Kama hii ni kweli, basi tumefika pabaya sana

Kama hii ni kweli, basi tumefika pabaya sana

Vitu vingine ukisikiliza vinasikitisha sana na maswali ni mengi kushinda majibu; kuna wahalifu wanajiamini sana nchi hii kuweza kufanya uporaji wa hadharani namna hii. Simply ni dharau kwa vyombo vya sheria ni watu ambao wanajiamini wapo juu yake; na kwa story yenyewe uwezi bisha wapo juu ya mkono wa sheria.

Jana tu kwenye thread ya Kabendera nili comment kuna uhalifu Tanzania auwezekani bila ya taasisi za ulinzi na usalama kuhusika; sasa kama ni issue za national security waanze kusafisha ndani ya nyumba za serikari kwanza (a lot of their employees can easily be compromised).
 
kuna uhalifu Tanzania auwezekani bila ya taasisi za ulinzi na usalama kuhusika; sasa kama ni issue za national security waanze kusafisha ndani ya nyumba za serikari kwanza (a lot of their employees can easily be compromised).
Uhalifu unaweza kuanzia serikalini kweyewe na viongozi wake wanaovisimamia vyombo hivyo.

Kiongozi ukikiuka sheria na kuamru vyombo unavyoviongoza vitimize uhalifu huo, huwezi kugeuka nyuma na kusema ni vyombo vinavyofanya uhalifu.

Ni kwa namna hiyo hiyo, hata wakuu wa vyombo hivyo wanapoona mkuu wao anawatumia kukiuka taratibu na sheria, wao pia watatafuta njia zao wenyewe kukiuka, hali kadhalika hata mtu wa ngazi ya chini kabisa anapotambua kwamba anatumika kufanya kazi yake kwa kuamrishwa kukiuka sheria na taratibu, yeye pia atajiwekea njia zake za kukiuka taratibu za kazi yake.

Kwa hiyo tusigeuke tu hapa na kuelekeza lawama kwa watu ambao pengine lawama haziwahusu.
 
Kalamu1,
Ebu tuache kugeuza kila kitu siasa.

Hapa kuna uhalifu wa mchana kweupe nje ya hapo kuna uzembe uliokithiri na so many administration issues mpaka mtu unajiuliza kama kweli jeshi la polisi linafanya kazi ivyo something is very wrong.

Aiwezekani mtu aishi Tanga ashindwe kwenda kuripoti ofisi za NIDA, TRA na Polisi; vilivyopo mkoani shida zake zitatuliwe mpaka aanze kuzungushwa safari za mikoani.

Ni jukumu la hizo taasisi kufanya coordination za kazi zao; mungu huo usumbufu tu alioupata unamuonea huruma wakati kwa jinsi swala lilivyo sensitive ulitegemea NIDA, TRA na Polisi wawe mstari wa mbele maana taasisi zao zime hujumiwa and that could lead to public mistrust katika shughuli zao.

Aiwezekani serikari itumie mabillioni kutuambia vitambulisho vya NIDA ni salama watu wanatoa fingerprint kuvipata na vinatumiwa kusajili au kama sehemu ya affidavit; halafu mtu aweze sajili kwa jina la mwingine that is a very serious breach.

Huyu mtu akisajili line ya simu akatumia mtandao vibaya, akafanya utapeli au chochote; TCRA au hao polisi wangemuelewa huyo aliyefanyiwa forgery kweli siyo yeye aliyetenda hayo makosa?

Kwanini hilo swala wanalichukulia lightly kutaka kujua how is that possible kupata hizo nyaraka wakati wametumia mabillioni ya card za kidigitali na ambazo zinaweza kuwa scanned.

Bado ata ujazungimzia utapeli wenyewe and how the whole thing was handled. If you ask me this is one of the very serious issues of breach and mistrust ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.

The poor guy tumuombee mambo mengine tuyasikie kwa wengine tu; hila this is very very very wrong at all levels na tuache siasa kwenye kila kitu.
 
Kalamu1,
Umeongea yaliyokuwa kwenye akili yangu. Yaani Raisi na watwala wengine wanawatuma vyombo vya dola kudanya uhalifu huku wakijua kabisa ni uhalifu. Unategemea wao binafsi wakikwama katika jambo fulani wasifanye ihalifu kama boss wao?? Watafanya sana tu wakijia boss hawesi kusema kitu maana wanajua maovu yake.
 
Kilatha,
TRA, POLISI,TAKUKURU, UHAMIAJI vimetumiwa sana na watawala kufanya uhalifu dhidi ya watu wanaoikosoa serikali hii ya awamu ya tano. Wale individual staff wa hivyo vyombo nao wakiamua kutumia ujuzi wao kiuhalifu wanaona hakuna wakuwakemea wala kuwazuia maana wana kibri cha kiwa karibu na hao wanaowatumia. Ndio maana usishangae uhalifu unafanywa mpaka unajiuliza hawa wanaoitwa TISS kasi yao ni kufatilia wanasiasa tu??
 
Pythagoras,
Clearly we ujali maasibu aliyokutana nayo huyo bwana. Maana umekadhania kuliweka swala lote kwenye political perspective.

Swala la polisi na siasa linasimama peke yake.

Na hili la raia kutotendekewa haki baada ya kunyan’nganywa (maana huu ata sio utapeli wa kutumia maarifa) ni sawa na mmbabe kuja kwako kuchukua mali yako mbele ya mashahidi na vyombo tunavyotakiwa kuviamini kutofanya lolote; isitoshe na usumbufu juu apewe yeye.

Sijapata kusikia duniani mshitaki anaambiwa alipiye yeye gharama za kumsafirisha mtuhumiwa kutoka kituo kimoja hadi kingine cha polisi tena afanye na negotiation ya gharama juu halafu polisi aamue kufanya kazi kutokana na dau analopewa la; only in Tanzania.
 
Back
Top Bottom