Kama huna Milioni 30 usimtafute Mc Gara B kwenye sherehe yako

Kama huna Milioni 30 usimtafute Mc Gara B kwenye sherehe yako

Hilo jina tu si zaidi ya laki tatu. Jina la kiuno, nani akuite kwenye sherehe yake, mwisho kwenye kumbukumbu unasikia jina hili.
 
Niliwahi kushiriki maandalizi ya harusi moja gauni LA harusi LA Bibi harusi lilikuwa halizidi laki 2 na siku amevaa waalikwa walipendeza zaidi yake. Ajabu MC alikuwa gara B na alilipwa million 3 cash.
Chakula plate moja kwa phili cake ilikuwa elf 30 akapunguza elf 29.
Sasa hii million 3 si Bora angemuita MC pilipili amlipe laki 5 tuu kuliko kupoteza hela...
Chakula cha huyu mwamba pia lilikuwa below standard ...
Harusi nzuri ni mipango tu na kupata watoa huduma sahihi ila sio kutumia gharama kubwa
 
Angekuwa brand tungemuana kwenye events kubwa kama fashion shows na international events au hata kuwa host kwenye shows za mainstream media.

Sasa yeye hata kidhungu tu kinampiga chenga afu anajiita brand kisa kawa maarufu kwa watu wa buza.
Hujamuona kule kwa tivii, kwenye kipindi cha MR RIGHT, warembo wakitafuta (wakiigiza) waume? Kila demu anasema, anataka apate mwanaume kama GALA'BIIIII!!!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Be MATURED hata kidogo please. Hata kama ni kutafuta comments SIO hivi.
ALIULIZWA HIVI:Ili Sherehe iwe nzuri inahitaji budget kiasi gani??
Ndio akasema kama sherehe itakuwa angalau na watu 200 inahitaji total cost ya Sherehe iwe 30M kwa maana ya ku cover kila KITU. Na akalezea venue set up, buffet set-up, n.k nk.... it's very reasonable kwa kuwa ukichukua wastani (Average) ya wageni 200 kwa 30M maana yake kila invitee amechanga 150K which is reasonable.

Sina any interest na GaraB lakini Kuna immaturity ya hawa Gen Z humu jukwaani Ina undermine JF.
lakini alieleta mada kacopy hyo quote kutoka page ya clouds
 
Dunia hii, haina usawa! Juzi Jumamosi, tulikuwa na harusi Mkoa mmoja kanda ya ziwa. Jumla ya michango ilikuwa 14M.
Zawadi tulitoa 3M. Mc tulimlipa 350,000/=Ukumbi 1,200,000/=. Tulikuwa na watu 246.
Watu walikula, kunywa na kusaza. Kupanga, ni kuchagua. Gharama zingine, ni za kujitakia!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Sawa kabisa! Sherehe ni kula na kunywa. Huwa nashangaa sana kwa nini watu huwa wanapoteza pesa kumlipa "msema chochote".
 
Hapo ndipo nilipoamua kwenda na mshenga wangu, nikaoa mida ya 12 jioni, mke wangu nikaweka begani, usafiri wangu uko wapi, dereva mshenga, kufika mtaani tukaingia ndani kesho asubuhi wanamuona mama mtu anafagia uwanja.
 
Haifiki
ILa ma Mc nao wamekuja na ile MC /MPIGA PICHA/MZIKI yani hao wote wanatoka kwa Gara B wanakwambia kufanya kazi na Mziki tofauti hawatoelewana pamoja na mpiga picha tofauti! Kwahiyo unakuta Mziki mil1 /picha labda package ya mil 2.5 na Mc Mil 3/4 unakuta anachukua kama mil 6/7 wanaletaga pia entertainers
 
Back
Top Bottom