Elections 2015 Kama hii ni kweli, then serikali yetu ni serikali dhalimu na haramu? Hukumu ya karma ijuu yake!

Na kama ni kweli Magufuli ameupata urais wa Tanzania kwa hila, na udhalimu, then tutashuhudia utawala wa mkono wa chuma, the reign of iron hand. Mtashuhudia udikiteta na udhalimu wa ajabu, kuna watu kwa sasa wanashangilia, lakini mwisho wa siku, watakuja kulia na kusaga meno!.

Kama uchaguzi mkubwa hivi wa rais na wabunge kumeweza kufanyika hila, hii inamaanisha kule ambako wapinzani wameshinda ni maeneo ambako hila zimeshindikana, hivyo kwa uchaguzi wa 2020, wapinzani jiandaeni kuyarejesha majimbo karibu yote na nchi kurejea kwenye mfumo wa chama kimoja.

Kipimo cha hili kitapimwa kwa chaguzi ndogo zozote zitakazotokea hapa katikati, kwanza upinzani hautaweza tena kushinda uchaguzi wowote, na kama kiti cha ubunge au udiwani kilichokuwa kinashikiliwa na upinzani kitakuwa wazi, uchaguzi wa marudio utakirudisha CCM kwa mbinu zile zile dhalimu by hooks and crooks!.

Kwa hili hasiri ya Mungu itawaka juu ya Tanzania yetu, tutapata mabalaa na majanga ya ajabu kwa sababu ya hasira ya Mungu, na as taifa tutasuffer ba kuna watu wataangamia!.

Ila pia, endapo tuhuma hizi ni za uongo, ni za kupika na ni uzushi, then John Pombe Magufuli, ndiye rais chaguo la Mungu kwa Tanzania aliyetangazwa mshindi siku yake ya kuzaliwa!, katika uchaguzi huru na wa haki, hivyo atasimama test in time, of which time will tell!.

Tanzania itapata neema, mafanikio na maendeleo ya ajabu kwa sababu ya baraka za Mungu zitakuwa juu yake, nchi yetu inakwenda kageuka kuwa ni ile nchi ya ahadi ya maziwa na asali.

Neno litasimama, mambo mengine yote yatapita, lakini neno litasimama!.

Mungu ibariki Tanzania.

Paskali
=====================

Ni wachache sana wenye akili kama hizi, tena niwe mkweli, sijawahi kumsifia mtu kama hivi. Ila Pascal Mayalla ni mtu uliyejaaliwa akili nyingi na uwezo wa kutazama mambo kwa mbali!. Hongera kwa hilo

Yote yaliyotabiliwa nawe ndo tunayoyashuhudia na mbaya zaidi hatujui tutatoka vipi kwenye mkwamo huu.. ni kama tumelidhika vile..!!

BACK TANGANYIKA
 
Nimekukubali@Pascal Mayalla naona kabisa mkono wa chuma na mengine zaidi ya kuhujumu upinzani. Kimsingi bandiko lako hili la 2015 leo 2018 lina tupatia mwanga. So it is a .. Karma
 
Ulitabiri mkuu yote yanatokea sasa Pascal Mayalla
 
Hakika hili jambo ulishuhudiwa na ROHO MTAKATIFU!

Bwana wa Majeshi azidi kukubariki na karama nyingi zaidi pascal, Ahimidiwe Bwana wa Majeshi milele na milele Amina.
 
Nafanya tuu tafakuri kuhusu mambo fulani ya kitu kinachoitwa karma kuhusiana na majanga mbalimbali.
P.
 
Nafanya tuu tafakuri kuhusu mambo fulani ya kitu kinachoitwa karma kuhusiana na majanga mbalimbali.
P.
Tafakuri yako iko vizuri sana, Mshukuru Mungu kwa kukujalia karama ya kuona mbali. kuna wengine wakifanya tafakuri kidogo tu njaa inauma na wanahamia CCM na uchaguzi unarudiwa, na walala hoi wanakuwa hoi Zaidi, wengine wanapata ajali kwenye vyombo vya usafiri wa majini ambavyo havina hata maboya, watu wanajazana ovyo, hakuna utaratibu wowote.

Uko vizuri mkuu, Hongera sana
 
Ushauri wa bure kwa Lowassa, Najua anaunga mkono juhudi, kwanza halafu kwa kwenda ikulu kinyemela, kwenda kupongeza, na sasa kuanza kahudhuria shughuli mbambali za maendeleo zinazo hutubiwa na rais Magufuli.

Nami nimpongeze Mhe. Lowassa, kwa the spirit upinzani sio uadui, now its just a matter of time tuu naye ataunga mkono juhudi.

Ombi moja kwake, kama alivyotoa statement hii kwenye bandiko hili, then atoe statement nyingine kilikanusha hii statement ya bandiko hili kwa kusema hii statement ilikuwa ni uongo tuu, ni siasa tuu, sisi wapenzi wake na wafuasi wake, tutamwelewa.

Na akiunga rasmi mkono juhudi, sisj nasi, tutaunga naye.

P
 
Watumishi fanyeni hujuma indirect dhidi ya serikali hii onevu kwenu ni miaka mitatu hakuna ongezeko la mshahara na maslahi yenu yanazidi kukandamizwa.
 

Pascal bhana, sasa unataka kusemaje?

Sheria ya karma hufuata penye shida...sawa na ulivyosema tusubiri baraka au laana
 
Baada ya Lowassa kusifiwa na rais Magufuli kuwa ni super man, nimemkumbuka naomba nimdurusu kidogo, niliwaji kusema nini humu kumhusu mtu huyu.

P.
 
Kufuatia kujitokeza kwa wafananishaji hoja humu jf, naomba kujitokeza kuliwekea caveat bandiko langu hili, lisije likafananishwa. Ajali ya Msamvu, iliyotokea leo asubuhi na kusababisha vifo vingi, ni ajali tuu ya janga, yaani tragedy, ilijitokea tuu, na sio miongoni mwa majanga na ma balaa niliyoyasema kwenye bandiko hili!.
P.
 
Mkuu Respect wa Boda, mimi sio mtabiri!.
P
 
Wanabodi,
Kitu kizuri kuhusu haki, haki kamwe huwa haipotei, hata kama sio kwa dunia hii, bali kwa dunia ijayo, na ubaya siku zote huwa haulipi na malipo yote ni hapa hapa duniani, hata kama sio kwako, then kwa kizazi chako!.
Kuna kitu niliwahi kukisema kwenye bandiko hili kuhusu udhalimu.

Zuio la Marekani kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ni uthibitisho wa mwanzo kuwa kuna udhalimu fulani unaofanywa na serikali yetu kupitia kwa baadhi ya viongozi wake kwa kuwatendea visivyo Watanzania.

Kitendo cha taifa la nje kushindwa kuvumilia hadi kuweka zuio ni uthibitisho kuwa
1. Ama wakubwa hawa wana jicho kali lenye uwezo wa kuona mbali na ndani kuliko uwezo wa jicho la serikali yetu, hivyo sasa baada ya kumzuia Makonda, serikali itaonyesha ushirikiano na Marekani kwa kuomba ipewe hizo taarifa na ikizithibitisha, then Makonda apewe haki yake sawasawa na matendo yake.
2. Ama yote Makonda anayotuhumiwa nayo serikali ya Marekani ni mambo ya kweli, na serikali ama unajua na imenyamaza, au serikali ndio ilikuwa inamtuma Makonda kuyatenda hayo ndio maana inamlinda, na hata sasa baada ya tuhuma hizi za Marekani, bado serikali itaendelea kumlinda na kumbeba. Na huu sasa ndio utakuwa ni uthibitisho wa udhalimu, na hapa Makonda hatakuwa peke yake, watakuwa wengi wakiongozwa na mtoa amri!, hivyo kama hii ya pili ni kweli, then kitu pekee kinachoweza kuishughulikia serikali ya aina hii inayofanya udhalimu kwa watu wake ni karma pekee!.

P
 
Mkuu pasco
Nimesoma kwa kina hili bandiko lako na nimegundua kuwa limejibu indirect, maswali uliyoyaacha katika ule uzi wa 2014 ,kuwa next President COULD BE JOHN POMBE MAGUFULI

Katika hili bandiko umejibu kwa kujua au kutokujua sababu za Magufuli kuwa Rais ambazo ulikataa kuzitaja katika uzi wa 2014 na baada ya jamaa kuwa rais

Asante sana kwa majibu yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, naheshimu sana upeo wako sichoki kukufatilia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Respect wa Boda upo? Mawazo yako haya yanaishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…