Kama huna pesa nyingi weka ndani, benki zinaiba kimya kimya

Kama huna pesa nyingi weka ndani, benki zinaiba kimya kimya

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
10,509
Reaction score
16,734
Kwa uzoefu wangu wa kuwa na akaunti kwenye benki tofauti za hapa nchini na kujua vitimbi vyao nimegundua hii huduma ni kwa ajili ya wafanyabiashara wakubwa na makampuni yenye wahasibu wanaopitia kila mstari kila siku.Kinyume chake kama unategemea ujumbe kwenye simu utaibiwa vibaya sana.

Akina sisi ukishawishiwa ufungue akaunti ujue utaibiwa na hutojua kirahisi na hutopata mtetezi.Mfano una akaunti ina laki moja wakati unatafuta nyengine upeleke eti uambiwe una pesa benki basi baada miezi kama mitatu itakuwa wameshazipunguza pakubwa na mwezi unaofuata wanafunga akaunti kabisa.Ukirudi kuuliza unaambiwa ile imeshafungwa labda ufungue nyengine leo leo itakuwa tayari.

Kwani kuna shinikizo gani la kisheria au la kiuchumi kubaki na akaunti mpaka ikahakikishwa kuwa mwenyewe hatorudi tena.Na kwanii mnazifunga bila kumpigia simu angalau mara moja wakati anuwani zake zote na vitambulisho ilikuwa ni lazima wakati wa kufungua.

Mara nyengine unaweza ukaona pesa imekatwa pakubwa akaunti iko hai lakini inapumulia kooni,ukiulizwa unaambiwa hizi ilikuwa ni makato ya kila mwezi mbona nyingi sana !.Au kuna pesa on hold ,sababu za hold si pale mezani wala wahudumu makao makuu wanaozijuwa na ukiwaambia waziwachie kila mmoja anashindwa.
 
Mkuu,ukiona kiasi fulani cha fedha hakina ulazima Sana wakuzungushia kwenye biashara zako,nunua madini uyahifadhi eg.dhahabu.madini yanapanda bei kila leo,hayaozi,hayabunguliwi na wadudu,hayana garama kuyatunza.ninamiaka mitano sijawahi kupeleka fedha bank
 
Kumbuka;
Utalazimika kuwa na Kibali cha kumiliki hayo Madini.
Kila mwaka pia utalazimika kulipia Kibali hicho ili kiwe Hai.

Kinyume na hapo unaweza kuwa unatenda JKosa la jinai pasi kujua na wenye Dola yao wakikugundua ni shida.

Angalizo tu.
 
Kumbukeni akiba benki inaweza kukupa dhamana ya mkopo mkubwa zaidi
 
Mkuu,ukiona kiasi fulani cha fedha hakina ulazima Sana wakuzungushia kwenye biashara zako,nunua madini uyahifadhi eg.dhahabu.madini yanapanda bei kila leo,hayaozi,hayabunguliwi na wadudu,hayana garama kuyatunza.ninamiaka mitano sijawahi kupeleka fedha bank

Mkuu embu fafanua,nimependa hii strategy
 
Akina sisi ukishawishiwa ufungue akaunti ujue utaibiwa na hutojua kirahisi na hutopata mtetezi.Mfano una akaunti ina laki moja wakati unatafuta nyengine upeleke eti uambiwe una pesa benki basi baada miezi kama mitatu itakuwa wameshazipunguza pakubwa na mwezi unaofuata wanafunga akaunti kabisa.Ukirudi kuuliza unaambiwa ile imeshafungwa labda ufungue nyengine leo leo itakuwa tayari.
Taja mfano mmoja tu wa bank
 
Hebu fafanua vizuri hayo makato unayokatwa ili tuelewe.pia inabidi kabla ya kufungua akaunti si kuna ile mikataba ya mteja unatakiwa uisome kabla ya kusaini.tatizo wengi husaini kabla ya kuisoma hata kama itahitaji mwezi waambie bila kuvisoma vipengele vyote sitosaini nipeni muda nikaisome nyumbani nikiilewa vyema nitarejea.Kila kitu kipo wazi kabisa.pesa zako kukaa benki wewe wanakopeshwa wengine na ndiyo benki hiyo wao wanaingiza faida ile mikopo ya watu wanawalipa kwa riba.Uzuri wa pesa benki pia hata benki ikiungua au ikiibiwa sheria inalazimu wewe ulipwe pesa yako tu.ila pesa kukaa nayo ndani ni hatari kwanza yakitokea majanga ya asili kama moto.Pesa yako ikikaa benki mfano laki moja wewe walalamika inaisha.lazima iishe kuna kodi asilimia kadhaa wanakulindia kuna asilimia kadhaa ndiyo zinaorodheshwa ni riba yako.ila inabidi uangalie hiyo laki imepindukiwa na miaka mingapi, pia kila benki ina asilimia zake za riba.ngoja niishie hapa tu.
 
Ukiweka nyumbani napo utakuja ibiwa mazimaaaa

Ova
 
"Mfano una akaunti ina laki moja wakati unatafuta nyengine upeleke eti uambiwe una pesa benki basi baada miezi kama mitatu itakuwa wameshazipunguza pakubwa na mwezi unaofuata wanafunga akaunti kabisa.Ukirudi kuuliza unaambiwa ile imeshafungwa labda ufungue nyengine leo leo itakuwa tayari."[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Una mawazo mfu Kama ya wanaCCM,, you're simply a bogus like Musukuma (MP).
 
Kuweka pesa benki ni woga wa maisha. Pesa inatunzwa kwa kununua mali, mifugo na kuwakopesha maskini waizalishe.
Kuweka pesa benki kuna umuhimu sana, kwa mfano unapotaka kufanya manunuzi ya pesa ndefu mfano kununua nyumba, ardhi au gari, hauwez kufanya hayo bila benk labda kama unataka kutapeliwa na kuingia kwenye mikono ya majambazi wakati wa kukabidhiana hyo pesa!
 
Mkuu,ukiona kiasi fulani cha fedha hakina ulazima Sana wakuzungushia kwenye biashara zako,nunua madini uyahifadhi eg.dhahabu.madini yanapanda bei kila leo,hayaozi,hayabunguliwi na wadudu,hayana garama kuyatunza.ninamiaka mitano sijawahi kupeleka fedha bank
Wakati wa kununua hayo madini unatumia njia gani kulipa hiyo pesa! Bila benki hao wanaokuuzia madin hawawez kukuzunguka ukapolwa hzo pesa!
 
Kuna ile bank ina logo ya rangi ya chama pendwa walishafunga account zangu mbili sina hamu nao kabisa, wakati account yenye umri sawa na hiyo kutoka Barclays (absa) wao nilkua pia sijaitumia kwa mwaka mzima lakini haikufungwa
 
Back
Top Bottom