Kama hoja ni Ufanisi wa Bandari Nawaza hivi..

Kama hoja ni Ufanisi wa Bandari Nawaza hivi..

Bwana Bima

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2014
Posts
429
Reaction score
929
1)Fanya utafiti yakinifu na makini kubaini gharama,namna bora ya uendeshaji,faida na mengineyo watu wa project wanaweza kunisaidia. Weka mipango mirefu na mifupi na kufanya tafiti za mara kwa mara kuona malengo yamefika wapi

2)Tafuta wataalam waliobobea kwenye maswala ya uendeshaji wa bandari kutia mafundi na waendesha mitambo kutoka nchi zilizoendelea kama Uk,USA, GERMAN,CHINA na zinginezo wape vitengo muhimu then nyuma yao wawe wazawa ambao ni wazalendo.Isipokua kama ilivyosasa bandar ni moja ya kanda kama sikosei ya kipolisi ibaki kama ilivyo llakini iwe chini ya usimamizi mkali wa ofisi ya raisi

3)Nenda taasisi kubwa za kifedha upate mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya uendeshaji kutia ndani kununua mitambo ya kisasa na vifaa vya kisasa ili kuendesha bandari kwa ufanisi.

Mengine mtanisaidia ikiwa. Ila kwa nchi yangu daah mengine nachekaga tu. Mfano hai kipindi mitihani ya Necta inachapishwa nje ya nchi mpka JPM alipoingia na kuamuru mitambo inunuliwe iwe inachapishwa hapa hapa. Hili jambo na mengine vinafanya viongozi wa nchi yetu waonekana sijui wanawaza kwa kutumia nini aisee!
 
Ufanisi ni geresha tu, wewe nitajie taasisi gani ya serikali INA ufanisi 100%.
TRA wenyewe wafanyabiashara kibao hawalipi kodi bidhaa za laki 5 risiti ya elfu 60. Basis tuikodishe TRA kwa watu wengine ili ituingizie mapato
 
Shida yenu ni dubai,mbona hata hao usa wanawatumia hao dp world?
 
Hapo ndo napochokaga na hizi taasisi. Lakini sehemu zote hizo ni wasimamizi mbovu na kuweka watu kwa kujuana ndo kunazimaliza hiz taasisi.
 
Nasikiaga wanasema Uraisi ni taasisi basi nayo ipangiswe maana imeshindwa kusimamia bandar zetu
 
1)Fanya utafiti yakinifu na makini kubaini gharama,namna bora ya uendeshaji,faida na mengineyo watu wa project wanaweza kunisaidia. Weka mipango mirefu na mifupi na kufanya tafiti za mara kwa mara kuona malengo yamefika wapi

2)Tafuta wataalam waliobobea kwenye maswala ya uendeshaji wa bandari kutia mafundi na waendesha mitambo kutoka nchi zilizoendelea kama Uk,USA, GERMAN,CHINA na zinginezo wape vitengo muhimu then nyuma yao wawe wazawa ambao ni wazalendo.Isipokua kama ilivyosasa bandar ni moja ya kanda kama sikosei ya kipolisi ibaki kama ilivyo llakini iwe chini ya usimamizi mkali wa ofisi ya raisi

3)Nenda taasisi kubwa za kifedha upate mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya uendeshaji kutia ndani kununua mitambo ya kisasa na vifaa vya kisasa ili kuendesha bandari kwa ufanisi.

Mengine mtanisaidia ikiwa. Ila kwa nchi yangu daah mengine nachekaga tu. Mfano hai kipindi mitihani ya Necta inachapishwa nje ya nchi mpka JPM alipoingia na kuamuru mitambo inunuliwe iwe inachapishwa hapa hapa. Hili jambo na mengine vinafanya viongozi wa nchi yetu waonekana sijui wanawaza kwa kutumia nini aisee!
Sahihi kabisa, iwapo hospitali ya Muhimbili, taasisi zake mbili ile ya moyo na ya mifupa zimeweza kufikia viwango vya kimataifa, Bandari zetu zinashindwa kuagiza mashine za uhakika na kusomesha wataalamu kweli?...

Bandari ni shamba la bibi la viongozi wetu kupitia makampuni ya kigeni...

Tuwazomee tu!
 
Sahihi kabisa, iwapo haspitali ya Muhimbili, taasisi zake mbili ile ya moyo na ya mifupa imeweza kufikia viwango vya kimataifa, Bandari zetu zinashindwa kuagiza mashine za uhakika na kusomesha wataalamu kweli?... Bandari ni shamba la bibi la viongozi wetu kupitia makampuni ya kigeni...Tuwazomee tu!
Bonge la point.kushindwa kwa taasisi nyingi ni rushwa,siasa na kuweka watu ambao hawastahili kama ulimsikia Assad alisema hawa watu wa bodi inabd sasa hv nafasi ziwe zinaombwa sio wateuliwe
 
Shida yenu ni dubai,mbona hata hao usa wanawatumia hao dp world?
Leta uthibitisho

Usichokijua hawa DP world walivyo enda USA kupeleka proposal yao walipewa 24hrs wawe washaondoka USA
 
tuvunje mjadala, DP WORLD iendelee kuwepo Tanganyika, ila
1. wabadilishe vipengele vya mkataba, visiwe vinatuumiza sisi tu.

2. wasituzuie kujenga au kuendeleza bandari zingine, wao wapewe tu DSM, na sisi tuwe na uhuru kuruhusu wawekezaji wengine kujenga bagamoyo, tanga, mtwara n.k na za kwenye maziwa ili washindane nao, pakiwepo ushindani ndio ufanisi utakuwepo. imagine leo hii tungekuwa na mtandao wa vodacom tu hakuna halotel wala tigo, voda wangeringa sana. hivyo dp world wasitupangie kwamba wakishida dsm sisi tusiendeleze kwengine bila kuwataarifu wao, kwenye nchi yetu.

3. kama wananchi wamewakataa, tusilazimishe wakubalike kwasababu tu wamechangia kujenga msikiti Mbeya au kwasababu ni waarabu au waislam. tusiwalete kwasababu ya udini wao, na tusiwakatae kwasababu ya dini yao, bali vigezo vya kwenye mkataba.
 
Back
Top Bottom