Sasa kama hako kakikundi kadooogooooo ka wanachadema kamelazimisha mahakama ihamie video conference, kama yangekuja mafuriko, basi kesi ingefutwa kabisaaaa!
Hebu nikurudishe 2020. Tundu Lissu alipokelewa na wanachadema kadhaa. Alipokwenda Dodoma kuchukua fomu, kulikuwa na watu wachache sana. Sasa Fast Forward alipofika Dodoma tena wakati wa kampeni. Uliona mtiti ule?
Kwanini? Ni kweli upinzani wana kazi kubwa saaaanaaa ya kuwaunganisha watanzania. Sisi sio kama Kenya. Wala sio kama Zambia. Watanzania wengi ni watii wa mamlaka. Lakini wanataka mabadiliko. Walishayakosa ndani ya ccm, wanayatafuta nje ya ccm. Hili ccm wanalijua, ndio maana hakuna uchaguzi halali Tanzania. Ila watanzania wanapoona hapa kuna uwezekano wa kuiweka kando ccm, wanajitokeza kwa wingi. Ndio maana Tundu Lissu alipata mafuriko ya watu siku za mwishoni wa kampeni. Na ndio maana ccm walianza kumwekea vikwazo kibao.
Kwa kufanikiwa huku, believe me, si wanachadema tu, bali watanzania wengi zaidi watampigania Mbowe. Na kama rais Samia anajitetea alikuwa kweli ana nia ya kukutana na wapinzani, "ratiba zikaingiliana", basi maana yake atalazimika kutafuta namna yakukutana nao