Stamina ft Fid Q - Wazo la leo
you know what majani?
nice to meet you homie!
yeah
elimika nyangema, maisha hayaendeshwi na
nguo
Pesa ni vazi la ngema, haliwezi kuwa na
mpasuo
vaa uaminifu, tupa boksi la kondomu
Hip Hop haijengwi na beef, underground
usiijaze form
maisha ni kujipanga, ewe mganga usigawe hirizi
viogonzi msiizuie ganja, huku mnachukua
ushuru wa lease
ridhiki ina kamba, ivute ili ikupe noti
mkulima rudi shamba, nahisi mbegu siku hizi
hazioti
maisha njia panda, mtembezi chagua pa
kwenda
uchumi vazi la bwanga, ukishuka uvishe
suspender
shiba kwa nia, ukiwa mrefu wa malengo
usikufuru we shukuru, ukifaulu kila tendo
punguza pupa, mpendaji uingie ndoani
mapenzi yamevaa bukta usiwaze, mapaji
hadharani
usilale kijinga kwenye kitanda cha ushamba
unaweza kuwa shabiki wa simba na ukaishi
mwembe'yanga
ah
hiki kijiko unachokiona, baada ya kula kwa
mkono
ndomu usiyoiona, mpaka ukishafanya ngono
neno la kuponya, lililokosa mdomo
na hili bonge la ngoma kwenu, kwangu ni kama
somo
hilo ndo wazo la leo, ishi usingizi wa furaha
mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha
Hilo ndo wazo la leo
usiishi kwa vikwazo, weka wazo kwenye vyanzo
vyako
Hilo ndo wazo
ah
underground panga tenzi, u'star hauji kwa
promo
hakuna tajiri wa mapenzi, kapuku punguza
ngono
bora uuitwe Mfalme Juha, kwenye utawala wa
kishamba
mapenzi yakikusumbua, tafuta daktari wa
kitanga
vazi unaloishi,mwenyezi yeye ndo Designer
shetani akikushawishi, mvute kwake kama Dyna
Dunia duara, jitahidi uizunguke
mla bata starehe hasara, wekeza hadhi isishuke
huna undugu na Bakhresa, ni aje aje unakula
unga?
Mateja mnahitaji sensa, taifa la kesho
linavunda
Dogo jifunze heshima, sio upaparazi
mwambie na dada ajitunze, mlango wake
asiuache wazi
kama unajijua ni mchoyo, basi usingonje
kupewa
tafuta pesa kwa moyo, sio kwa ushindi wa
ngekewa
Sharo mpe salamu, The Great braza Kanumba
Mwambie bongo sio tamu, na Lulu bado
wamemfunga
hiki kijiko unachokiona, baada ya kula kwa
mkono
ndomu usiyoiona, mpaka ukishafanya ngono
neno la kuponya, lililokosa mdomo
na hili bonge la ngoma kwenu, kwangu ni kama
somo
hilo ndo wazo la leo, ishi usingizi wa furaha
mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha
Hilo ndo wazo la leo
usiishi kwa vikwazo, weka wazo kwenye vyanzo
vyako
Hilo ndo wazo
utamu wa ndafu ya harusi, sio wa ndoa we
kilaza
mbuzi atabaki mbuzi, hata ule hadi ukasaza
nchi tayari imekonda, mwananchi tafuta ulaji
life ngumu hadi ombaomba, kidonda anafanya
mtaji
ukipata mazuri, jipange kukwepa hasara
kijana vazi la msuli, haliwezi 'kuvisha busara
ukiishi kwa hisia, kila story litakubanza
cha msingi kuweka nia, ujivunie kuwa Mtanza
(nia)
kata ya kijiji, haibebi maji ya maendeleo
katibu tunza mgwiji, msuli ukishuka kimeo
uchumi unashika tama kwenye shavu la
mlanguzi
Raia usilaumu chama, shiriki kwenye uchaguzi
unaweza kuvaa kinga, ila ukafa kwa uaminifu
mzinzi usigawe ujinga, sambaza ujumbe wa sifa
hakuna snitch kama pesa, ukiwa naye fanya
vya maana
akiondoka atakutesa, utamsaka usiku na
mchana

ah. mia