Huwa nautaratibu wa kununua kila kitu cha mwezi mzima kuanzia mboga na vyakula.
Sa nikaanza relationship na ki-graduate kimoja chenyewe kinajifanya kwao mambo safi.
Kiakili kako vizuri tu na kanajitambua kimaisha.
Weakness yake ni kwenye misosi, mvivu kupika, anachojisikia kula kwa wakati huo ndio ukatafte regadless kipo ndani na kinaweza kupikwa au la;
Unakuta jioni kapika msosi fresh tu halafu badae anakuambia mi sijisikii kula hiki chakula nataka chips kuku au na mishikaki...heh maajabu
Nikaona isiwe kesi nikawa nanunua viazi hata ndoo nzima ili akisikia hamu akaange. Viazi vitaoza hapo wala hana mpango.
Vijana tuwe makini sana kwenye selection. Siko nae tena maana sio kwa nyodo zile. Mambo mengine yote yuko fresh ila hapo ndio balaa.