Kama hujajipanga vizuri usichokoze ujenzi

Huwa ni taabu mno
 
Gharama inaweza kuwa kubwa au ndogo kulingana na eneo ulipo, kwa Mwanza mfano, gharama ya mchanga, mawe, maji na matofali si ghali sana kama nilivyoona kwenye mchanganuo wako.
Kuna maeneo yana changamoto ya malighafi za ujenzi mpaka kero. Mfano; ujenzi nyumba na majengo kwa Wilaya ya Makete, mchanga ni changamoto sana. Unatakiwa kwenda kuchukua mchanga Makambako au Mbeya (sehemu moja inaitwa Number 1) zaidi ya kilometa 100. Gharama ya Trip moja ya Lori la mchanga inakuwa kati ya Shilingi 300,000 na Shilingi 400,000.
 
Eeeh mbona hio bei ya mchanga ni kawaida hata huku ambako kuna mashimo ya mchanga?
 
vipi ushahamia Accumen Mo hujatualika mm na mdogo angu Mshamba mwenye michongo kwenye haryuusiii 😁😁😁😁😁
 
Eeeh mbona hio bei ya mchanga ni kawaida hata huku ambako kuna mashimo ya mchanga?
Maeneo mengine mchanga una gharama ndogo sana. Mfano: Mbeya - trip 1 ya Lori la mchanga ni sh 100,000, Dodoma - Trip 1 ya Mchanga ni Sh 120,000 n.k
 
Hapana,
Sio kweli. Ujenzi kama unataka kujenga we anza na chochote ulicho nacho. Mshahara wangu haujaongezeka sana Kwa hivi karibuni lakini nimemudu kujenga ndani ya miezi 6 nyumba kubwa tu na ikaisha kabisa.

Sasa nimejiuliza miaka ya nyuma Kwa mshahara almost huo huo nilikua nafanyia nini hata sijui.

Ukiwa na mentality hizo kwamba mpaka upate kikubwa ndio uanze ujenzi utaishia kua mpangaji milele
 
Ila JF raha sana.
 
Tuseme nyumba yako kubwa imegharimu 60m. Ili uimalize kwa miezi 6 inabidi kila mwezi utumie wastani wa 10m.
Huku maisha mengine yakiendelea inabidi uwe na mshahara wa 12m kwa mwezi au sio?
 
Tuseme nyumba yako kubwa imegharimu 60m. Ili uimalize kwa miezi 6 inabidi kila mwezi utumie wastani wa 10m.
Huku maisha mengine yakiendelea inabidi uwe na mshahara wa 12m kwa mwezi au sio?
Ndo maana nimesema JF ni raha tupu. Unaweza kuta mwenzio anakunja 20m kwa mwezi. Inawezekana.
 
A
Alafu bei za kupangisha nyumba sasa ni ndogo nilivyokuwa huko nilishangaa sana juu ya hili.
 
A

Alafu bei za kupangisha nyumba sasa ni ndogo nilivyokuwa huko nilishangaa sana juu ya hili.
Ingawa huwa kuna kipindi cha neema kwenye kodi ya nyumba kama umejenga nyumba Standard. Wakati wa Ujenzi wa Mradi wa Barabara wa Njombe - Makete - Isyonje niliwahi kuwapata Wajenzi wa Barabara (Wachina) walipangisha nyumba yangu kwa Shilingi 650,000 kwa mwezi. Halafu Apartment ya Jiko, Sebule na Chumba cha Kulala chenye Choo nilipangisha kwa Shilingi 80,000.
 
Ngoja nijipange kuushtua nione nguvu zitaishia wapi
 
Wewe mzee kwanini unatufokea?

Tumekukosea nini
 
Wewe ni mhaya, au mhaya wannabe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…