Kama Iran hawakumuelewa Netanyahu, Walitakiwa kumuelewa rais wao mstaafu Mahmoud Ahmadinejad. Israel iko kila kona Iran

Kama Iran hawakumuelewa Netanyahu, Walitakiwa kumuelewa rais wao mstaafu Mahmoud Ahmadinejad. Israel iko kila kona Iran

ukipenda kula shartiuliweeee

tutajibu kwa wakati wetu na kwa mda muafaka.
Shikamooo Neta

Nachopende neta akiwa anakupiga anakujuza kaa mbali na wananchi wako

Usipotiii anawapitia kama upepo na anapiga palepale alipoona mpo maraa tiii

Mkuu hamasa kaenda

Mara tii katibu kaenda


anaefwata n huyu raisi wa Iran niko pale kwa masawe na Al jazmoshi yangu
 
Netanyahu juzi amesema mkono wa IDF unafika kila kona Iran.
Nimeangalia interview moja kati ya Rais mtaafu wa Iran Ahmadinejad na CNN -Turk, anathibitisha Mossad wametapakaa kila kona Iran.

Anasema Iran Ilianzisha kikosi maalum cha kijasusi kupambana na Mossads waliojipenyeza Iran. Cha ajabu walikuja kugundua mkuu wa kikosi hicho ni jasusi nguli la Mossad, na wanakikosi zaidi ya 20 nao ni maajent ywa Mossad. Kikosi hiki kilikuwa ni cha hadhi ya juu sana, kilichofanywa vetting ya juu sana.
Hayo waligundua baada ya wababe hao kumaliza misheni yao kuua wanasayansi, na kuibq documents nyingi za miradi ya nyuklia na kukimbilia Israel.

Hii story inawafanya wairan na mawakala wake kuwa uchi leo zaidi ya zamani mbele ya Israel.

Baada ya mabomu 200+ kurushwa Nimemuona Netanyahu anaongea huku anatetemea, hadi ikabidi mchukua video amzoom ili kumficha mikoni, huku wakiahidi kulipa kisasi kwa wakati muafaka na kishindo muafaka.

Makombora yalikuwa na kasi kubwa kiasi kwamba Muda yaliyotumia kufika Iran ni mfupi kuliko muda wa ndege za kivita kutoka Israel kufika iran na kurudi Israel. Rais wa Iran anasema hilo ni funzo kuwa Israel itakapotuma ndege ijue kabla hazijaanza kurudi zitakuta Israel imeshateketea.

Jambo ambalo wakubwa hawa hawajui, Israel inauwezo wa kuwashambulia kwa mfumo wa trojanhorse. Yaani wakati unategemea ndege, kumbe huko ndani yako jamaa wamo kitambo na kwa staili ya ajabu wakawaumiza kuliko wanavyokusudia.

Poa sababu za iran Kuishambulia Israel hazina mashiko. Hakuna ushahidi kuwa waliomuua kiongozi wa Hamas walikuwa ni Israel. Kuuwawa kwa Kiongozi wa Hamas ni suala la Lebanon sio Iran. Hivyo Israel inajipa uhalali kwa kufanya itakavyo kulipa kisasi maana kimsingi imeshambuliwa na kuchokozwa sana.


Tuombe amani, ila tutarajie jibu la kisayansi sana lenye uchungu mkubwa sana kwa wapenzi wa Iran.


Ni hayo tu.

Mtumishi Matunduizi.

View: https://youtu.be/AbfgOx3wnfg?si=-3wjamHNvrX-6d-2
 
Iran anajua kuna gharama ya anayoyafanya na ameshakubaliana na hiyo gharama, anajua nguvu ya anaopigana nao, amechagua kutokuwa mnyonge na kujishusha amechagua kuwa na msimamo hata kama utamcost.

Kuna mahala unafika Enough is enough na unakuwa tayari kwa lolote, Iran kaamua lolote na liwe na hahitaji huruma ya yeyote.
Ameamua kusimamia anachoamini bila kuyumbishwa na mtu yeyote.

Iran wameishi na vikwazo miaka mingi kutokana na misimamo yao na bado wanavikwazo vingi lakini hawajali wameamua kusimamia wanachokiamini.
 
Jambo vita ni mbaya ila bila kupigana hawataheshimiana maana diplomasia imeshindwa kuweka utulivu mashariki ya kati.

Miaka nenda miaka rudi, tunasikia kelele zao tu za kutunishiana misuli na uchokozi wa rejareja wa kutupiana silaha. Sasa waachwe tu. Wapigane mpaka pale wenyewe watakapoona inafaa kuacha mapigano. Watakaa na kufanya tathimini ya uamuzi wao wa kuingia vitani (faida na hasara). Halafu baadaye watajua namna bora zaidi ya kushughulikia tofauti zao. Kutia ndani na kudanganywa na watu wengine ili wapigane.
 
Miaka nenda miaka rudi, tunasikia kelele zao tu za kutunishiana misuli na uchokozi wa rejareja wa kutupiana silaha. Sasa waachwe tu. Wapigane mpaka pale wenyewe watakapoona inafaa kuacha mapigano. Watakaa na kufanya tathimini ya uamuzi wao wa kuingia vitani (faida na hasara). Halafu baadaye watajua namna bora zaidi ya kushughulikia tofauti zao. Kutia ndani na kudanganywa na watu wengine ili wapigane.

Tatizo Kuna vizabi zabina vinaiingilia ..

Undumila kuwili wa Magharibi dhidi ya Iran nani asiyeuona?
 
Nimeusoma uzi vizuri sana, sijaona kama mwandishi kaweka mahaba ya kidini au kazungumza kuhusu uwezo wa nani ni mkubwa; kama nimemuelewa vizuri, mleta uzi ni kwamba kwa maana ya upataji taarifa kati ya nchi hizi 2, Israeli na Iran then Israeli yupo juu zaidi cause most of senior officials wa security system wa Iran ni mapandikizi ya Mossaid. Sasa issue ya uwezo kati ua Russia na USA na Israeli umeiona wapi kupitia uzi hu?
 
Kile kijirais cha Iran kilichouliwa na Israel hayakuwa maslahi ya Iran? 😂🤣
Aliyekua maslahi ya Iran amelipiwa kisasi chake ndege zote zilizoruka kumuua na na command center ni majivu saiv
 
Basi ni kwamba Iran inajua kila mpaka kuuliwa kwa Rais wake ,halafu ishu ya kufa kwa viongozi pale ni kawaida ...Iran karusha mabomu yale kulinda heshima tu basi ili Israel asizidi kumdharau ila alikuwa hana mda wa kulipiza .

Iran analenga sehemu za majeshi sio wananchi wasiokuwa na hatia , usichokijua Utawala wa Iran na israel wote wamekalia kuti kavu ...Netanyhulu analinda kibarua chake kwa shinikizo la wtu la bado kuwa watu wanampinga , vivyo hivyo kwa Iran ndio maana Netanyuhlu anatumia propaganda za kumchafua kiongozi wa Iran ili kuungwa mkono na wairan .

Hii ngoma ni mbichi wale wanamjua israel ....Israel ana nafasi moja tu ya kummaliza Ayatollah ijumaa ijayo maana ataongoza sala kubwa hapo Iran ....Atakuwepo hadharani kumbuka jamaa alishawahi kushambuliwa enzi za urais ndio maana mkono wakee mmmoja haufanyi kazi .....
Ajaribu hio move uone nin kitatokea pale mido east kuua sio shida US anaweza kuua yeyote pale Iran lakin yuko makini mno. Alijaribu kwa Suleiman nadhani hawezi fanya tena ijekua kiongozi Mkuu wa mamlaka ya Iran ni bora uue rais wao wanaweza kupapasa tu wakamuacha
 
Israel fanya waarabu wapelekewe moto. siwapendi wayahudi lakini haizidi waarabu. ugomvi wangu na waarabu ni mentality yao ya kuona weusi kama slaves. wakibadilika hilo sina tatizo nao.
chondechonde tu Israel msije ikatokea mkamalizana na hao mkaja kuitwanga tu Qatar napopatia rizki.
 
Poleni sana 1=3 endelezeni ndoto zenu kuliota shetani lenu takatifu ndio lilimpotexa Paulo kwenye njia panda ya Jerusalem to Damascus chini ya mti wa mkunazi. Israel hawezi kupigana na Iran acheni kujidan'gan'ya.

Leo mmeingiza ground force mkakimbia kipigo cha kuchungulia tu Lebanon wawili wamekufa na 18 wamekimbizwa Hospital.


View: https://youtu.be/X2mi5DC9Yi0?si=0i0kftKD7t3WP7Lg
 
Jinsi toka jana nyuzi za Iran na Israel zilvyojaa, kwenye gahawa watanikoma ntavyokuwa nashusha nondo
 
Nimeusoma uzi vizuri sana, sijaona kama mwandishi kaweka mahaba ya kidini au kazungumza kuhusu uwezo wa nani ni mkubwa; kama nimemuelewa vizuri, mleta uzi ni kwamba kwa maana ya upataji taarifa kati ya nchi hizi 2, Israeli na Iran then Israeli yupo juu zaidi cause most of senior officials wa security system wa Iran ni mapandikizi ya Mossaid. Sasa issue ya uwezo kati ua Russia na USA na Israeli umeiona wapi kupitia uzi hu?

Kuongelea kadhia ya mashariki ya kati ukamsahau Marekani kuwa ndiye mwenye lake jambo ni kutojitendea haki mwenyewe.

Kama ilivyo Hezbollah, Houthi au HAMAS kwa Iran; ndivyo ilivyo Israel kwa Marekani.

Hata ndondi si ni kwa uzito?

Marekani saizi yake warusi; Israel wake Iran; zichapwe kavu kavu heshima iwepo:

Undumila kuwili wa Magharibi dhidi ya Iran nani asiyeuona?

Au wewe huoni hivyo?
 
Back
Top Bottom