Kama hujawahi kukutana na usumbufu, dharau na jeuri za watumishi wa serikali, utaendelea kutoona anachofanya Makonda

Kama hujawahi kukutana na usumbufu, dharau na jeuri za watumishi wa serikali, utaendelea kutoona anachofanya Makonda

Wazo zuri lakini thubutu watanzania ni wezi kuanzia viongozi hadi wananchi.

Kibaya zaidi ni dunia ya utapeli
Ndio maana ya mifumo, kwani pesa ikiingia Mpesa, Songesha inakuuliza unajisikiaje 😂😂. Wanakulamba tu. Leo hii kwanini tunampa askari tochi ya speed. Kwanini isikae system pale inacheck speed, inapiga picha, inatambua gari, na kukuwekea faini yako. Sasa tunakazana kusema askari wanaongoza kwa rushwa, tumetengeneza mazingira kwa kuongea sana
 
Na wale waliopotezwa na kuuwawa na wengine kupigwa risasi na wanamtaja Makonda?!

Na yule aliemtolea Bastola Waziri fulani na kutaka kumuua?!
Hilo halihalalishi uzembe wa watumishi wa serikali
 
Wamama wa Masai Market waliokuwa wameporwa ardhi yao na Katibu wao.Imerudi kwa wenyewe. Mzee Massawe aliyenunua ardhi milioni 26 na aliyemuuzia kiwanja kuuza kiwanja hicho hicho kwa kampuni binafsi.Mzee Massawe amerudishiwa kiwanja chake.

Mtoto aliyebakwa na Polisi kumzungusha mama wa mtoto kwa nia ya kuwalinda watuhumiwa.Wahusika wote wamekamatwa.Mtandao wa Halmashauri ya Jiji wa kula pesa umegundulika na wahusika kusimamishwa kazi.Longido pesa za afya milioni 600 wahusika wapo Polisi.Mtandao wa mashine feki Karatu wahusika wamekamatwa.Hayo ni machache ya mengi yaliyofanyika chini ya uongozi wa Makonda.
Mkuu usisahau hayo ndiyo majukumu ya mkuu wa mkoa sio hisani kwa wananchi, wala sio kazi ya ziada kwamba katumia ubunifu na akili Kuya fanya hayo.

Ndiyo majukumu anayo lipwa Kuya fanya. Kuna wakuu wa mikoa wengi wamefanya hayo yote bila kupayuka Mkuu.
 
Alipovamia nani alijeruiwa,aliuwawa au kunyang'anywa mali yake?,tumia akili unalishwa maneno unashiba
Mkuu mpaka mtu afe ndio uone kuwa ni jambo baya! Hii ni akili ya wapi!
 
Kero zipo nyingi sana haswa local goverment. Hiki kiburi kinatokea sababu hakuna anaenwafuatilia, so wanatengeza dynasty zao ili kujinufaisha. Although nqpingana na makonda kwenye mambo mengi, kwenye hili nuunga mkono. Madudu ni mengi sana
Uko na akili sana.
Kuna wengine kwa sababu ya kumchukia Makonda wanapings kila anachokifanya.
 
Mkuu usisahau hayo ndiyo majukumu ya mkuu wa mkoa sio hisani kwa wananchi, wala sio kazi ya ziada kwamba katumia ubunifu na akili Kuya fanya hayo.

Ndiyo majukumu anayo lipwa Kuya fanya. Kuna wakuu wa mikoa wengi wamefanya hayo yote bila kupayuka Mkuu.
Katika wakuu wa mikoa takribani 30 je ni wangapi wanafanya hayo anayofanya Makonda?nitajie hata watano tu
 
Ukweli ni kwamba yawezekana Makonda ana mapungufu yake kama mwanadamu mwingine yeyote. Lakini kwa kero za nyingi ya ofisini za uma hasa unapokuwa unahitaji huduma yenye viashiria vya maslahi, utazungushwa na kusumbuliwa kwa vitu vidogo sana, unapoteza muda, gharama ya fedha na gharama zingine nyingi.

Kusema kweli kuna wakati mjane mmoja alikuwa anafuatilia mirathi ya mme wake yaani amekamilisha kila kielelezo kinachotakiwa lakini ilimchukua miaka 3 kupata hiyo hela huku akienda maofisini kila wiki.

Kuna wakati unawaza kama bunduki zingekuwa zinauzwa kiholela basi wengi wa watumishi wa umma wangesha kula chuma.

Yawezekana approach ya Makonda sio nzuri kama ndivyo lakini naomba tunapomkosoa tuje na majawabu ya kuondoa hizi dharau za watumishi wa umma kwa watu ambao kimsingi ndio mabosi wao.
Kwa hio Dharau zitamalizwa na Makonda? Vipi akihama Arusha?
 
Hii mada imenigusa sana.
Kuna kipindi fulani hivi nilikuwa nafuatilia mafao yangu kwenye tawi mojawapo la PSSSF Dar.
Basi bhana nikakusanya nyaraka zote zinazohitajika nikapeleka na kama ujuavyo ukipeleka nyaraka ukifika kwanza utakutana na mtu wa mapokezi akazikagua nyaraka zangu akaona zimekamilika kisha baadae akaniruhusu nikazikabidhi kwenye ofisi iliyopo kwa ndani kwa mtu anayehusika naye akazicheki akaona ziko sawa akaniruhusu niondoke na akadai nisubirie mpunga ndani ya miezi 3 salio litakuwa linasoma.
Nilivyoondoka ikapita kama mwezi mmoja hivi siku wananipigia simu njoo unahitajika kwenye ofisi ya PSSSF nyaraka zako zina shida,nakumbuka siku hiyo nilikuwa safarini mkoa fulani kwenye kuchakarika sikutilia maanani nikapotezea hadi siku nilivyorudi dar nikawaendea kuwasikiliza nilivyofika nilikutana na mdada mmoja hivi anajiamini sana na anadharau ananiambia kirahisi tu "karatasi zako umekosea kujaza zichukue uondoke nazo ukajaze upya halafu uzilete siku nyingine" nikamuuliza unasemaje?akarudia tena "karatasi zako zimekosewa ondoka nazo ukajaze upya tena siku nyingine uzilete.
Aisee hapohapo nilijihisi mapigo yangu ya moyo yanakwenda mbio kwa hasira aisee nilimuwashia moto ofisi ilikuwa haitoshi nilimpiga maswali magumu akawa anashindwa kunijibu baadae alivyoona namzidi hoja akataka kuniitia polisi wani arrest baada ya hapo nikamwambia nipe makaratasi yangu nitapeleka kwenye ofisi nyingine hapo nilimkatisha tamaa kabisa ili kama anawaza mambo ya rushwa ajue kwangu hapati hata mia mbovu,alinipa makaratasi yangu nikaondoka.
Sasa fikiria kero kama hizi anatokea mtu wa kuzishughulikia watu wanambeza.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Shida kubwa katika nchi hii ukitatua tatizo la Mnyonge au mtu duni huesabiki kama umetatua tatizo kwasababu wanyonge hawana forum ya kutoa ushuhuda.
Wazungu sidhani kama wanatupenda na ili kujua kwamba wanatupenda kinafiki ili wapate kitu kutoka kwetu nenda kwenye nchi zao utapata ushahidi hivyo basi inawezekana kwasababu binafsi baadhi ya watu hawampendi Makonda lakini ni busara kutumia jitihada anazozifanya kurekebisha mambo iwe fundisho kwa warendaji wengine nchini kwasababu hakuna ubishi kwamba mafisadi,wezi,wala rushwa,waonezi,wavivu wanazidi kuongezeka kila kukicha inawezekana kuna mahali wamegundua pamelegea.
Makonda ameibua maeneo ya kuyafanyia kazi kama nchi.
 
Mkuu achana na huyo chizi amejaza story za vijiweni za wanasiasa. Nilichogundua asilimia kubwa ya watanzania hawatumii ubongo wao kufikiri na kutatua jambo, wanafuata mkumbo tu.
Huyo ni takataka za kina maria sarungi. Toka 2018 stori ni hizo na wanasheria wapo si wapeleke hizo evidence.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Mkuu usisahau hayo ndiyo majukumu ya mkuu wa mkoa sio hisani kwa wananchi, wala sio kazi ya ziada kwamba katumia ubunifu na akili Kuya fanya hayo.

Ndiyo majukumu anayo lipwa Kuya fanya. Kuna wakuu wa mikoa wengi wamefanya hayo yote bila kupayuka Mkuu.
Nitajie Mkuu wa Mkoa mwingine aliyefanya hayo unayoita majukumu ya Mkuu wa Mkoa?
Huo ubunifu wa kutatua kero za wananchi on the spot umefanywa na wangapi?
Makonda anajua wajibu wake kwamba ni kuwatumikia wananchi badala ya kuungwa mkono wavimba macho wachache wanapinga anachofanya.
Viongozi wakosolewe kwa kutofanya wajibu wao na waungwe mkono na kusifiwa wanapotimiza wajibu wao wa kuwasaidia wananchi.
 
Na wale waliopotezwa na kuuwawa na wengine kupigwa risasi na wanamtaja Makonda?!

Na yule aliemtolea Bastola Waziri fulani na Ben
Ben Saanane wako na Dereva wa Lisu wankunywa Mvinyo baada ya kubadilishwa Uraia wao..
 
Ukweli ni kwamba yawezekana Makonda ana mapungufu yake kama mwanadamu mwingine yeyote. Lakini kwa kero za nyingi ya ofisini za uma hasa unapokuwa unahitaji huduma yenye viashiria vya maslahi, utazungushwa na kusumbuliwa kwa vitu vidogo sana, unapoteza muda, gharama ya fedha na gharama zingine nyingi.

Kusema kweli kuna wakati mjane mmoja alikuwa anafuatilia mirathi ya mme wake yaani amekamilisha kila kielelezo kinachotakiwa lakini ilimchukua miaka 3 kupata hiyo hela huku akienda maofisini kila wiki.

Kuna wakati unawaza kama bunduki zingekuwa zinauzwa kiholela basi wengi wa watumishi wa umma wangesha kula chuma.

Yawezekana approach ya Makonda sio nzuri kama ndivyo lakini naomba tunapomkosoa tuje na majawabu ya kuondoa hizi dharau za watumishi wa umma kwa watu ambao kimsingi ndio mabosi wao.
MTU mvivu atamchukia Makonda.
 
Back
Top Bottom