mbona kwenye nyuz za fukuza msaliti mpo namba moja kutoa matamko, ya kwamba mzinz havumiliki vp leo mmepatwa na nini?? Mi nimetoa tu kanuni na adhabu kwa mwenye kustail hy adhabu
TUSOME MAJIBU YA YESU KRISTO ALIPOLETEWA MASHTAKA DHIDI YA MWANAMKE MZINIFU KATIKA BIBLIA (INJILI YA YOHANA 8:3-11)
[3]Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.
[4]Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.
[5]Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?
[6]Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
[7]Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
[8]Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
[9]Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.
[10]Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?
[11]Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.