Kama huyu ndio msimamizi wa Uchaguzi basi tusubirie maumivu

Kama huyu ndio msimamizi wa Uchaguzi basi tusubirie maumivu

Bado watanzania wengi wanahitaji elimu ya hii demokrasia ya vyama vingi na hizi siasa za vyama vingi.

Lakini pia bado Watanzania wengi tunahitaji kufundishwa nini maana ya uongozi, kiongozi ni mtu wa namna gani na nini kazi yake hasa.
Wananchi wanahitaji nini kutoka kwa kiongozi na kiongozi unahitaji nini kutoka kwa kiongozi.

Watanzania pia tunahitaji sana kujua nini utumishi wa umma na nini utumishi wa chama, wakati gani unakuwa mtumishi wa umma na wakati gani unakuwa mtumishi wa chama.

Wananchi na viongozi wa umma wanapaswa kufundishwa ni nini kazi ya vyombo vya dola na nafasi yao hasa kwenye uongozi ni nini.
Vyombo vyote vya dola pia vinahaitaji sana kupata elimu ya nini nafasi yao kwa jamii na nini kazi yao kwa Taifa hili.

Wananchi na Viongozi wote tunapaswa kujua pia CCM ni chama cha siasa kama vilivyo vyama vingine, kuna CCM chama cha siasa na CCM chama kilichoshika dola, CCM kama chama dola kazi yake kuu ni kusimamia, kulinda na kutetea maslahi ya Tanzania na watanzania bila uonevu, vitisho nk
CCM kama chama cha siasa kazi yake ni kulinda maslahi ya chama chake na kutengeneza misingi yake inakayofanya kiaminike na CCM bila kutumia dola wala Kodi za wananchi.

Mwisho wa kabisa, Watanzania na viongozi wetu kwa ujumla tunapaswa kutembea tembea na kujifunza namna mataifa yaliyoendelea wanavyofanya mambo yao na kujenga mataifa yao pamoja namna ya kuongoza watu.
Yote hayo wanayajua sema hii nchi ilishatekwa nyara na kikundi kidogo sana na wako tayari kufanya lolote lile ikimradi wabaki madarakani na ndio maana utaona wanadharau nyingi kwa vyama vya upinzani na wananchi kwa ujumla.
 
Muda umekaribia sana wa anguko kuu la CCM hizi ni dalili tu😆😂

Kujifanya umekasirika na kwamba uko radhi kuua na kupoteza hakusaiidii chochote 😁
Wimbo wako tangu umejiunga JF
 
Najiuliza kama sisi ni exceptional mbele ya macho ya Mungu kwamba je hatutapitia mkondo wa kumwaga damu kama wenzetu? Kwa mawazo kama haya na huyu ni msimamizi wa uchaguzi!
Na huko ndiyo tunakoelekea, wameshabinafsisha nchi, kama vile sisi sote ni watumwa wao. Wewe fikiria walifuta kabila zima la wamasai hii ni record na mwenye uwezo huo si binadamu mwenzio kumfuta binadamu mwenzio
 
Mimi Hili nalijua na ndio maana siwezi enda kupiga kura huku nilijua kabisa napoteza muda wangu tu mara ya mwisho kupiga kura ilikuwa 015 na hii nilienda Kwa sababu Babu aliniambia nikampigie kura yake Kwa JPM ashudie rais wa kisukuma.
 
Mhe.waziri amenikumbusha enzi za Sadam Hussein na waziri wake jina nimesahau.
Alikuwa ni waziri wa propaganda bwana Muhammad Saeed Al-Sahhaf..

Huyu jamaa ndiye MTU pekee alibakia Ikulu ya Swadam Qussein (Sadam Hussein) wakati inatekwa lkn majeshi ya washirika yakiongozwa na Richard Amayans na Tom Fanks Moja ya makomandoo maalumu kutokea kamandi maalumu ya Bahrain ya jeshi la Marekani na Uingereza pamoja Na Ayom Sharii wa Kikosi maalumu ndani ya MOSSAD hawakufanikiwa kuona alikopitia Mpaka leo haijulikani alikokimbilia.

Baada ya siku 21 za mashambulizi makubwa na makali ya jeshi la anga la washirika Baghdad ilianguka na walinzi wa Ikulu waliuawa.

This marked the end of Saddam mpiganani atakayekumbukwa na vizazi vijavyo..

Badae aliishia kujificha shimoni na kukamatwa kama fala akapigwa kama akafa akazikwa Mpaka Sasa hajafufuka msengerema yule!
 
Mimi Hili nalijua na ndio maana siwezi enda kupiga kura huku nilijua kabisa napoteza muda wangu tu mara ya mwisho kupiga kura ilikuwa 015 na hii nilienda Kwa sababu Babu aliniambia nikampigie kura yake Kwa JPM ashudie rais wa kisukuma.
Hahahaahaha afadhali aiseee
 
Kuna koloni linaitwa Danganyika linatawaliwa na malkia toka nchi ya mbali sana ijulikanayo kama Zenjibar. Malkia huyu anatumia dola kubakia madarakani na anachota hela nyingi Sana na kuzipeleka kwao.

Hivi mlivyoifilisi Zanzibar toka 1960 na kuiuwa zaidi ya maelfu ya watu na mnaendelea kutuuwa hizo pesa unazozisema haziwezi kufidia hata roho moja ya hawa mliowauwa
 
Back
Top Bottom