Hapa ndo udhaifu wa mwafrika ulipo. Hatukubali matokeo. Tunatafuta kila sababu ili tu tuonekane tumeonewa ili tuwaridhishe washabiki wetu.
Washabiki wote wa Lowasa lazima wawe wakweli na mmwambie ukweli Edward Lowasa kuwa Kura hazijatosha. Hizo kura million 10 anazosema amepata wekeni tu mfano wa majimbo matano ya kuonesha tofauti ya kura zilizohesabiwa na kusainiwa majimboni na zile zilizosomwa na tume ya Uchaguzi.
Wakati matokeo ya Ubunge majimboni yakisomwa hakuna hata mmoja aliyekuja na mfano hata mmoja. Zimekuwa zikitengenezwa tofauti za kuumba (Tunduma na Bumbuli) ambazo zote zimekuwa debunked na rekodi sahihi za tume na majimboni.
Kama EDO anajua kuna wizi na anajua ulivyofanyika; aje na mifano ya rekodi, siyo sweeping statements kwamba alipata kura million 10. Kampeni za mijini tu kwenye wapiga kura 30% na kununua media (TV na Magazeti) haitoshi. Unahitaji wapiganaji on the ground. Hakuna vita ambayo imeshawahi kushindwa kwa kutumia air power na pyschological warfare peke yake. You need ground solders. Hao maeneo mengi ya nchi hawakuwepo; ukiachana na mikoa miwili ya Arusha na Kilimanjaro pekee.
Edo is dangerously polarizing na hilo ni mojawapo ya matatizo yake makubwa. Wakati ana win hardcore supporters, methods zake vile vile zinafanya apate hardcore opponents. Si mkusanyaji, ni mtawanyaji. Challenge ya kwanza kuunganisha Upinzani alishindwa and he nearly killed Ukawa.
Magufuli hakuhitaji wizi wa kura kushinda huu uchaguzi, wala CCM haikuhitaji wizi wa kura kushinda majimbo mengi. Walichohitaji ni Ukawa iliyokosa mwelekeo. Hakuna mtu hata mmoja aliyeweza kusimamia hoja ya katiba ya warioba na kuielezea vizuri. Hiyo inaonesha kwamba, kampeni ya Edo ilijaa wadandiaji, si watu original waliokuwa wakijua Ukawa inasimamia nini. Matokeo yake walipoteza mwelekeo wakafanya kampeni ya kutoa ahadi; kampeni ambayo haikuwatofautisha na CCM. Wananchi wengi wanajua kuwa hizo ahadi ni uongo na nyingi hazitekelezeki.
Wananchi walitaka kusikia alternative thinking. Edo alitegemea Mbowe, Sumaye na Kingunge kuwa ndo wasemaji wakuu. Ni vigumu sana kuwashawishi watanzania wengi kuwa Sumaye na Kingunge ni watu tofauti na wale waliokuwa CCM. Mbowe watanzania walishamkataa mwaka 2005.
Tulitarajia Lowassa aongozane na Kina Lissu, Mnyika, Mwalim, Lema, Mdee ili kuwaonesha wanachadema wa siku zote kuwa Lowasa ni Chadema. Hilo halikutokea. Watu hao wote walijichimbia majimboni kwao kupigania uhai wao Bungeni.
Kwa kufanya uchambuzi makini usio na chembe ya unafiki, ni wazi hizo kura million 10 anazodai kuzipata Edo ni za kupikwa na washabiki wake wanaotaka kuendelea kufaidi mfuko wake.
Ataheshimika sana hata akikaa kimya tu. Kura milioni kumi akiulizwa ushahidi uko wapi itakuwa kichekesho!