravity) hufanya kazi ya kuhakikisha hewa inabaki katika uso wa dunia kwa njia kadhaa:

1. Uvutaji wa Molekuli za Gesi: Mvuto wa dunia huvuta molekuli za gesi, kama vile oksijeni, nitrojeni, na kaboni dioksidi, kuelekea katikati ya dunia. Hii inamaanisha kuwa molekuli hizi zinakaa karibu na uso wa dunia badala ya kutoroka kwenda angani.

2. Shinikizo la Anga: Mvuto wa dunia huunda shinikizo la angahewa ambalo ni kubwa zaidi karibu na uso wa dunia na hupungua kadri unavyopanda juu kwenye angahewa. Shinikizo hili husaidia kushikilia gesi kwenye tabaka za chini za angahewa.

3. Uzito wa Molekuli: Molekuli za gesi zina uzito fulani, na mvuto wa dunia huvuta molekuli hizi chini. Molekuli zenye uzito mkubwa zaidi, kama vile oksijeni (O2) na nitrojeni (N2), huvutwa kwa nguvu zaidi kuliko molekuli nyepesi kama hidrojeni (H2) na heli (He). Hii inasaidia gesi nzito kubaki karibu na uso wa dunia.

4. Mzunguko wa Hewa: Mvuto husaidia kudumisha mizunguko ya hewa katika tabaka za chini za angahewa. Mizunguko hii husaidia kusambaza gesi muhimu kama oksijeni na dioksidi kaboni kwenye uso wa dunia na kusaidia katika kudumisha mazingira ya hewa imara.

Kwa sababu ya mvuto wa dunia, molekuli za gesi zinashikiliwa karibu na uso wa dunia, hivyo kuhakikisha kuwa hewa inabaki na kutunza mazingira yanayofaa kwa maisha duniani.
 
Umewahi kusikia maneno kama inertia, centripetal force, centrifugal force, impulse? 😂😂
Wote tunafahamu upepo ukiwa mkali unaweza kusogeza au kuyumbisha vitu, lakini kwa mujibu wa sayansi, dunia inazunguka kwa 1,040mph, mzunguko huo ni wa kasi kubwa lakini hatujawahi kuhisi au kuona kitu chochote kikisogea au kuyumba.

Je ni sababu zipi zinafanya tusihisi au kuona dalili za mzunguko wa dunia?
 
Mgandamizo wa hewa wala hautegemei kwamba hewa hiyo lazima iwe imefungiwa kwenye chombo au eneo fulani lililozibwa pande zote.

Shinikizo au mgandamizo ni kugandamiza (kama neno lenyewe lisomekavyo).

Kitu kimoja kikiwa juu ya kingine, hapo tayari kuna mgandamizo.

Hewa inakuwa na mgandamizo kwa sababu molekyuli moja ya hewa inakandamiza nyingine na nyingine nayo inakandamizwa na nyingine.

Molekyuli za hewa zinakandamizana kwa sababu zina uzito. Molekyuli zina uzito kwa sababu zinavutwa na kani ya dunia.

Mchawi hapa ni uvutano wa dunia. Isipokuwepo kani ya uvutano wa dunia, vitu vinakosa uzito.

Dunia haiwezi tena kushikamana kama ilivyo.

Na wala hakuna kitu chochote kinachoweza kusalia kwenye uso wake -- vyote huachana na kusambaratika.

Nguvu hii au kani ya uvutano ndiyo ambayo akina Albert Einstein na wanasayansi wabobevu wa nadhari gidamu (string theory) wamejaribu kuchunguza asili na chanzo chake bila mafanikio.
Kama mgandamizo wa hewa hautegemei eneo lililokuwa closed, kwanini kuna mitungi ya gesi?
 
Back
Top Bottom