Kama ilivyo kwa sanaa ya muziki na kazi nyingine za sanaa zipewe nafasi ili ziweze kukua zaidi

Kama ilivyo kwa sanaa ya muziki na kazi nyingine za sanaa zipewe nafasi ili ziweze kukua zaidi

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Sanaa ni ufundi wa kuwasilisha fikra na mawazo ya binadamu kwa njia aidha ya kuchora, kuchonga, uandishi, upambaji, mitindo, ufinyanzi, uimbaji, Uigizaji na vitu vingine vifafananavyo na hivyo, ni hali ya kuyapa umbo au (kibebeo) mawazo ili yaweze kufika kwa hadhira ili aidha kuelemisha, kuburudisha, kuonya au kuweka kumbukumbu ya jambo fulani.

Kazi zote za sanaa kwa ujumla wake zina lengo moja la kufikisha ujumbe au mawazo ya msanii husika. Pamoja na umuhimu huo wa kazi za sanaa lakini pia kazi za sanaa zinaweeza kutatua changamoto ya Ajira kwa vijana au kwa mtu yeyeto anayefanya kazi ya sanaa.

Baadhi ya faida za kazi ya sanaa:
  • Kuongeza kipato
  • Kutunza na kukuza Lugha
  • Kutoa ujumbe wenye lengo fulani( kuonya, kuelimisha na kuburudisha)
  • Kuongeza misamiati
Pamoja na mazuri hayo ya kazi za sanaa bado sehemu kubwa ya kazi hizi hazipewi uwanja wa kusambaa au kufika mbali ili kuibua au kukuza vipaji vingine kwa ajiri ya kuinua vijana kujikwamua kutoka lindi la umasikini. Kama kazi hizi zingepewa uwanja sawa zitapunguza changamoto ya ajira katika jamii zetu.

Jamii zetu kwa sasa kwa kiasi kikubwa zinaendeleza zaidi sanaa ya Muziki na kusahau kuendeleza na sanaa nyingine kwa nguvu ileile kama itumikayo katika sanaa ya muziki.

Baadhi ya Changamoto iwakutayo wasanii wanaofanya sanaa nyingine

  • Kukosa ufadhili
Pamoja na changamoto hii kuwakumba wasanii wa nyanja zote lakini wasanii wanaofanya sanaa tofauti na muziki hukutana na changamoto zaidi kutokana na imani haba kwa wafadhili kuhofia kutorudi kwa mitaji watakayotumia,(kukosa faida)
  • Kukosa majukwaa kuwasilisha kazi zao
Wasanii hukumbana na changamoto ya kukosa majukwaa kuwasilisha kazi zao kutokana na ukosefu wa pesa kulipia muda wa hewani ili kazi zao zitangazwe na vyombo vya habari, lakini pia kutokuwepo kwa matamasha ya kutosha yanayohusisha sanaa tofauti na uziki.
  • Sera zinazorudisha nyuma juhudi za wasanii
Kuna baadhi ya sera zinawanyima wasanii fursa ya kufanya kazi zao ziende mbali, mfano kulipia "blogs" na vitu kama hivyo vinawanyima wasanii fursa maana kimsingi wanakuwa hawana uwezo wa kulipa na hivyo kubaki na kazi zao.

Ni wito wangu kwa vyombo vya habari vijitahidi kutangaza kazi zingine za sanaa ili wasanii wanaojitahidi kufanya kazi hizo waweze kupata kipato na pia sanaa iweze kufika mbali ili kutatua tatizo la ajira katika nchi yetu.

Pia Baraza la sanaa liwe bega kwa bega na wasanii katika kutatua changamoto za wasanii kama wizi wa kazi zao, kuhakikisha wanapata hati miliki na pia kuwaelekeza njia nzuri ya kuwasilisha kazi zao na si kusubiri wakosee na kuwapa adhabu tu.
 
Back
Top Bottom