Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,042
- 17,320
Kuna wazazi hawataki watoto wao waongoze darasani kwa kuogopa kulogwa! Kuna watu wakichomoza katika biashara watagundua adui wake wa kwanza ni shetani baada ya kuanza kutupiwa majini na ndoto za mashambulizi usiku na nyoka/wanga/unawindwa kuuawa! Kama una ndoto za kuwa kiongozi kama ujajijenga kiroho usithubutu! Hawa viongozi kabla ya kuja kwetu kuomba kura uanzia kwenda kwa waganga wa kienyeji na kuloga wapiga kura wake kwenye njia panda na kuwalisha kwenye ndoto nyama za maiti kuingia nao maagano alafu anakuja kwenu kwenye campaign kuomba kura kwa unyenyekevu wakati kaishawamaliza kiroho! Kama hutaki kupambana usiombe kuwa mkuu idara ndo utagundua wachawi ni staff wenzako (hii inawahusu waajiriwa). Hitimisho! Jipange kupambana! Jipime nguvu zako vinginevyo utaendelea kuwa masikini na fukara na hutoboi! Huna nguvu ,za kiroho huwezi oa/olewa na binti/kijana utaishia kwa makahaba/singlemother/sugarmam. Hila nakushauri mtafute Mungu yupo wa kukusaidia lakini mtafute kwa bidii hapatikani kwa urahisi vinginevyo utaishia kwa makuhani wa shetani wanajiita manabii! Mimi na nyumba yangu tutamtumainia Bwana kwa kumtafuta na nguvu zake!