Kama hujawahi kufika jiji la Tanga, basi haya ndio mambo yanayopatikana huko

Tanga ni mji ninaoupenda sana. Ukitaka kufaidi jiji la Tanga nenda wakati huu wa Ramadhan. Pale town usiku kama uko uarabuni ni uislamu mtupu. Kilichonikera ni kuna hotel moja iko katikati ya mji kwamba ukienda na demu lazima muonyeshe cheti cha ndoa. Kama sikosei inaitwa Khayrat au jina linalofanania hivyo.
 
Somehw true...sema breakfast ya buku inaweza kuwa tasty but sio muhimu...mkoa usiojali vegetables ni huu..sema ni wapish kwel kwel
 
Umesahau majini na misukule kuzagaa mitaani usiku
😅😅😅 enzi hizo tuko usagara pale usiku tunatoka manane ya usiku tuko road trip kwa miguu kuvizia vigodoro ila zaidi nilipendaga baikoko sio hivi vigodoro vya mitaani vya kishenzi yaani utamu wa tanga ipigwe ile baikoko yenyewe ya kimombasa au kizigua kidigo ujionee uumbaji watoto wa mule wana balaa zito........

Hapo ndiyo nilipo amini tanga mahaba yamezaliwa, ukipata demu wa kitanga mcheza koko ukiweka ndani ukamnyima koko ndoa kwishney 😅😅😅

Vile vile kitandani uwe njema, ukikaa wiki hujapeleka uno na ndoa kwishney anaruhusiwa binti kurudi kwao kulalamika humpi unyumba.

Wadaslam wanapiga miguu yote kwao wanaona ndo mahaba 😅😅😅

Kuhusu majini usiku na misukule haikudhuru kama haikuhusu ila usiku hatujawai kutana nayo labda wapasua nazi tanga hiyo ni warranty lazma uwakute. Nazi kupasuliwa tanga ilikuwa ni warranty na mayai viza, ila kwa sasa sijui kama wameacha.....😅
 
Mtoto wa kahana, signatory na singano mzimuni mimi ni kuchaj simu tu ilikuwa, ulikuwa CBG mpaka organic chemistry ikuumize kichwa 😅😅😅 wale wa PCM na simple harmonic yao.......

2013/2015 pale
 
Mwaka x nilienda tanga kupeleka mzigo......
Bwana eee njiani namwambia dereva wahi tushushe asubuhi sana mchana au jioni tuondoke,,,, tulifika saa kumi na moja alfajiri lile soko lilifunguliwa saa tatu na mwenye mzigo nafanya kumpigia mimi yeye hana wasiwasi dereva akaniambia hii ndio tanga usiwe na haraka. Mzigo ulishushwa saa tano.
Nilipelekwa kula supu tamu sana ya samaki kwa mama mmoja hivi nimeshamsahau... Mchana tukaletewa wali samaki wali umechanganywa na kitu kama choroko na umewekewa nazi vilinishinda wakawa wanacheka tu ilibidi twende hotel kula
 
Kodi ya chumba cha kupanga unalipa kulingana na uwezo wako ila wanapendelea sana ulipe kila mwezi (Kange kwa Masai na Kasera) wanaoishi maeneo hayo wanaelewa

Halafu hilo la daladala kupiga u turn kumfata mtu mmoja ni kawaida sana
Pia Tangamano ni soko ambalo kila Jumanne na Jumamosi ni Gulio kwa kununua vitu bei rahisi raha sana.

Kuna kibao cha KARIBU TU HAKUNA KIBAO CHA KWAHERI
 
Duu chips tu Tayali Mbona rahisi Vist Tanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…