Kama hujakomaa kiakili acha kuoa

Kama hujakomaa kiakili acha kuoa

Mwananchi wa chini

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
227
Reaction score
599
Moja ya dalili za mwanaume aliekomaa kiakili ni yule ambae mtakosana kwa jambo dogo lakini baadae atakupigia simu na mtaongea hatakasirika siku nzima ..

Kwa sababu anajua yeye ni mwanaume ...
wanaume wa hivyo wanajua wana mambo mengi ya kuweka akilini na sio ugomvi kati yake na mke wake ambae ni sawa mwanae niliyepewa kama zawadi na Mungu kama msaidizi wske.

Mmeamrishwa kuishi nasi kwa akili lakini Ajabu ni pale mume anapotumia nguvu nakukabiliana na mapungufu ya wake au wenza wao.

Kama hujakomaa kiakili... (huna akili) usioe. Umri,mwili mkubwa na mali zako haziwezi kukufanya kuwa mume bora kwa mke wako kinyume chake utakuwa mwanaume kwa mkeo.

Kabla ya kumlaumu mkeo kwamba hafai na niwahovyo na kwamba wanawake wote ni sawa, jiulize wewe umefanya jitihada zipi kumfanya akutii katika mambo yote,akuheshimu na kukupenda?...

Ukweli mchungu ni huu...Baadhi ya wanaume wamekuwa wakipoteza nguvu nyingi sana kumshambulia mwanamke na kuweka mapungufu ya mwanamke as if wanaume wote ni malaika.

Hili njambo ni lahovyo na linadumisha mno ustawi wa ujenzi wa familia zisizo na Amani kwa kuwa wanaume hamuambiani Ukweli hamtaki kufundishana ila mnapongezana hata pasipo stahili ili kulinda uanaume wenu.

Jambo ambalo ni tofauti kidogo kwa wanawake.
Japo hupingana lakini huthubutu kuelezana.
Hili likitokea na kwa wanaume kuna namna fulani ya sintofahamu ndoani zitapungua.

Zaidi ya yote wanaume wamekuwa walalamikaji kama ambavyo wanawake walioumizwa na wanaume washenzi wanavolalamika.

Utasikia mwanaume akiwaita wanawake wote ni mashetani, na kujinadi kwamba wameoa ili wapumzishe akili zao.
Sasa blaza utapumzisha akili gani wakati akili zenyewe za kupumzisha hauna.....
Mtaniwia radhi sana kama nimewakwaza, ila ukweli ndio huo.

Ni kweli kabisa wanawake wasumbufu wapo hilo sipingi .
Wanawake walioshindwa kulinda ndoa zao wapo na ndio hawa wanaobwata kwamba wanaume wote ni washenzi lakini tutambue kwamba hatutakiwi kuimba wimbo wa wengine wenye maumivu yao....

Chukua mmoja mwenye mapungufu mkamilishe awe bora kama unavyotaka utafuta dhana ya wanawake wote ni sawa.
Wapo wanofurahia utamu wa ndoa na mahusiano ukiwaambia hivyo watakuona chizi....

Wewe kama ulikumbana na malikia wako mkaishi poa na akaja kukugeuka mithili ya lishetani usiseme wengine kwa ujumla wao kwamba hawana maana...
Kila mmoja anacheza ngoma yake ni midundo ni tofauti pia
Nakutakia siku njema
 
Ukweli mtupu.. Si kila kitu ni cha kila mtu aisee. Kuna wengine tubaki watazamaji tu. Mimi akili ninazo tena nyingi sana ila sio za kuishi na Mwanamke 😝!!.
Most of my time natumia kujikosoa na kujirekebisha kiasi kwamba nakosa hata confidence ya kumshawishi mtoto wa watu awe mke wangu maana kila nikijipima kwenye viwango vya mume bora bado najiona nitakua "Bora mume".
Mtoa mada una hoja, ngoja wengine tukue kwanza aisee.
 
Sio baadae akupigie sim Umpigie hata wewe Maana Kama kosa ni lako still akupigie wewe Kukulamba miguu wakati wewe ndio Mwenye makosa, Akiwa kakosea yeye basi Ni wajibu wake Kujishusha ili Mambo yakae sawa

Stress zitamuua huyu dada Eti wanawake wote mashetani, Tangu lini wanaume tukaongea Lugha hii, wanawake nyie baadhi yenu ndo Mnakuwaga na kauli za Jumla kuwahukumu wanaume wote utadhani umeolewa na wanaume wa Dunia Nzima Kumbe Mshenzi ni huyo wako


Neno " ...wanawake wote ni sawa" Hii sio kauli ya Wanaume hata kidogo labda Huyo wako Usituhukumu kwa makosa ya Mtu mmoja
 
Mbona leo maada za kuoa zimekuwa nyingi humu?!
Au ndo mwezi wenyewe huu wa valentine
Sa hivi hata nikiposti uzi wa kutangaza biashara yangu ya majeneza sidhani kama uzi utapata wachangiaji
 
unatafutiwa visa valentine usipate mtoko kuwa mpole utakosa ving
 
Mwanaume mwenye akili anatakiwa amuoe mwanamke asiye na akili wataishi pamoja maisha yao yote, lakini siyo vinginevyo
 
Mbona leo maada za kuoa zimekuwa nyingi humu?!
Au ndo mwezi wenyewe huu wa valentine [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sa hivi hata nikiposti uzi wa kutangaza biashara yangu ya majeneza sidhani kama uzi utapata wachangiaji
K zimeachika nyingi ukiona hivyo au zimekula vitasa vya kutosha
 
Moja ya dalili za mwanaume aliekomaa kiakili ni yule ambae mtakosana kwa jambo dogo lakini baadae atakupigia simu na mtaongea hatakasirika siku
.
.
.
Nimechukua hii point najitahidi kuishi humu pia huwa sipendi kuyaweka makwazo sana moyoni
 
Duniani Kuna mambo mengi na muda ni mchache....
Kila mtu afate ile NJIA ANAYOONA YEYE KUWA NI SAWA.

#YNWA
 
Jinsia yako tafadhal mtoa mada,
Tuondoe kwanza iyo sintofahamu.

Kisha ndo Tuendelee na huu mjadala wetu[emoji4]
 
Chukua mmoja mwenye mapungufu mkamilishe awe bora kama unavyotaka utafuta dhana ya wanawake wote ni sawa.
Wapo wanofurahia utamu wa ndoa na mahusiano ukiwaambia hivyo watakuona chizi

USHAUR mzur Sana,
Ila Sasa mtoa mada iyo dhana yako ya "wanawake wote sio sawa"

Sisi wanaume tukiwaelezeaga kwenye mustakabali mzima wa PAPUCHI nako mmetofautiana huwa mnataka kabisa hadi kurusha ngumi.[emoji4]
 
Kuoa Ni kwa wenye akili tu wasio na akili waendelee kuwa mabachela
Naunga mkono hoja,
Ila tatizo mtoa mada naona Kama katuchanganya.

Content yake inavitu vingi Sana vya kujadili ukiachilia mbali suala lake la kuoa kwa wenye akili.

Tunatakiwa tulijadili suala lake kipengele mpk kipengele[emoji4]
 
Back
Top Bottom