Bado watanzania wengi wanahitaji elimu ya hii demokrasia ya vyama vingi na hizi siasa za vyama vingi.
Lakini pia bado Watanzania wengi tunahitaji kufundishwa nini maana ya uongozi, kiongozi ni mtu wa namna gani na nini kazi yake hasa.
Wananchi wanahitaji nini kutoka kwa kiongozi na kiongozi unahitaji nini kutoka kwa kiongozi.
Watanzania pia tunahitaji sana kujua nini utumishi wa umma na nini utumishi wa chama, wakati gani unakuwa mtumishi wa umma na wakati gani unakuwa mtumishi wa chama.
Wananchi na viongozi wa umma wanapaswa kufundishwa ni nini kazi ya vyombo vya dola na nafasi yao hasa kwenye uongozi ni nini.
Vyombo vyote vya dola pia vinahaitaji sana kupata elimu ya nini nafasi yao kwa jamii na nini kazi yao kwa Taifa hili.
Wananchi na Viongozi wote tunapaswa kujua pia CCM ni chama cha siasa kama vilivyo vyama vingine, kuna CCM chama cha siasa na CCM chama kilichoshika dola, CCM kama chama dola kazi yake kuu ni kusimamia, kulinda na kutetea maslahi ya Tanzania na watanzania bila uonevu, vitisho nk
CCM kama chama cha siasa kazi yake ni kulinda maslahi ya chama chake na kutengeneza misingi yake inakayofanya kiaminike na CCM bila kutumia dola wala Kodi za wananchi.
Mwisho wa kabisa, Watanzania na viongozi wetu kwa ujumla tunapaswa kutembea tembea na kujifunza namna mataifa yaliyoendelea wanavyofanya mambo yao na kujenga mataifa yao pamoja namna ya kuongoza watu.