Kama jibu hili la kipuuzi alilolitoa Rais Chakwera wa Malawi ndizo akili za Wapinzani wengi Barani Afrika, ni bora Vyama Vikongwe vitutawale milele

Kama jibu hili la kipuuzi alilolitoa Rais Chakwera wa Malawi ndizo akili za Wapinzani wengi Barani Afrika, ni bora Vyama Vikongwe vitutawale milele

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Ndiyo maana sijutii na kamwe sitokuja Kujutia kuwa mwana CCM Chama ambacho ni 'Kikongwe' kabisa nchini Tanzania kutokana na kwamba Wapinzani wengi Barani Afrika nimegundua japo wakiwa hawajapata Madaraka na Kushika 'Dola' huwa wanatuaminisha Watu tuliochoka na 'Mifumo' Kandamizi iliyopo na 'Umasikini' lakini na Wao wakiwa 'Uongozini' hufanya 'Upuuzi' maradufu ya walioukuta

Leo nilikuwa nimepanga kabisa Kutizama Mahojiano kati ya Mtangazaji Mahiri ambaye Kwangu Mimi ni 'Critical and Great Thinker' wa 'Kutukuka ' kabisa Shaka Ssali wa Voice of America akiwa na Rais wa Malawi Bwana Lazarus Chakwera aliyetokea kwa Wapinzani na ambaye Waafrika wengi wasiovipenda Vyama Vikongwe viendee 'Kutawala' walimpenda ila 'alichokijibu' nilijikuta napandwa na Jazba na kuacha kabisa Kumtizama na Kumsikiliza

Hili ni Swali la Kawaida tu ila lenye Mitego mingi ndani yake aliloulizwa na Mtangazaji Shaka Ssali...
Mheshimiwa Rais Chakwera wakati wa harakati zako pamoja na Kampeni zako ulitokea Kuzikonga sana Nyoyo za Wamalawi na hata Waafrika wengi hasa kutokana na Misimamo yako na nakumbuka mara kwa mara ulisema ukiwa Rais utawapenda Wamalawi wote bila kujali kama walikupigia Kura au hapana ili kuleta Umoja. Je, Mheshimiwa Rais Chakwera imekuwaje ulipoapishwa tu kuwa Rais 98% ya Wateule wako ni ama Ndugu zako wa Damu au wa Mkeo au ni Marafiki zako wa karibu mno?

Lifuatalo hapa chini ni Jibu la Mheshimiwa Rais wa Malawi Lazarus Chikwera ambalo sioni aibu ( haya ) kuliita ni la 'Kipuuzi' pia
Nashukuru kwa Swali lako zuri Shaka Ssali ila Jibu langu Kwako ni rahisi sana tu. Nimeteuwa Wasaidizi wangu kuanzia Mawaziri pamoja na Waandamizi wengine Serikalini kwakuwa ningekuwa ni Mwendawazimu Kuteua Mawaziri kutoka katika Maeneo ambayo hayakunipigia Kura na hata kama walinipigia basi zilikuwa ni Kidogo halafu niwaache wale ambao ndiyo walinipigia Kura nyingi. Siku zingine watajifunza kwani hata Mimi pia ni Binadamu siwezi Kuwapenda Watu wasionipenda au wasioniunga mkono.

Kwa 'Upuuzi' huu wa Rais Chikwera na Wapinzani wengine Barani Afrika nasema ni Heri Vyama Vikongwe kama CCM viendelee Kushika Hatamu tu.
 
Magufuli alipoenda Arusha na Kilimanjaro alitangaza kuwasamehe wapiga kura kwa kuwa hawakumchagua kwa wingi.

Mwanza wakasamehewa kubomolewa nyumba zao zilizotakiwa kubomolewa kupisha upanuzi wa airport sababu wao ni wapiga kura wake.

Huku Afrika kwa ujumla kama mshindi wa urais asipokuwa na moyo wa kusamehe Kama Magufuli akiingia Ikulu ni kiama kwa wasiompigia kura.
 
Utupe na alichofanya Magu kama aliteua toka maeneo ambapo hakupata kura

Nitajie Kwanza hayo maeneo ambayo kwa mujibu wako Wewe Rais Dkt. Magufuli hakupata Kura na pia hajateua Watu kutoa hayo Maeneo husika.
 
Kwa hiyo ulitaka ajibuje ili apatie? Unajua wakati wa utawala wa Peter Mutarika Chakwera ali treatiwaje?

Unataka kuniambia LISSU akiwa rais kuna siku atakaa na kuisifia CCM au JPM?

Ukiwa jukwaani unaweza tamka mambo ambayo ki uhalisia moyoni yapo tofauti na yanayotoka kinywani. GADAMN
 
Magufuli alipoenda Arusha na Kilimanjaro alitangaza kuwasamehe wapiga kura kwa kuwa hawakumchagua kwa wingi.

Mwanza wakasamehewa kubomolewa nyumba zao zilizotakiwa kubomolewa kupisha upanuzi wa airport sababu wao ni wapiga kura wake.

Huku Afrika kwa ujumla kama mshindi wa urais asipokuwa na moyo wa kusamehe Kama Magufuli akiingia Ikulu ni kiama kwa wasiompigia kura.

Nikiichukua sababu ya Rais wa Malawi Chakwera na Kiongozi wa Upinzani nchini Uganda Dkt. Kiiza Besigye aliyoitoa leo 'siwaamini' tena Wapinzani.
 
Kwa hiyo ulitaka ajibuje ili apatie? Unajua wakati wa utawala wa Peter Mutarika Chakwera ali treatiwaje?

Unataka kuniambia LISSU akiwa rais kuna siku atakaa na kuisifia CCM au JPM?

Ukiwa jukwaani unaweza tamka mambo ambayo ki uhalisia moyoni yapo tofauti na yanayotoka kinywani. GADAMN

Sasa kama Watu walidhani Wapinzani ni Darasa tosha la Demokrasia lakini kumbe nao wakipewa 'Dola' ni walewale kwanini akina CCM wasitawale?
 
Sasa kama Watu walidhani Wapinzani ni Darasa tosha la Demokrasia lakini kumbe nao wakipewa 'Dola' ni walewale kwanini akina CCM wasitawale?
CCM iliwapa lini wapibzani nafasi ya kutawala nchi wakawa vile vile ki democrasia? CCM wapo imara kwa sababu wanasajiri vijana wanaopenetrait ndani ya serkali kwa maelekezo ya kulibda chama( UVCCM TO TISS)
 
'wanaopenetrait' na 'kulibda' ndiyo Viswahili gani hivi? Sasa kama Kuandika tu vyema kwa Lugha ya Kiswahili hamuwezi je, kuitoa 'CCM' mtaweza?
 
Ni jibu la kijinga.

Sijisikii hata kuelezea alitakiwa kujibuje ila ni jibu la kijinga na la kipuuzi.
 
Kwani kule jimboni kwa Mbunge mstaafu maarufu kama bwege walijibiwa nn juzi na mtu ambaye anasisitizaga maendeleo hayana chama.
Hakuna utofauti na alichojibu Chakwera
 
Back
Top Bottom