Kama hewa itatoka katika eneo lililo na uwazi, je ni kitu gani huzuia hewa isitoke nje ya uso wa dunia?

Kama hewa itatoka katika eneo lililo na uwazi, je ni kitu gani huzuia hewa isitoke nje ya uso wa dunia?

Ningekuona mwenye busara kama ungesema kwa nini unadhani hayo yaliyofafanuliwa hayaingii akili mwako.
Mkuu kutokuweka neno MWANGU kusikutoe kwenye reli maana hakuna sehemu pia nimesema kwamba hayaingii akilini kwa WATU WOTE,

haikutakiwa kuwa point ya kuilalamikia kwani inakosa neno la kuweka wazi kwamba nilikusudia akilini kwa nani
Eleza sababu ya kutokubaliana nalo. Ndiyo maana umepewa maelezo anuwai na mifano mbalimbali.
Unachosema ni sahihi mkuu,lazima kuwe na maelezo ya kukataa jambo.

Yaani, usikatae wala kupinga jambo fulani tu.
Sababu zinazowekwa nazo zina utata,haziko clear.

Mfano kuhusu gravitational force unaithibitishaje ?
 
Mkuu kutokuweka neno MWANGU kusikutoe kwenye reli maana hakuna sehemu pia nimesema kwamba hayaingii akilini kwa WATU WOTE
Umejuaje? Unaona hadi akilini mwa wengine? Au unapinga ili kupinga tu kama ilivyo ada kwako.

Sasa nadhani huo ndio uongo mkubwa zaidi uliowahi kuusema.

Mfano kuhusu gravitational force unaithibitishaje ?
Achana na uthibitisho kwanza. Je, gravitational force (kani mvutano), unaelewa maana yake?

Tuanzie hapo kwanza.
 
Umejuaje? Unaona hadi akilini mwa wengine? Au unapinga ili kupinga tu kama ilivyo ada kwako.
Wapi nimesema kwamba haiingii akilini kwa watu wote ?
Achana na uthibitisho kwanza. Je, gravitational force (kani mvutano), unaelewa maana yake?
Ni kani mvutano,hiyo ndio maana yake inajieleza katika tafsiri.
 
Umejuaje? Unaona hadi akilini mwa wengine? Au unapinga ili kupinga tu kama ilivyo ada kwako.
Wapi nimesema kwamba haiingii akilini kwa watu wote ?
Achana na uthibitisho kwanza. Je, gravitational force (kani mvutano), unaelewa maana yake?
Ni kani mvutano,hiyo ndio maana yake inajieleza katika tafsiri
 
Kurusha kitu kikaenda juu zaidi sio kwenye space tu, hata ndani ya maji pia.

Lakini binafsi sijawahi kuamini kama kuna mtu amewahi kutoka nje ya dunia(space)
Hakuna aliyewahi kutoka nje ya dunia, achana na ngonjera za NASA.

Juu kabisa mbingu/anga ni maji, na haya ndo yanayoleta mvua n.k enzi za Nuhu Mungu alifungulia madirisha ya mvua kwa kasi na dunia ikajawa maji.

Wakati wa uumbaji alitenga maji ya juu na ya chini, Soma Mwanzo 1:6-7. Sio rahisi mwanasanyansi akakubali hii kitu ila Bible inatueleza.
 
MImi bado sijaona uthibitisho wa kwamba kuna gravity.

Tunathibitishaje kwamba hiyo gravity ipo achilia mbali kwamba fulani amesema ?
Gravity inajidhihirisha, hata kama huioni. Ukitaka kujua ipo, chukua jiwe halafu lirushe kwenda juu kwa nguvu, baada ya ile nguvu yako uliyotumia kulirusha kuisha, lile jiwe linaanza kurudi chini kwa kasi, sasa nini kinavuta hilo jiwe kurudi ardhini? Kwanini lisiendelee tu hadi nje ya dunia? Kinachovuta vitu vyote pamoja kuka duniani ndio kimepewa hilo jina.., ‘Force of Gravity’
 
Mimi bado nafanya tafiti kuhusu hilo.

pia kuhusu Gravity na Mambo mengine, hata mimi niliyasoma nikiwa shule, tena nilikuwa napenda sana hizo topic. Niliamini na nilikuwa na ndoto za kujifunza zaidi kuhusu space.

Lakini kwa sasa nimepata mashaka kidogo kuhusu hii nadharia, na najaribu kudadisi na kufanya tafiti kuhusu nadharia mbadala..

Lengo la kuuliza au kuleta mada hii, ni kujaribu kuona ni namna gani wenzangu bado wanaishi kwa kuamini mambo ya shuleni pasipo kuhoji na kutafakari kwa kutumia akili zao binafsi....
Unafanya utafiti? Are you serious 😂? Hii ndo methodology unahis itakupa majibu
Inaonekana huna skills za research bado huna msingi wa physics sasa unahis utapataje majibu?
Waliofanya tafiti wakagundua Dunia ni duara na inazunguka wamefanikiwa kutengeneza satellites,na vitu vingi vya kianga vinavyosaidia Dunia
Sasa ww unataka ugundue nn au unafanya tu umbea 😂
 
Hiyo center iko wapi ?

Mfano tu sumaku

Unawaza sahihi kabisa.

Ndio maana hapa hakuna anayekuja na jawabu moja linalomake sense.

Wote wanakuja na majibu ambayo hayo majibu yenyewe yana utata.

Mtu anasema gravitational force wakati hiyo gravitational force yenyewe kuithibitisha ni tatizo.

Mtu anasema kwa sababu eti dunia inazunguka,wakati kuthibitisha kama dunia inazunguka pia ni ishu.

So wanakuja na majibu ya kukariri darasani wakati wewe umeuliza swali linalotaka common sense kulifahamu basi waje na majibu yenye common sense kabisa yenye logic.
Huwezi kupata sense kama huna msingi wa hayo mambo mtu anasema hajasoma physics hajui hayo mambo kwa undani unahisi ataelewaje?
Ni sawa na kuangalia mpira na mwanamke atakuwa anauliza tu maswali yasiyokuwa na misingi kuhusu sheria za mpira na hatakuelewa 😂😂😂
 
Swali lako ni muhimu sana na linahitaji ufafanuzi juu ya jinsi angahewa (atmosphere) inavyofanya kazi duniani.

Kwanza kabisa, ni muhimu kuelewa kwamba hewa inayozunguka dunia ipo ndani ya tabaka la angahewa (atmosphere) ambalo linafanya kazi kutokana na nguvu za uvutano (gravitational force) za dunia. Hii mvuto wa ardhi unafanya kazi kama kizuizi cha asili ambacho kinazuia hewa isikimbie kwenda kwenye anga la wazi.

1. Nguvu za Uvutano (Gravity): Nguvu za mvuto wa dunia huvuta hewa na gesi nyingine kuelekea kwenye uso wa dunia. Nguvu hizi zina nguvu zaidi karibu na uso wa dunia na hupungua unapoenda juu. Ndiyo sababu hewa ni nyingi zaidi karibu na ardhi na inakuwa nyepesi zaidi (yaani hewa inavyoongezeka juu haina msongamano mkubwa).

2. Mgandamizo wa Hewa: Mgandamizo wa hewa hutokana na uzito wa hewa uliopo juu kushinikiza hewa iliyopo chini. Hii husababisha hewa kuwa na mgandamizo mkubwa karibu na uso wa dunia na mgandamizo huo hupungua unavyopanda juu.

3. Tabaka za Angahewa: Angahewa ya dunia imegawanyika kwenye tabaka tofauti kama vile Troposphere, Stratosphere, Mesosphere, Thermosphere, na Exosphere. Tabaka hizi zina kiwango tofauti cha mgandamizo na joto, na zote zimeshikiliwa pamoja na nguvu za uvutano wa dunia.

4. Mzunguko wa Hewa (Atmospheric Circulation): Mzunguko wa hewa duniani unachangiwa na joto kutoka kwenye jua. Jua huinyesha uso wa dunia, na kufanya hewa ya chini kuwa joto na kuanza kupanda juu. Hewa hiyo inapofika juu, inapoa, na kushuka tena. Hii mzunguko unasaidia kusambaza hewa duniani kote, kuweka hewa kwa mgandamizo tofauti sehemu mbalimbali.

Kwa hiyo, huku dunia ikiwa ndani ya anga (space) isiyokuwa na mwisho, nguvu za uvutano wa dunia zina uwezo wa kuzuia hewa isikimbie na kuifanya iwe na mgandamizo tukiwa kwenye uso wa dunia. Angahewa la dunia ni kitu cha kipekee kinacholindwa na mvuto wa ardhi ambao umeweka msingi kwa viumbe hai kuishi.
 
Mkuu, This sunday kama ratiba zako zitakuruhusu naomba tufanye online meeting (google or zoom) ningependa tufanye mdahalo then tuzichallenge facts zetu kwa pamoja mimi na wewe.
Kama utakuwa interested naomba unitumie email yako pm tuongee vizuri zaidi
Mkuu wazo zuri hilo, ila kwa sasa nipo milimani nikirudi town tutafanya jambo
 
Mimi naona hii gravity ni ubabaishaji tu,inaact vipi according to weight na kwamba eti the heavier the matter the more it is affected.

Ndege kifaa inaruka juu zaidi ya ndege kiumbe.

Wakati huo ndege kifaa ni nzito kuliko ndege kiumbe.

So tulitegemea hii ndege isiweźe kuruka juu zaidi ya ndege kiumbe kwani ni nzito hivyo ingeathiriwa na gravitational force.

Kwa mantiki hiyo dhana ya kwamba grav.force inaathiri kitu kizito zaidi sio kweli,mbona imeshindwa kuathiri kifaa kizito ndege na inamuathiri binadamu ambae ni mwepesi kuliko ndege ?

Eti mkuu Bob Manson hii imekaa sawa kweli ?
Mkuu, Gravity haina uhalisia wowote, ukirusha jiwe juu lazima lirudi kwasababu ya uzito wake na uwepo wa nafasi isiyokuwa na kizuizi.
 
Hakuna aliyewahi kutoka nje ya dunia, achana na ngonjera za NASA.

Juu kabisa mbingu/anga ni maji, na haya ndo yanayoleta mvua n.k enzi za Nuhu Mungu alifungulia madirisha ya mvua kwa kasi na dunia ikajawa maji.

Wakati wa uumbaji alitenga maji ya juu na ya chini, Soma Mwanzo 1:6-7. Sio rahisi mwanasanyansi akakubali hii kitu ila Bible inatueleza.
Ni kweli kabisa juu kuna maji, kwani mwanzo kabisa palikuwepo maji pande zote, juu na chini, katika yake ndipo ikawekwa dunia
 
Back
Top Bottom