Mkuu uko right, karma inafuata mising ya cause and effects, na ukiishamaliza kulipa, unakuwa set free!, mimi niliamini Lowassa aliishailipia bad karma yake kwa wema alioutenda na kidogo iliyobakia ndio hiyo anayoendelea kuilipa kwenye hali ya afya yake!, hivyo by the time anagombea, he is a clean man out of bad karma!, ila pia it is possible maovu yake yalikuwa yamepitiliza hivyo ameyafidia kwa kuukosa urais!. With karma!, no one can tell, ndio maana nimemaliza kwa kauli hii
Pasco
Post zako nyingi sana zina mashiko,lakini inanisikitisha sana kwamba kuna jambo moja ambalo linafanya yote hayo unayozungumza yakose tija.Jambo hili lisingekuwapo,basi yale unayozungumza yangekuwa na maana na tija kubwa kwa watanzania.
-Jambo hili ndilo lililonifanya nisipoteze muda kujiandikisha kupiga kura kwa muda mrefu sasa ingawa wengi wanaonifahamu walinipinga.
-Jambo hili ndilo linalofanya mchakato wa katiba mpya usifanikiwe.
-Jambo hili ndilo linalofanya hata baadhi ya vifungu katika katiba ya sasa visifuatwe.
-Jambo hili ndilo linasababisha mambo mengi machafu yasiyo na idadi kiasi cha kushindwa kuyaweka yote hapa ubaoni.
Jambo hili ni 'watu wanaotuongoza nyuma ya pazia' au naweza kusema 'dark government'/serikali isiyoonekana.Watu hawa si ule mfumo wa CCM kama wengi wanavyofikiri na wala si usalama wa taifa.Hawa ndio wanaomuweka rais wamtakaye madarakani,na hata wakimuweka rais aliyechaguliwa na wananchi basi lazima afuate matakwa yao kwenye mambo mazito mazito yanayohusu uchumi.Watu hawa wana elimu ya juu zaidi kuliko sisi.
Jambo hili wengi hulidharau na kulichukulia kama ni hadithi za Abunuasi kujenga nyumba angani.Ndio maana hatufanikiwi kwa muda mrefu sana katika masuala ya kisiasa na uchumi kutokana na kilema hiki tulichonacho cha kutojua ukweli huu.Cha msingi ni kujua kiini cha tatizo,halafu ndio tujue jinsi ya kulitatua tatizo.Sina maana kwamba hatuwezi kushindana na watu hawa,bali elimu na ujuzi wa kiini cha tatizo ndio msingi wa utatuzi,sisi hatujui kiini cha tatizo,tunagusa juu juu tu.
Hili ni suala pana sana,linanipa uvivu kuandika kila kitu.Lakini tutake tusitake,ukweli ni kwamba rais wetu akiwa na urafiki na watu hawa lazima awe adui na wananchi wake,vinginevyo,rais wetu akiwa rafiki wa wananchi wake,basi lazima awe na uadui na watu hawa.Ukiwa na urafiki na watu hawa,kamwe huwezi kushitakiwa na kuhukumiwa kwenye ile mahakama ya kimataifa bila kujali kama umeua watu wangapi nchini kwako.Watu hawa wakisema wanamtambua Lowassa kama rais basi atakuwa rais,wakisema wanamtambua Magufuli kama rais basi atakuwa rais.Wananchi hawana maamuzi juu nchi yao.(Rejea statement ya Joseph Stalin wa Urusi ya zamani kuhusu wananchi na uchaguzi).
Tuko gizani,ukombozi pekee tulionao sasa ni elimu sahihi kuhusu kiini cha tatizo,na si ushabiki.Tusidanganyike kwamba eti serikali yetu inasaini mikataba mibovu,ukweli ni kwamba serikali inasainishwa mikataba mibovu,haisaini kwa ridhaa yake.Nani anaijua mikataba ya madini mfano gesi na urani?Mkiijua mtalia sana,ni bora msiijue ili muishi kwa amani rohoni mwenu.Nani anajua kwanini Kiwete alikwenda sana Marekani kabla ya uchaguzi?Sehemu kubwa sana za muhimu katika nchi hii zimeshauzwa na nyingine tumesainishwa mikataba inayodumu kwa zaidi ya miaka 80 au 90?Kiini cha tatizo ndio mpango mzima.
Huwezi kutatua tatizo kwa kutaka katiba mpya bila kujiuliza kwa nini hata ile iliyopo haitekelezwi.Kama watu wanakiuka hata mafundisho ya Mungu wao kwenye misaafu,itakuwa katiba iliyoandikwa na binadamu?
Mifumo katika sekta ya elimu,afya,madini,kilimo na viwanda imekamatwa kisawasawa na watu hawa.Huwezi kuboresha sekta hizo nilizozitaja kama una urafiki na watu hawa.Wapo waliowahi kupingana na watu hawa lakini hivi sasa hawapo kwenye uso wa dunia.Najua pia kwamba kuna udhaifu binafsi wa viongozi ambao hauchangiwi na watu hawa,lakini ukweli unabaki palepale kwamba watu hawa ndio wameshikilia sehemu kubwa muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.
Huu ndio mfumo/utawala ulio nyuma ya pazia/dark government ambao ndio unaathiri hatua yoyote ya kimaendeleo nchini kwetu.Kikwete alijiamini sana kwamba CCM watashinda kutokana na kuahidiwa na watu hawa.
Mambo yaliyojificha yanayoonesha kwamba hawa viongozi wetu wana ujamaa na watu hawa;
1.Angalia Kikwete jinsi anavyosalimiana na Obama,halafu linganisha na Kikwete jinsi alivyo grip mkono wake na Magufuli jana.
2.Angalia Uhuru Kenyata jinsi alivyosalimiana na Obama na John Kerry.
3.Fautilia Kikwete jinsi alivyosalimiana na Uhuru Kenyata.
Haya ni kwa uchache tu.Watu wanaweza kuona kama ni maigizo,lakini haya yanaashiria kuna nguvu kubwa inayotutawala,tusipopata elimu sahihi kuhusu jambo hili tutaendelea kutawaliwa milele huku tukibaki kufanya ushabiki wa vyama vya siasa kama ilivyo kwenye soka.