Wanabodi,
Kuna hii tuhuma iliyotolewa leo na Edward Lowassa.
Kama tuhuma hii ni kweli, then serikali ya Magufuli ni serikali haramu na serikali dhalimu!. Kwa mujibu wa katiba yetu, Tume ya Uchaguzi, ikiisha kumtangaza fulani ndie mshindi, kwa tangazo hilo ndio limehitimisha rasmi mchakato wote wa urais.
Mgombea urais akiishatangazwa kuwa ni mshindi, regardless amepatikanaje, kihalali au kiharamu, by means of hooks or crooks, kwa bao la kisigino, faulo au bao la mkono, as long as yeye ndie ametangazwa mshindi, this is the end that justifies the means!, there is nothing more anyone can do, ukubali usikubali matokeo, uwe ulimchagua, au hukumchagua, umtambue, au usimtambue, its never gonna change a thing!, huyu sasa ndie rais wetu and this is a fact!.
Kitu kizuri kuhusu haki, haki kamwe huwa haipotei, hata kama sio kwa dunia hii, bali kwa dunia ijayo, na ubaya siku zote huwa haulipi na malipo yote ni hapa hapa duniani, hata kama sio kwako, then kwa kizazi chako!.
Then namshauri Edward Lowassa, kuwa umetimiza wajibu wako, kutaka kuwatumikia Watanzania!. Umefanya kazi yako, imekamilika!. Sasa nakuomba statement yako hii iwe ndio ya mwisho, usiendelee kulalamika popote, bali sasa nenda zako kajipumzikie kwa amani kwa kuchunga ng'ombe wako kama ulivyoahidi, tena usipeleke malalamiko yako mahali pengine popote zaidi ya kwa aliye JUU, hivyo haya meingine yote muachie Mungu!, YEYE ndiye atakulipia!. kuna mahakama ya haki kuliko mahakama zote za dunia hii, au za ulimwengu huu!, hii ni mahakama ya karma, ndio mahakama pekee ya haki bin haki!.
Kwa wale wote waliomchagua Lowassa lakini haki zenu zikadhulumiwa, poleni sana!, Mungu atawalipia.
Na wale wengine wote wanaoshangilia ushindi haramu, ushindi dhalimu, hawa wanashangilia ujinga!, hawa nao pia watakuwa na sehemu ya malipo yao kwenye karma.
Neno litasimama, mambo mengine yote yatapita, lakini neno litasimama!.
Ila pia, endapo tuhuma hizi ni za uongo, ni za kupika na ni uzushi, then John Pombe Magufuli, ndiye chaguo la Mungu la rais wa Tanzania aliyetangazwa mshindi siku yake ya kuzaliwa!, hivyo atasimama test in time, of which time will tell!.
Mungu ibariki Tanzania.
Pasco
Kwa rejea mambo ya karma, karibu mitaa hii
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili
"Bora Katiba", Tuikubali!, Tusiichukie CCM!, Kwa Sababu
When Karma comes calling, she stings like a bitch
Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanaz
"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu ya Miujiza Ya Uponyaji kwa
Hapa ndo udhaifu wa mwafrika ulipo. Hatukubali matokeo. Tunatafuta kila sababu ili tu tuonekane tumeonewa ili tuwaridhishe washabiki wetu.
Washabiki wote wa Lowasa lazima wawe wakweli na mmwambie ukweli Edward Lowasa kuwa Kura hazijatosha. Hizo kura million 10 anazosema amepata wekeni tu mfano wa majimbo matano ya kuonesha tofauti ya kura zilizohesabiwa na kusainiwa majimboni na zile zilizosomwa na tume ya Uchaguzi.
Wakati matokeo ya Ubunge majimboni yakisomwa hakuna hata mmoja aliyekuja na mfano hata mmoja. Zimekuwa zikitengenezwa tofauti za kuumba (Tunduma na Bumbuli) ambazo zote zimekuwa debunked na rekodi sahihi za tume na majimboni.
Kama EDO anajua kuna wizi na anajua ulivyofanyika; aje na mifano ya rekodi, siyo sweeping statements kwamba alipata kura million 10. Kampeni za mijini tu kwenye wapiga kura 30% na kununua media (TV na Magazeti) haitoshi. Unahitaji wapiganaji on the ground. Hakuna vita ambayo imeshawahi kushindwa kwa kutumia air power na pyschological warfare peke yake. You need ground solders. Hao maeneo mengi ya nchi hawakuwepo; ukiachana na mikoa miwili ya Arusha na Kilimanjaro pekee.
Edo is dangerously polarizing na hilo ni mojawapo ya matatizo yake makubwa. Wakati ana win hardcore supporters, methods zake vile vile zinafanya apate hardcore opponents. Si mkusanyaji, ni mtawanyaji. Challenge ya kwanza kuunganisha Upinzani alishindwa and he nearly killed Ukawa.
Magufuli hakuhitaji wizi wa kura kushinda huu uchaguzi, wala CCM haikuhitaji wizi wa kura kushinda majimbo mengi. Walichohitaji ni Ukawa iliyokosa mwelekeo. Hakuna mtu hata mmoja aliyeweza kusimamia hoja ya katiba ya warioba na kuielezea vizuri. Hiyo inaonesha kwamba, kampeni ya Edo ilijaa wadandiaji, si watu original waliokuwa wakijua Ukawa inasimamia nini. Matokeo yake walipoteza mwelekeo wakafanya kampeni ya kutoa ahadi; kampeni ambayo haikuwatofautisha na CCM. Wananchi wengi wanajua kuwa hizo ahadi ni uongo na nyingi hazitekelezeki.
Wananchi walitaka kusikia alternative thinking. Edo alitegemea Mbowe, Sumaye na Kingunge kuwa ndo wasemaji wakuu. Ni vigumu sana kuwashawishi watanzania wengi kuwa Sumaye na Kingunge ni watu tofauti na wale waliokuwa CCM. Mbowe watanzania walishamkataa mwaka 2005.
Tulitarajia Lowassa aongozane na Kina Lissu, Mnyika, Mwalim, Lema, Mdee ili kuwaonesha wanachadema wa siku zote kuwa Lowasa ni Chadema. Hilo halikutokea. Watu hao wote walijichimbia majimboni kwao kupigania uhai wao Bungeni.
Kwa kufanya uchambuzi makini usio na chembe ya unafiki, ni wazi hizo kura million 10 anazodai kuzipata Edo ni za kupikwa na washabiki wake wanaotaka kuendelea kufaidi mfuko wake.
Ataheshimika sana hata akikaa kimya tu. Kura milioni kumi akiulizwa ushahidi uko wapi itakuwa kichekesho!