Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Nilichojifunza hapa Tanzania, ukidhamiria kufanya jambo fulani, ukalipa jitihada za kutosha na fedha , lazima jambo hilo lifanikiwe.
Kwenye moja ya sehemu ambayo kwa macho yangu nimeshuhudia hilo ni ujenzi wa madarasa zaidi ya 12,000 tena kwa viwango vizuri sana uliofanyika kipindi hiki cha Awamu ya Sita. Ndani ya miezi 3 tu, taifa limeshuhudia operesheni yenye mafanikio zaidi ya asilimia 95 ya ujenzi wa madaraka kwa ajiri ya watoto wetu kwenye viwango vya juu kabisa vya ubora!
Moja ya maeneo ambayo kwa Awamu zote 5 za nyuma Taifa hili tumekwama ni suala la kupima na kupanga miji na maeneo yetu
Jambo hili limekuwa likifanya Taifa letu kuonekana la hovyo kutokana na watu kujilimia na kujenga hovyo kila kukicha!
Leo hii ukitoka Manyara kwenda Arusha maeneo ya Tarangire unashuhudia ujenzi holela wa nyumba hadi kwenye eneo ambalo ndo yalikuwa mapito ya wanyama. Kilimo pia kinafanyika kwa kasi kwenye maeneo haya.
Leo hii ukienda Mwanza, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro, Songwe, Tanga, Dar es Salaam, Morogoro na mikoa mingi unaona Jinsi watu wanavyozidi kujenga kila siku bila mpangilio, Wengine wanajenga hadi maeneo ya hifadhi jambo litakaloleta hatari kubwa sana huko mbeleni maana kwa Jinsi watu wanavyozidi kuongezeka Tanzania, itafika wakati Taifa zima litakuwa squatters
Naomba serikali ya Awamu ya 6 ijiondoe kwenye dhambi hii! Watanzania wa sasa wana uwezo wa kujenga nyumba Nzuri tena sana na hili limeonekana hadi maeneo ya Dodoma yaliyopangwa na kupimwa vizuri. Kinachotakiwa kufanyika kuanzia sasa ni Serikali kuweka nguvu kubwa sana kwenye kupima na kuyapanga, maeneo yote na miji yote ya nchi hii na Kuhakikisha kila sehemu inaendelezwa na kulimwa kimpangilio.
Hakuna gharama kwenye kupima na kupanga miji yetu na Tanzania nzuri Kama Dubai , Texas, New York inawezekana
Naomba kuwasilisha!